Wasomi wanaojaribu kudhibitisha matakwa ya kielimu na kupata miundomsingi ya uwakilishi bunge na taifa lengwa wanaweza kuchukulia kuwa lazima waanze upya. Wanaweza kutumia muda mchache kuchunguza vyanzo vya data vilivyopo ili kupata manufaa kama:
- Wakati mchache unaohitajika kufanya uchunguzi
- Gharama yote inayohitajika kuwa chini
- Mapengo yaliyotambulika yanayotoa utafiti zaidi
- Mapengo ya data ya kawaida yaliyotambuliwa ili kupata haja za maendeleo ya kawaida
Ni maeneo machache tu ambayo hayajatafitiwa. Na pia maeneo machache ambayo chanzo cha habari kuyahusu hayajajulikana. Tatizo ni kupata habari iliyopo kutoka kwa jamii funge au zinazodhibitiwa na imani fulani. Mashirika ya kimataifa hupendelea kushirikisha wenyeji katika data iliyopo. Mara nyingi huwa hawaelewi chimbuko la habari lililopo hasa iwapo habari yenyewe ni simulizi na ya kitamaduni na hivyo basi huwa wa kwanza kuchukulia kuwa kitu fulani kigeni kinachopendeza kinastahii kufanywa. Lakini wale wanaoshughulikia mipango ya uchaguzi wanastahili kuelewa kazi yao kuhusiana na mipaka pana ya kidemokrasia. Habari kamili inahitajika kwa wanaotawala na shirika la jamii. Na uchaguzi unastahili kurahisisha kukusanya na kuwepo kwa habari.
Karatasi, Watu au Mego
Habari iliyopo kwenye data ya tarakilishi hupata umaarufu wa kuimarishwa na kudumishwa na hata kusambazwa kutoka eneo moja hadi lingine. Kama imekusanywa vizuri na ambapo upangaji wa zana tepetevu na zana ngumu za tarakilishi umefanywa, uhifadhi wa data wa tarakilishi unaweza kuwa bora. Huenda pia likawa jambo la kuvunja moyo hasa katika mataifa yanayoendelea. Habari inaweza kuhifadhiwa katika maumbo yasiyooana, au huenda ikawa imepitwa na wakati ama haijakamilika na hivyo kukataliwa. Tarakilishi huenda zikawa laana au ushindi wa demokrasia wazi. Habari zipatikanazo kwenye maandishi huwa hazipati matatizo ya kutopatana. Hapa shida huwa ya uhifadhi, iwapo nyaraka na machapisho yapo, na gharama za kufanya marudio.
Watu Huona tu Umbali wa Upeo Wao
Wale wanaotafuta data hutaka tu kuchunguza maswali yanayotegemewa, yanayopatikana, na gharama. Kwa mfano, katika maeneo mengine ambapo pamekuwepo na mfumo wa kimabavu, huenda pasiwe na utamaduni rasmi wa “uhuru wa kupata habari”. Urasimu wa serikali huenda usijali kutafuta habari. Huenda ikaichukulia kuwa heshima au hata siri ya taifa. Vilevile, kuna hatari kuwa data inayopatikana na serikali ikabadilishwa kwa sababu za kisiasa. Ndipo hata ikiwekwa wazi kwa umma haitakuwa na manufaa yoyote kwa wasomi.
Hata hivyo, hata data isiyo na hitilafu huwapa wasomi masuala ya utumizi wake kwa sababu, kuna habari kubwa ya ukweli inayohitaji uteuzi wa kimakini. Wasomi hutaka kubainisha habari wanayohitaji na jinsi watakavyoitumia hata kabla ya kuanza utafiti. Patakuwepo na urudiaji wa utumizi wa maswali haya, kwa sababu wakati habari fuani imetoewa kwa umma huzua maswali zaidi. Hata hivyo umakini ni jambo la maana.
Kuangalia Katika Maeneo ya Kawaida
Orodha ya majina ya wapiga kura na data inayohusiana nayo hutoa mahali pa kuanzia ikiwa orodha hizi zimekusanywa kwa taifa nzima au kwa sehumu. Itatoa habari muhimu kuhusu idadi ya wapiga kura na maeneo yao. Katika mataifa yanayoendelea na jamii za mpito hata hivyo, orodha ya upigaji kura huenda isiwe nzuri. Wasomi katika hali hii watahitajika kuchunguza ukweli wa orodha ya wapiga kura ya wakati huo ili kuelewa utumizi wake.
Ili kubainisha orodha, habari kuhusu maafisa wa usajili pia inastahili kuwepo, mahali waliposajilia watu, na hata mahali palipotathminiwa lakini hapakutumika. Kati ya maeneo haya patakuwepo na mahali pengi pa umma kama vile maktaba, shule, ukumbi wa jamii, zahanati na afisi za serikali pamoja na majengo yasiyodumu yaliyo kama mahali pa mikutano ya wanajamii kama vile uwanja wa michezo, soko na kadhalika.
