Mipango ya elimu inapaswa kutumiwa katika mipaka ya raslimali zilizopo. Hili halipaswi kuchukuliwa kama kizuizi ikiwa waelimishaji wanazingatia suala la raslimali kabla ya ya kupanga maazmio na kuweka mkakati na mipango ya kielimu.
Pamoja na raslimali za kawaida za watu na pesa, waelimishaji watahitajika kuzingatia chochote kingine ambacho nchi inaweza kutoa katika vitu kama vile miundomsingi na mtaji wa kijamii.
Katika jamii nyingi zinazobadilika, hasa baada ya vita, mizozo ya kikabila au hali ngumu ya kiuchumi, ubora wa muundomsingi unaweza kuwa moja katika changamoto kubwa dhidi ya kutekeleza mpango wa elimu kwa wapigakura, hasa kwa upande wa usambazaji.
Kunaweza kuwa pia na mtafaruku kuhusu anayepaswa kushughulikia gharama ya baadhi ya shughuli na vitu mbalimbali. Katika visa vingine, kwa mfano, sheria ya uchaguzi inaweza kuhitaji vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali kupeperusha jumbe rasmi kuhusu elimu kwa Wapigakura. Muda wa maongezi wa bila malipo usipotolewa kwa njia ya wazi na bila utata, fasiri tofauti tofauti zinaweza kuzuka kati ya chombo hicho na halmashauri ya kusimamia uchaguzi kuhusu anayepaswa kushughulikia gharama ya utangazaji.
Tathmini ikishafanywa kuhusu raslimali zilizopo, inaweza kupatikana kwamba zinaafiki kutekeleza mipango hiyo muhimu.
Hata hivyo, changamoto nyingine nzito zinaweza kuibuka. Katika hali hii, halmashauri ya kusimamia uchaguizi inaweza kuwa kama kichocheo cha kupata raslimali. Haipaswi kubaki tegemezi katika hali ya kukosekana aui uchache wa raslimali hizo hata japo inaweza kuhitajika kujenga mikakati, hasa ya kielimu ambayo itaeleza sababu za uchache huo raslimali zilizopo. Kunaweza pia kuwa na uwezekano wa kupata raslimali kutoka kwa sekta ya kibinafsi (angalia Sekta ya Kibinafsi) vilevile Usaidizi wa Kimataifa) au wa kushawishi kupatikana kwa raslimali kwa kubuni ushirikiano wa kimpango mashirika ya kushughulikia raia (tazama Mikakati ya Ushirikiano katika Elimu kwa Wapigakura) na sehemu inayohusu Mashirika Yaliyopo ya Kijamii). Hatimaye, vigezo vya mpango wa elimu kwa wapigakura vinapaswa kudhihirisha uamifu katika kupiga hesabu za raslimali. Bajeti ya elimu kwa wapigakura haiwezi kutatiza matayarisho mengine kwa shughuli ya uchaguzi, ilhali usimamizi wa uchaguzi hauwezi kupitisha raslimali za kitaifa zinazohitajika kwa shughuli nyingine.