Ili shirika lifaulu katika kutekeleza wajibu wa elimu kwa Wapigakura na malengo ya Mpango wake, inafaa kuwashirikisha wale ambao wana manufaa ya kimsingi katika matokeo ya Mpango huo. Washika dau wanafaa kufahamishwa kuhusu Mpango, na kuombwa idhini na usaidizi wao. Inawezekana kuwa washiriki wote katika mchakato wa uchaguzi watahisi kuwa wana haki ya kutoa maoni, kushiriki katika, na kutathmini kufaa kwa Mpango. Wanaweza kuchagua kutotumia haki yao. Hata hivyo, baadhi ya watu wanaweza kuamua kukashifu au hata kuhujumu Mpango.
Wapigakura wenye maarifa watafanya lolote, kwa hivyo, kuelezea azimio lao namatarajio na vilevile kuelezea shabaha na mipaka ya Mpango pamoja na washika dau wote. Maingiliano haya yanaweza kupangwa, lakini pia kila mara yatahusisha shughuli zisizotarajiwa (tazama Taratibu za Ushirikiano). Katika nyakati zingine, hata inaweza kuibua mabishano ya umma. Hili linakubalika, bora tu haibadiliki na kuwa hasara au kufifisha uadilifu au hisi za kibinafsi za waelimishaji.
Makundi Matatu
Kila mara, huwa kuna makundi matatu ya washika dau wanaohusika katika uchaguzi:
Wasimamizi wa uchaguzi. Katika hali nyingi, sheria ya uchaguzi itaunda tume ya kitaifa ya uchaguzi au kitengo fulani maalum cha serikali kinachowajibikia usimamizi wa uchaguzi. Kwa kutegemea vitengo vya kimuundo vya baraza hili, kunaweza kuwa na idara maalum zinazowajibikia mambo kama vile elimu kwa Wapigakura, uhusiano wa umma, utoaji mafunzo, uundaji wa sheria, maandalizi ya uchaguzi, na kadhalika. Kunaweza kuwa na mabaraza ya kisheriavilevile, kama vile taasisi za kutunga sheria zenyewe, mashirika ya kutoa ulinzi; au serikali za mitaa, lakini zina wajibu fulani kusaidia katika maandalizi ya uchaguzi.
Wagombezi. Wagombezi wa kimsingi katika uchaguzi ni washindani ambao wanashindania kivyao au wanawasilishwa na vyama vya kisiasa vilivyosajiliwa, miungano ya umma au makundi ya Wapigakura. Ndani ya miungano yao ya kampeni na kila mara kwa usaidizi wa vitengo mbalimbali vya vyama vya kisiasa, wagombezi wanaweza kuwa na raslimali ambazo zimedhamiriwa shughuli kama vile habari kwa Wapigakura na shughuli za kuwahamasisha watu kujitokeza na kupiga kura.
Wapigakura. Kundi la tatu la washika dau linahusisha wale wote wanaopiga kura. Wapigakura wanaweza kutazamwa kwa ujumla; kugawanya katika makundi, kama vile wapigakura wanawake, vijana na wale wanaopiga kura kwa mara ya kwanza, au Wapigakura wa kijeshi; na katika misingi ya miungano na mashirika rasmi zaidi yanayoelezwa kwa ujumla kama mashirika ya kijamii. Mashirika haya ya kijamii, ambalo ni kundi moja kubwa linalohusisha makundi mengine, katika hali mbalimbali, na wakati mwingine kwa kukosea, yameelezwa kama huru, yasiyo ya kiserikali, au sekta ya kujitolea.
Mashirika ya kijamii hutekeleza wajibu muhimu katika elimu kwa Wapigakura kwa sababu ya uwezo wake wa kuhamasisha watu kuhusu shughuli za umma, uwezo wake kufikia watu wa aina mbalimbali, na raslimali zake zote.
Uchaguzi unahusu ushindani na vilevile ushirikiano. Waelimishaji wa Wapigakura hutegemea tabia ya ushirikiano ya washikadau wote kuhakikisha ukubalifu wao na uungwaji mkono wa Mipango yao.