Habari nyingine muhimu inaweza kupatikana kwa miundo inayotofautiana na habari asilia ipatikanavyo kwenye tarakilishi. Miongozo ya simu inaweza kuwa ya maana kama vile miongozo ya kiserikali, barua za ulipaji kodi na orodha za anwani(ambapo hizi ni nyaraka za umma), orodha za leseni za radio na runinga na utafiti wa kuuzwa.
Kando na hizi habari muhimu za kimaeneo na anwani, patakuwepo na ripoti na vitabu vya mwaka vya serikali kuhusiana na habari mbalimbali. Katika mataifa yaliyo na umasikini mwingi, ripoti hizi lazima zingefanywa na maejenti wa kimataifa au mashirika ya kimataifa yaliyo na hamu ya kuleta mipango ya maendeleo na nafasi za maendeleo.
Kwa kuongezea kwa ripoti yenye lengo la kimaendeleo, mataifa mengi yana ofisi za kitalii na machapisho ya kitalii, ambayo hutoa habari muhimu kuhusu taifa na usafiri. Jedwali kuhusu usafiri wa magari moshi na mabasi, orodha ya majina ya mahoteli, anwani za maofisi ya habari za kienyeji, haya yote huongezea habari kuhusu miundomsingi na utawala msingi.
Kutokana na kuchipuka kwa mitandao ya intaneti, imekuwa rahisi kutafuta na kupata habari kuhusu mataifa. Hata ingawa sio habari yote inayoweza kupatikana ndani ya taifa, itashangaza kiasi cha habari inayoweza kupatikana katika taasisi za kiakademia. Kwa sasa, kupata habari katika taasisi kama hizi katika Amerika Kaskasini na Kusini pamoja na Kaskasini mwa ekweta ni nyingi kwenye mtandao. Lakini taasisi hizi, huwakaribisha wahudumu wa habari ambao huunganisha mashirika na mitandao kule Kusini mwa ekweta.
Kando na vifaa hivi muhimu vya habari, huenda pakawa na maktaba, idara za serikali, vitengo vya utafiti vinavyoshikana na taifa, eneo, na serikali za mitaa, na taasisi za utafiti za kisheria za taifa au eneo. Hizi zote hukusanya habari, baadhi yazo zitatoa habari pindi zinapohitajika na pengine kwa malipo. Mashirika ya kijamii ya kimataifa au kitaifa yana tajiriba pana ya kibinafsi. Yamekusanya habari kuhusu mataifa na kila mara hutaka kutoa habari hizi bila malipo kuliko idara za serikali.
Pengine, habari zile za umuhimu kuliko zote, lakini hazipatikani kwa urahisi, ni data iliyokusanywa kutokana na upigaji kura wa kisiasa. Sababu kuu kwa kuzuia habari hii ni kuwa ina umuhimu katika mielekeo ya mtu na maoni ya vikundi na undani wa mambo yanayohusiana na uchaguzi. Kama ingewezekana pawepo na uhusiano mwema na wanaokusanya habari hizi za utafiti, ingewezekana kuwaomba wachanganue tena data iliyopo ili kujibu maswali fulani ambayo wanaofunza kuhusu upigaji kura wanaweza kuwa nayo.
Vyanzo vyote na mashirika yaliyoorodheshwa pale juu yamekuwa yakikusanya habari si kwa manufaa ya uchaguzi lakini kwa sababu zingine, kwa hivyo, habari huwa na undani na kina ambacho maafisa wanaoandaa kwa kipindi cha uchaguzi fulani hawangependa kutoa nakala.
Kwa wakati uo huo hupata pigo kutokana na kupangwa tena kwa mifumo ambayo ni muhimu kwa wanaofunza elimu ya upigaji kura. Kazi hii huenda ikawa ngumu huhitaji muda mwingi na huwa ghali. Kutofanana kwa data, habari iliyokusanywa kwa vipindi tofauti na iliyo na vipengele vinavyotofautiana vya utegemezi, habari fupifupi zenye upendeleo kwa miji na watu, mbinu za kupata hela, na mijadala ya zamani ya kisiasa vyote hushirikiana dhidi ya mkusanyaji/mtafiti.
Huenda pakawa na nyakati ambapo kazi ya kukusanya habari hizi ni nyingi, huhitaji muda mwingi, huwa ghali hata kuliko kutafuta habari nyingine mpya nyanjani. Lakini hili halitawezekana mahali ambapo wanaofunza elimu ya kupiga kura wanafanya kazi yao. Tukilenga maendeleo na uelewaji wa jumuiya ya kupiga kura, muundomsingi wa taifa uliopo wa kusaidia vipindi vya kielimu, na kushikilia haja za kielimu zinazopata makundi mbalimbali na wasikilizaji itasaidia kuhakikisha kuwa data iliyopo inaweza kutegemewa.