Wapigakura na wananchi hawapatikani pekee yao kama watu binafsi katika ombwe tupu. Na pia vyama vya kisiasa si wawakilishi wao wa kipekee katika uwanja wa kisiasa. Eneo hili la mada litachunguza istilahi “mashirika la kijamii”. Huku sehemu hii ikishughulika na umuhimu wa mashirika la kijamii kuhusika katika mchakato wa kuunda, kutekeleza na kutathmini Mipango ya elimu kwa Wapigakura, pia itajitokeza na ufafanuzi wa kutumika katika matini haya kuhusu “mashirika la kijamii”.
Shirika la kijamii: Ufafanuzi Unaotumika hapa
Sehemu hii itafuata mtazamo wa kijumla na mpana kwa dhana ya “shirika la kijamii”. Hasa, inafuata ufafanuzi mpana wa “shirika la kijamii” ulioelezwa na Larry Diamond:
uwanja wa maisha ya kijamii yenye mpangilio ambao ni wa hiari, unaojiendeleza wenyewe, (kwa wingi) unaojitosheleza, wenye uhuru kutoka kwa serikali, na unaotawaliwa na utaratibu wa kisheria au fungu la kanuni za pamoja. Ni tofauti kutoka kwa jamii kwa ujumla kwa kuwa unahusisha wananchi wanaofanya kazi kwa pamoja katika umma ili kuwasilisha matamanio, mapenzi na mawazo, kubadilishana habari, kutimiza malengo ya pamoja, kutoa matakwa kwa serikali, na kuwataka maafisa wa serikali kuwajibika…haihusishi…juhudi za kisiasa za kuchukua mamlaka ya kiserikali.
[1]
Katika maneno mengine, mashirika ya kijamii yanahusisha miungano au makundi mbalimbali na mashirika wanachama ambayo yanawaleta wananchi pamoja kufanya kazi katika Nyanja za kisiasa na kisera. Haiwezi kutenganishwa na sekta ya kibinafsi, kama inavyofanywa wakati mwingine, kwa sababu bila shaka itahusisha makuundi yenye haja za kibiashara na kiuchumi. Pia mashirika ya kijamii hayawezi kujadiliwa kama sekta huru, kwa sababu inaweza kudhihirisha miegemeo mikubwa. Hata hivyo, inaweza kutazamwa kuwa kundi kubwa linaloleta pamoja matamanio na raslimali ambazo, zinaweza katika nyakati muhimu katika historia ya nchi, kuendeshwa katika hali ya kuendeleza malengo fulani ya kijamii.
Kwa sababu zilizodhamiriwa humu, waandishi watatahadharisha dhidi ya matumizi ya istilahi ambayo itaashiria maana ya kimtazamo. Katika matumizi yake mengi, uchukulio ni kuwa mashirika ya kijamii ni kwa ajili ya maendeleo, au yana sera ya kijamii ya kuwanufaisha masikini na watu wasiojiweza, au yana mtazamo mahususi wa mahusiano ya kijamii na kiuchumi. Wakati ambapo inatumika namna hii, hata hivyo, dhana hii inaweza kuzua ubishani, hasa wakati inapotumika katika muktadha wa uchaguzi. Katika mazingira ambapo utawala wa kisiasa au kiuchaguzi yanadhamiriwa kupunguza ushindani wa kisiasa, matumizi ya kimaoni au kimtazamo ya dhana “mashirika ya kijamii” yanaweza kusababisha kutengwa kwa mashirika ya kijamii kutoka kwa kampeni na uchaguzi kwa ujumla.
Uhamasishaji wa Mashirika ya Kijamii Wakati wa Uchaguzi
Uchaguzi ni mojawapo wa shughuli zile muhimu ambapomashirika ya kijamii – kwa sababu ya raslimali yake, hali yake ya kujitolea, ujuzi wake mpana, na uwezo wake wa kufikia sekta zote za jamii – yanafaa kuhamasishwa na, pale inapowezekana, kuendelezwa katika hali ya kukuza shughuli za kielimu zisizokuwa na mwegemeo.
Makundi haya huenda yasiwe na shughuli za kisiasa au kiuchaguzi kama au hata za kielimu kama malengo yake ya kimsingi. Kutokana na hayo, yatafaa kujadili masuala yoyote ya kisiasa na wanachama wake. Aina za makundi haya zinahusisha miungano ya wafanyikazi, makundi ya kijamii, mashirika ya kibiashara na kitaalamu, na hata makundi ya kidini.
Kunaweza kuwa na mashirika na miungano mingine ambayo kwa pamoja yanaunga mkono uchaguzi fanifu lakini itabakia huru kutoka kwa wagombezi na kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi. Baadhi ya makundi haya yanaweza kuwa na wajibu mahususi katika michakato ya kisiasa na kiuchaguzi, kama vile mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika na elimu kwa raia na Wapigakura, uhamasishaji wa umma, uchunguzi wa uchaguzi na uhesabu sambamba wa kura, na haki za binadamu. Mfano mmoja maarufu wakundi kama hili katika Marekani ni Muungano wa Wanawake Wapigakura.
