Elimu kwa raia na wapigakura vinapaswa kuzingatia utamaduni. Jinsi mpango wa elimu utakavyotekelezwa kwa watu, lugha itakayotumika au zitakazotumika, mbinu za utekelezaji zitakazotumiwa, mbinu za mawasiliano zitakazotumika, na mitindo ya waelimishaji vyote vinapaswa kuzingatia utamaduni na mapendeleo ya kidini ya eneobunge husika.
Mapendeleo haya yanaweza kuwa vizuizi, mtego au mwanya. Vyovyote vitakavyokuwa, waelimishaji watakuwa na uhusiano wa kipembuzi navyo. Elimu ni, katika uasilia wake, kichocheo cha hali kubaki vile iliyokuwa. Hutoa mwangaza wa kindani katika taswira mpya, na hili linaweza kuchochea watu au makundi yao kuangazia kihakiki kaida ambazo wao huzipuuza. Kwa kuwa shughuli za elimu kwa wapigakura haziongozwi tu na haja hizi wapigakura bali pia na amri ya serikali, waelimishaji watataka kutahadharia jinsi wanavyoingiliana na tamaduni na dini za watu.
Hakuna haja ya kurejelea kaida hizi kama zinakinzana na ujumbe wa uchaguzi. Ilhali, elimu kwa raia na wapigakura itatokeza wazi tabia ambazo haziafikiani na kaida kubalifu zinazoendelea kuongezeka. Huu mtanziko ambao waelimishaji watalazimika kukabiliana nao. Ncha za mtanziko huu hujikita sana katika nchi zisizo na serikali yenye mfumo wa kidemokrasia. Hata katika nchi zenye demokrasia hata hivyo, unaweza kuchipuka katika makundi tengwa.
Kizuizi
Utamaduni na dini vinaweza kuwakilisha kizuizi kwa waelimishaji kwa sababsu hujenga jamii zilizo na ishara na lugha za kibinafsi. Jamii hizi mara nyingi hazifungiwi lakini zikiwatambua kutoka nje ya mazingira yao zinaweza kuwashuku.
Huenda wakawa wamejenga maoni na kaida kuhusu wajibu na uwezo wa kufikia elimu, na kuhusu maana ya demokrasia na kama inakubalika. Badala yake, tamaduni mbalimbali zinaweza kuwa na misimamo thabiti kuhusu anayefaa au asiyefaa kuwaelimisha wanaume, wanawake, au hata watoto. Wanaweza kuwa na mifumo ya uongozi na mamlaka ambazo haziafiki pendekezo la kijumla la usawa ambalo ndilo msingi wa demokrasia wakilishi.
Mwisho kabisa, kunaweza kuwa na manung’uniko kuhusu mbinu ya kuelimisha. Mitindo ya kufundisha na kusoma inaweza kuwa ilitungwa na desturi zao za kitamaduni na kidini, hivi kwamba maarifa kama vile kazi za makundi, mtindo wa maingiliano katika kufundisha, mazoezi ya kufikirisha kihakiki, matumizi ya hojaji za kupima viwango, na matumizi ya mitambo ya kutoa sauti na picha vinaweza kuishia katika watu kukwepa, au kuhudhuria lakini wakijikokota katika kusoma.
Mtego
Bila shaka, vizuizi vinaweza kuishia kuwa mitego itakayowatatiza waelimishaji. Utamaduni na dini vinaweza kutumiwa kuhakikisha kwamba watu wa kawaida ambao huenda wakataka elimu nzuri kuhusu uchaguzi na haki zao kama raia, wananyimwa nafasi ya kupata elimu hii. Katika hali hizi, kukosekana kivyovyote kwa hisia za utamaduni na dini hakuwezi kutazamwa kwa wepesi tu bali utatumiwa kama kijisababu cha kuhujumu mpango huo wa elimu. Kwa sababu hii, waelimishaji watataka kupima hisia hizi kwa makini ili zisije kuwa vizingiti.
Nafasi
Heri nyingi bila shaka, huwa pale ambapo waelimishaji wanaelewa mazingira watakamofanyia kazi, au kuwa kwamba wamepanga ratiba yao hivi kwamba wamejenga timu inayoelewa mazingira haya. Kisha, wao hupewa pahali pa kupata nahau nyingi, analojia, kaida na hadithi fupi zinazoweza kuwasaidia wanafunzi kujua njia mpya za kutumia katika kuelewa ukweli kuwahusu wao wenyewe na mafunzo yanayopatolewa kuhusu uchaguzi na raia.
Kwa kutoa mfano mmoja tu, inaweza kuwa muhimu kuzingatia waelimishaji kutoka Afrika Kusini waliolazimika kutafuta njia ya kuwasaidia watu kuelewa siri ya uhalisia wa kupiga kura. Katika majidiliano na wanawake kutoka kwa jamii za kiasili, waligundua kwamba ujauzito hutoa nafasi ya taswira ya kistiari. Yaani, jinsia ya mtoto huwa haijulikani kabla kuzaa. Hata hivyo, waligundua pia kuwa istiara hii haingeweza kutumika vilivyo katika mpango wa elimu kwa sababu ya mwiko wa kuzungumza waziwazi mbele ya watu kuuhusu ujauzito. Kwa sababu hiyo, umbo jingine liliteuliwa ili kujadiliwa – lile la mbegu iliyopandwa na mkulima. Hakuna anayejua jinsia ya mbegu hiyo hadi inapochipuka na kukua. Michoro iliyotumiwa kusaidia majadiliano yaliyofanywa ana kwa ana hata hivyo inaangazia mwanamke mjamzito. Anapiga kura lakini hali yake haingaziwi. Inatambuliwa hata hivyo na wanawake hasa, na dhana ya kupiga kura kisiri inawasilishwa – kisiri.