Wajibu wa kuendesha elimu kwa Wapigakura unaweza kupatikana kutoka kwa vyanzo mbalimbali, kwa mfano kupitia kwa sheria au kauli ya maazimio. Zaidi ya wajibu huu, hata hivyo, wale wanaowajibikia elimu kwa Wapigakura watata kujadili malengo na mipaka ya Mpango fulani mahususi wa elimu kwa Wapigakura na wale wanaoshiriki katika mchakato huo, pamoja na wasimamizi wa uchaguzi, wagombezi wa uchaguzi na mashirika ya kijamii. Kila mojawapo wa makundi haya yana jukumu la kutekeleza katika mchakato mzima na, kutokana na hayo, watakuwa na nia au haja katika juhudi za elimu kwa Wapigakura.
Sehemu hii inajadili kila mojawapo wa washika dau hawa, inaangalia majukumu yao katika kuhakikisha kuwa shughuli yenye ushindani mkudwa – kutwaa mamlaka waliyopewa na umma – pia ni shughuli shirikishi, na kisha kupendekeza namna ambavyo malengo na mipaka ya elimu kwa Wapigakura yanaweza kuendelezwa katika hali fulani mahususi.