Pamoja na hayo, labda kutakuwa na makundi mbalimbali ambayo yataendesha elimu kwa Wapigakura na uhamasishaji wa Wapigakura unaoelekezwa kimsingi kwa wanachama wao. Wanachama kama hao wanaweza kuhusisha vijana na wale wanaopiga kura kwa mara ya kwanza, wanawake Wapigakura, jamii ndogo, jamii za mashambani au zisizoweza kufikiwa kwa urahisi, Wapigakura walemavu, na wakimbizi wa ndani kwa ndani au wakimbizi wanje. Baadhi ya Wapigakura hawa wanaweza kuwa katika hatari kwa sababu ya wao kukosa habari, huruma, hali ya kuhisi kutengwa kutoka kwa taasisi na michakato iliyopo, au uwezekano wa kutumiwa vibaya.
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Mashirika ya Kijamii
Matumizi ya dhana sekta ya Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali pamoja na mashirika ya kijamii, na hali ya baadhi ya viongozi katika Mashirika Yasiyokuwa ya Kijamii kuchukua nafasi ya wasemaji wa mashirika ya kijamii, hayafai kutatiza waelimishaji na wasimamizi wa uchaguzi kuhusu tofauti kati yao. Bila ya kujua namna ambavyo Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali yanavyoonekana kuwa, kwa kweli mashirika haya ni sehemu ndogo ya kile ambacho kinajulikana kwa upana kama mashirika ya kijamii.
Mashirika ya kijamii kwa upana yanahusisha miungano ya kila aina amabyo imeshatajwa. Lakini waelimishaji huenda wakataka kuzungumzia kwa undani makundi yote katika nchi yao. Baadhi ya mengine, kama vile ya kimichezo na vilabu vya kijamii au makundi ya ushirika na mikopo yanaweza kuwa makundi yasiyozingatiwa na yasiyochaguliwa moja kwa moja kuendeshea elimu kwa Wapigakura. Hata hivyo, wanachama wa makundi haya yanaweza kuwasilisha mitazamo yote ya kisiasa na hivyo kuwa raslimali muhimu isiyo na mwegemeo ya kuendeshea Mpango wa elimu kwa Wapigakura.
Kupanga Mashirika ya Kijamii
Inafaa kuwa rahisi mno kuwasiliana na wasimamizi wa uchaguzi wa kitaifa, au katika uchaguzi wa mashinani, wasimamizi wa uchaguzi wa manispaa, kuhudhuria mkutano wa kubadilishana mafunzo kuhusu shughuli za elimu kwa Wapigakura na, pale panapowezekana, kuwashirikisha. Inafaa vilevile kuwezekana kufanya mialiko sawa na hiyo kwa vyama vya kisiasa, miungano, au makundi yenye shughuli maalum kwa kutumia raslimali kama vile orodha ya vyama vilivyosajiliwa (aidha vilivyosajiliwa na wizara ya sheria au tume ya kitaifa ya kusimamia uchaguzi, kwa mfano) au orodha ya vyama vilivyo na viti katika bunge la kitaifa. Pia inawezekana kuhimiza wagombezi kukutana pamoja kushirikisha juhudi zao za pamoja wakati wa uchaguzi.
Lakini wakati inapokuja kwa mashirika ya kijamii, inaweza kuwa vigumu zaidi kupata orodha kamilifu ya makundi yasiyo rasmi au makundi huru ya wananchi. Na hata si yote ambayo yatakuwa na haja katika kutoa usaidizi. Na, miongoni mwa makundi ambayo huenda yakawa na nia. Huenda yasifahamiane au yakakosa kuwa na uzoefu wa awali wa kufanya kazi pamoja. Kutokana na hali yake halisi, mashirika ya kijamii hayawezi kushirikishwa kupitia kwa baraza fulani. Sehemu mbalimbali za mashirika ya kijamii yanaweza kusawazishwa na, kwa kutumia mashirika ya katikati, baadhi yao yanaweza kuhimizwa kujipanga vizuri zaidi kwa minajili ya Mpango fulani mahususi wa elimu kwa Wapigakura.
Hatua mbalimbali zinaweza kuchukuliwa kufahamisha na kusaidia makundi ya mashirika ya kijamii na hata kushirikisha juhudi zao katika kusaidia uchaguzi. Hatua hizi ni pamoja na mikutano ya mara kwa mara kufahamisha makundi (kwa mfano kuhusu mabadiliko yanayoendelea katika kampeni za uchaguzi kama vile matumizi ya kanuni mpya au taratibu mpya za uchaguzi au teknolojia) na kuendeleza ushirikiano na ushirikishi; vipindi vya mafunzo kuwaandaa wale wenye jukumu la moja kwa moja katika kuwashirikisha Wapigakura; taarifa fupi za mara kwa mara kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi; maswali yanayoulizwa mara kwa mara ambayo yanasambazwa kupitia kwa kipepesi au barua pepe, na shughuli zingine kama hizo na zinazonuiwa kuleta umoja na uelewano.
Washika dau katika Elimu kwa Wapigakura
Kuchukulia mashirika ya kijamiikama washika dau katika shughuli ya ukuzaji wa shabaha, malengo, na mipaka ya Mpango wa elimu ni muhimu. Mashirika haya yana uwezo wa kutoa habari za haraka na za kutegemewa kuhusu Wapigakura. Pia wanaweza kuwa na wafanyikazi au watu wa kujitolea wenye uwezo wa kufikia jamii za mitaani na ambao wana tajriba za kufanya kazi na jamii hizo. Pia wanaweza kutoa pendekezo lenye gharama za chini kuhusu jinsi ya kufika mashinani na kibinafsi kuwasilisha ujumbe unaotumwa kupitia kwa vyombo vya habari.
Maelezo:
[1] Larry Diamond, “Katika Hatua ya Kuunganisha Demokrasia”, Jarida la Demokrasia 3 (Julai 1994): 5