Ni nani anayeishi wapi?
Swali hili linaweza kuwa la kwanza na la kimsingi zaidi ambalo waelimishaji wanafaa kuuliza wakati ambapo wanaandaa Mpango jumuishi, pale ambapo ni wa kitaifa, kieneo, au kimashinani katika upeo wake. Hakika, neno demografia (habari za takwimu kuhusu uzazi na watu kwa ujumla) linahusiana kwa karibu na demokrasia na pia linaweza kusemekana kuwa msingi wa majadiliano kuhusu uwakilishi na uongozi.
Habari kuhusu Sensa
Swali la ni nani anayeishi wapi huwa linajibiwa kupitia kwa sensa ya kitaifa. Pale ambapo sensa hii hufanyika mara kwa mara na mashirika yenye hadhi katika hali ambapo hakuna ushawishi kwa watu kuepuka au kukwepa kuhesabiwa na pale ambapo hakuna uwezekano wa kutokea kosa la kiusimamizi wakati wa kuhesabu au wakati wa mchakato wa kutayarisha matokeo, kutakuwa na deta ya kutegemewa na waelimishaji. Katika mazingira ya kimpito, hata hivyo, wakati ambapo mipaka imechorwa upya au pale ambapo kumekuwa na uhamaji kwa wingi au mabadiliko katika idadi ya watu, huenda kusiwe na deta ya sensa ya moja kwa moja. Hali hii huenda ikawa tokeo la ugumu wa mazingira ya kisiasa, au uhaba au kutokuwepo kwa raslimali za kifedha, au kutokuwepo kwa taasisi yenye tajriba na inayokubalika kwa umma ya kuendesha shughuli ya sensa.
Kwa kawaida, deta inayokusanywa kupitia kwa sensa inafaa kujumuisha habari kuhusu makundi ya kirika, kama vile ni watu wangapi waliopo wa makundi mbalimbali ya kirika, jinsia na deta kuhusu hali ya kijamii na kiuchumi, na habari kadha za kimsingi kuhusu familia. Haya yote yatakuwepo kulingana na eneo la kijiografia, na maeneo haya ya kijiografia yanaweza kuhusisha maeneo madogo sana yaliyotengewa ujumuishaji wa hesabu. Habari hizi zote muhimu zinaweza kuwepo katika programu inayohusu mifumo ya habari ya kijiografia (Mifumo ya Habari za Kijiografia) ambayo huwezesha uratibu kwa misingi ya kutumia ramani. Au inaweza kuwasilishwa katika chati au grafu, vijitabu, au majedwali. Katika baadhi ya mazingira ya kimpito, hata kama kuna nia na uwezo wa kukusanya deta kuhusu watu, huenda ikawa vigumu sana kupata habari kama hizo kutoka kwa ofisi ya kiserikali ambayo haifanyi kazi katika hali ya uwazi au haijichukulii kuwa inayopaswa kuajibika kwa umma.
Njia ambazo hesabu hizi zinaweza kufanyika hutofautiana kulingana na aina ya jamii na raslimali zilizopo. Kwa jumla, sensa ni hesabu kamilifu ya kila familia, na kwa sababu hii hufanyika mara kwa mara, kwa kawaida kila miaka mitano au kumi. Sensa inaweza kuwa ghali na inahitaji maandalizi mengi. Nchi zinaweza kujaribu kuhakikisha kuwa sensa na uchaguzi wa kitaifa hazisadifiani.
Pia zinasababisha ubishani. Matokeo ya sensa yanatumika kwa mipango ya kitaifa na kwa kuweka mipaka ya maeneo ya uchaguzi (tazama Deta ya Idadi ya Watu). Katika nchi nyingi idadi ya watu katika kila jimbo au eneo ina athari ya moja kwa moja kwa idadi ya watu ambao wanaweza kuchaguliwa kutoka katika jimbo au eneo hilo. Kwa sababu hii, matokeo ya sensa yanaweza kuchunguzwa kwa uangalifu zaidi. Maswali yanayoulizwa yanaamua aina ya habari zilizopo kwa waandaaji na wanasiasa, na zinaweza kuathiri mitazamo kuhusu eneo fulani hasa inapogunduliwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoongea lugha fulani mahususi au wanajieleza wenyewe katika hali fulani.
Kwa sababu ya ubishani huu, kuna uchunguzi fulani wa matokeo ya sensa. Njia mojawapo ambapo hili hufanyika ni kupitia kwa kuendesha uchunguzi kielelezo kupimia deta; njia nyingine ni kuangalia maelezo sambamba kama vile utafiti wa idadi ya watu wanaozaliwa na wanaofariki na uhamaji wa kijumla wa watu. Lakini, pia kwa sababu ya ubishani huu, kunaweza kuwa na deta ambayo inafaa kuchunguzwa dhidi ya habari nyinginezo. Katika nchi zenye mipaka wazi, pale ambapo kumekuwa na mizozo, pale ambapo taasisi inayokusanya deta ya idadi ya watu inashukiwa, au pale ambapo ukusanyaji wa deta mpya ya kifamilia unaweza kusababisha kupotea kwa manufaa yanayotolewa na serikali, watu wanaweza kuchagua kujitambulisha.
