Waelimishaji sharti wakisie na kuelewa mahitaji ya wale wanaowandalia mipango ya elimu. Kuna njia kadha za kutathmini mahitaji na wanaofanya mipango ya elimu watazingatia yafuatayo.
- Muda uliopo
- Uchangamano wa mipango na uenezi wa kijiografia
- Kama mipango inatekelezwa kwa mara ya kwanza au kama kuna habari za kiasasi ya kuweza kuafikia maeneo lengwa.
- Kuwepo kwa fedha.
Waelimishaji watahakikisha usaidizi wa kitaalamu. Sehemu hii inatoa mwongozo wa kuzingatia usaidizi ufaao wa kitaalamu na jinsi ya kusimamia usaidizi huo. Sehemu ya “Ukaguzi” inafafanua taratibu changamano ambayo watoa elimu wataanzisha, lakini kuna uwezekano wa kutumia “data iliyopo” na kutumia timu ya waelimishaji kupata habari kupitia “washiriki na waamuzi”.