Kabla ya kuendelea na uundaji na utekelezaji wa Mpango wa elimu kwa Wapigakura, wasimamizi wa uchaguzi wanaweza kugeukia kwanza sheria za uchaguzi, pale inapopatikana, kuamua ni nani anayefaa kushiriki katika shughuli kama hizo. Hata kama sheria ni wazi zaidi kuhusu ni makundi gani katika jamii yanafaa kuendesha elimu kwa Wapigakura au habari kwa umma, na sheria nyingi si wazi, bado inawezekana kufasiri sheria ili kuitekeleza.
Baada ya kutambuliwa ni makundi gani yaliyo na wajibu kisheria au haki kisheria kuhusika katika elimu kwa Wapigakura, mchakato wa kuunda shabaha, malengo, na vigezo vya Mpango fulani mahususi wa elimu kwa Wapigakura utatoa nafasi ya kuunda miungano, au kuunda ushirikiano mwafaka, katika shirika la kijamii na baina ya mashirika ya kijamii na mawakala husika wa serikali, kama vile wasimamizi wa kitaifa wa uchaguzi. Kwa kujenga miungano, wasimamizi wa uchaguzi na makundi ya mashirika ya kijamii yanaweza kupunguza gharama ya kijumla ya Mpango wa elimu kwa Wapigakura huku yakiendeleza uwezo wake wa kuwafikia watu wengi zaidi.
Makubaliano kuhusu shabaha, malengo, na vigezo vya Mpango fulani wa elimu kwa Wapigakura yanaweza kuafikiwa kupitia kwa njia mbili muhimu:
Kwa upande mmoja, wasimamizi wa uchaguzi wanaweza kuamua haya wao wenyewe na kisha kujaribu kuyauza kwa wale ambao wanatumai kushirikiana nao. Mwelekeo huu mara nyingi hufichua upungufu kwa kuzingatia muda unaohitajika kuuza Mpango na vilevile kutokuwa na hisia za umiliki miongoni mwa mashirika ya kijamii, na tatizo katika ukuzaji makubaliano na kisha kuyaendeleza katika kipindi chote cha Mpango. Upungufu huu unaweza hatimaye kusababisha aidha upinzani au chuki na mashirika ya kijamii, ambao baadaye utaathiri mtazamo wao kuhusu wasimamizi wa uchaguzi na kuhujumu jitihada za baadaye katika ushirikiano.
Kwa upande mwingine, wasimamizi wa uchaguzi wanaweza kutumia mbinu kadha kuhakikisha umiliki wa mapema na usaidizi unaoendelea wa Mipango ya elimu kwa Wapigakura. Haya yanaweza kuhusisha:
- mikutano ya waelimishaji
- mikutano ya mashauriano
- mahojiano na viongozi wa mashirika ya kijamii
- usambazaji mpana na wazi wa nakala chafu na nakala safi za sheria na kanuni za uchaguzi
- utoaji wa nyaraka zingine ambazo huenda zikawa muhimu kwa waelimisaji kama vile taafifa kwa vyombo vya habari, vifaa vya kutolea mafunzo kwa wafanyikazi wa uchaguzi, na vifaa vya utoaji habari kwa umma, kwa mfano, Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara, kwa wakati ufaao.
Wasimamizi wengi wa uchaguzi wanahofia kuwa shughuli hizi zinachelewesha mchakato au, katika hali ya kutolewa kwa nakala chafu, inaweza kusababisha mkanganyiko. Ingawa kunaweza kuwa na tofauti ya maoni, hata hivyo, au hata mabishano ya umma, hatua hizi mara myingi husababisha sheria bora na Mipango bora mwishoni na hifadhi katika muda unaohitajika kuwaleta watu katika shughuli, na kuwaeleza zaidi kuhusu mchakato wa uchaguzi, au kuwazoesha kwa viwango vilivyowekwa na Mpango. Wakati na juhudi ambazo ziliwekezwa awali katika mchakato huu mara nyingi hutuzwa kwa ufanisi hatimaye.
Kwa habari zaidi au mipangilio ya kuendesha Mipango ya elimu kwa Wapigakura, tafadhali rejelea sehemu ya Mpangilio Mahususi wa Uchaguzi.