Huku sensa ikifanyika katika misingi inayotambulika kote ulimwenguni, nchi zenye makazi makubwa yasiyokuwa rasmi mijini zinaweza kuona vigumu kumudu hali hii. Katika baadhi ya hali, picha zinazopigiwa angani na deta kielelezo kuhusu idadi ya watu katika kila makazi inaweza kutumika kupata ukadiriaji bora zaidi.
Deta ya Sensa Kutumiwa kwa Tahadhari
Waelimishaji hutaka kuitumia deta ya sensa kwa tahadhari kidogo; na wanaweza kutaka kuitumia pamoja na deta iliyokusanywa wakati wa usajili wa wapigakura au na taarifa ya ziada iliyotolewa kwa wale wanaofanya kazi katika eneo husika. Licha ya hadhari hii, bila taarifa ya sensa halmashauri za kusimamia uchaguzi zitasumbuka kwa kiwango fulani. Katika kisa cha nchi mpya au mipaka mipya ya maeneo ya usimamizi kwa mfano, au pengine kwa sababu sensa haijafanywa kwa miaka mingi, mpango wa halmashauri za kusimamia uchaguzi unaweza kuwa hafifu au mkubwa zaidi. Huu wa mwisho japo ghali, unaweza kuwa bora.
Taarifa za Kimsingi Zinazohitajika
Waelimishaji watataka kuwa na uwezo wa kuigawa nchi katika maeneo ya upigaji kura na wana taarifa zifuatazo za kimsingi kwa kila eneo:
- jumla ya idadi ya watu
- idadi ya wanaume na wanawake
- idadi ya watu waliofikisha umri wa kupiga kura
- idadi ya watu walio kati ya miaka 18 na 25, 26 na 40, na zaidi ya miaka 65
- aina za makao wanamoishi watu hawa
- uwezo wa mapato
- lugha ya kimsingi inayotumika katika nyumba hiyo
Kwa kuwa na taarifa inayotambua, hata kama ni dhuluma, matabaka ya kiuchumi na kijamii ya watu, ama kwa kuzingatia aina ya makazi yao au mapato ya nyumba hiyo hutoa ishara ya mitindo ya kimaisha ya watu. Kwa kujua watu ambao ni vijana, na pengine wanaopiga kura kwa mara ya kwanza; na gani ambao ni wazee hivyo basi huduma maalumu pia itakuwa muhimu. Katika visa hivi vyote, waelimishaji watataka kutumia taarifa nyingine waliyonayo katika kufasiri deta ya kidemografia.
Kufasiri Deta
Kufasiri maelezo kuwahusu watu kuanzia kwa umri au mapato huhitaji uelewa wa utamaduni wa nchi hiyo. Je, watu huenda kazini wakiwa katika umri wa chini? Miaka ya juu kabisa amabyo wengi wao hufikisha? Afya ya watu hao ni aina gani? Watu hao hupata watoto wakiwa katika umri gani? Ni viwango vipi vya mapato vinavyochukuliwa kuwa umaskini au utajiri, na hilo hudhihirikaje katika maisha ya watu au hatua wanazochukua?
Vitoa Taarifa
Waelimishaji wanaweza kujaribu kupata taarifa ya kidemografia kwa kuanza na mashirika yanayoshughulika na sensa ya kitaifa au idara husika za serikali, na kisha kutafuta taarifa inayofanana na hiyo iliyotayarishwa na Benki ya Dunia, Shirika la Afya Ulimwenguni, au Umoja wa Mataifa na mashirika yanayohusiana nao. Wakibahatika, taarifa hii itakuwepo kwenye tarakilishi na wakiwa na bahati kabisa watakuwa na uwezo wa kufikia deta ya kisasa ya GIS. Taarifa yoyote ile iwayo, bado itafungiwa na mipaka ya wakati na italazimika kusahihishwa kulingana na makadirio bora yanayoweza kupatikana.
Wajibu wa Halmashauri za Kusimamia Uchaguzi
Kwa kuwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi ina haja ya dharura ya kuwa na taarifa nzuri ya kidemografia, itataka kujadiliana na mashirika na ofisi za serikali njia zinazoweza kutumiwa kuboresha taarifa iliyopo. Hili ni jukumu la kijumla badala ya kuegemea uchaguzi pekee. Hata hivyo, kupata taarifa ya kiwakati na linganifu kuwahusu watu kutasaidia kwenye mipangilio ya uchaguzi kuanzia kwa uratibu wa shughuli ya elimu kwa wapigakura hadi kwa kutambua idadi ya Wapigakura waliohitimu. Hawa wa mwisho wataathiri idadi ya vituo vya kupigia kura,idadi ya kura zitakazochapishwa, idadi ya vifaa vya uchaguzi vitakavyohitajika, na idadi ya wafanyakazi kwenye upigaji kura watakaoteuliwa na kadhalika. Kwa hivyo, waelimishaji watataka kuwa na uwezo wa kufikia deta kuhusu idadi ya watu na kupendekeza taarifa nyingine za ziada kuhusu hali ya kiuchumi na kijamii na hisia inayoweza kukusanywa.