Wakati ambapo halmashauri ya kusimamia uchaguzi na mashirika ya kijamii yanavyoendelea na uundaji wa Mipango ya elimu kwa Wapigakura, itakuwa muhimu kwao kuelewa muktadha ambamo mipango kama hiyo itaendeshwa. Tathmini hii inafaa kuhusisha uelewaji wa mfumo wa kisheria wa uchaguzi, hali mbalimbali za kisiasa, Wapigakura, kwa ujumla na pia kuhusiana na makundi maalum na rasilmali zilizopo kuendesha mpango.
Ukadiriaji wa muktadha pia utakuwa muhimu zaidi katika mazingira ya kimpito ambapo panawezekana kuwa na mabadiliko muhimu katika mazingira ya kisiasa. Haya yanaweza kujumuisha katiba mpya, sheria za uchaguzi zilizotungwa au kufanyiwa marekebisho hivi maajuzi, mabadiliko katika utaratibu wa uchaguzi, kuanzishwa kwa mifumo mipya ya uwakilishaji au teknolojia za uchaguzi, uanzishaji wa halmashauri ya kudumu ya uchaguzi au mashirika wakilishi katika maeneo ya mashinani, ukuaji wa vyama vya kisiasa na makundi ya kijamii, kuruhusu sehemu fulani za jamii kupiga kura, uhamaji wa wananchi wengi (pamoja na watu waliopoteza makao yao kutokana na vita), mabadiliko katika au labba kuharibika kwa miundomsingi ya nchi, uongezekaji kwa haraka wa vyombo vya habari, na kadhalika.
Uelewaji wa muktadha huchangia katika kuhakikisha kuwa Mipango ni faafu, ni yenye manufaa, nani muhimu. Pia ni muhimu katika kuhakikisha kwamba mipango si ya gharama nafuu tu bali inaweza kutathminiwa kwa urahisi wakati inapokamilika.
Kuhusu Wapigakura, waelimishaji watataka kujua habari muhimu za kimsingi na kisha, wakitumia mbinu mwafaka zaidi zilizopo, watatambulisha mahitaji ya kielimu ya Wapigakura kwa ujumla na vilevile kama Wapigakura lengwa.