Elimu kwa wapigakura huwa tegemezi, kama njia nyingine za elimu kwa fikira za kiitikadi. Waelimishaji watahitaji kutawala tofauti baina ya washikadau na matokeo ya itikadi tawala, katika programu ambazo zimekua.
Kupambana na tofauti mbalimbali
Itakuwa afadhali iwapo fikira hizi za kiitikadi zitaeleweka na kufanywa wazi na waelimishaji. Hata hivyo kuna changamoto. Na mara nyingi huwa kunatokea mapatano ya kisiri kati ya washikadau tofautitofauti ambao wanataka programu ya kielimu lakini wana haja tofauti katika wanachopaswa kufanya. Mtazamo huu huwa si mbaya. Eti kwa sababu kuna waelimishaji wanaotumia fursa hii kuyachacharisha mashirika kuwa ya kidemokrasia huku wengine wakitaka upigaji kura uende vizuri siku ya uchaguzi na wengine wakitafuta kupata uaminifu wa wapiga kura ili katika maisha yao ya usoni waweze kutumia uaminifu huu kuendesha programu za kielimu au za kuendelea, jambo hili halifai kumaanisha kuwa hawawezi kushirikiana. Wala haimaanishi kuwa wapiga kura hawatapata ujumbe.
Hata hivyo kuna kiwango katika uenezi ambao huenda ukawa kati ya waelimishaji. Ikiwa uenezi huu ni mkubwa mno, huenda ukaleta mashindano na wakati mwingine ugomvi. Uamuzi utapaswa kufanywa kuhusu kile kinachowezekana na kisichowezekana pale ambapo kuna tofauti za kiitikadi kati ya waelimishaji na kati yao na wagombeaji na tume ya uchaguzi.
Tofauti za itikadi huchorwa kati ya elimu inayoleta kujuana na elimu inayoleta nguvu. Katika uwanja wa elimu ya upigaji kura, tofauti hii huweza kuleta mtazamo kwa malengo ya elimu ya upigaji kura na ugomvi unaoweza kutokea.
Uwezeshwaji na Mahusiano
Elimu ya upigaji kura inaweza kuleta kukubali kwa mfumo fulani wa uchaguzi, kuwapa watu motisha ya kujiandikisha na kupiga kura, kuwapa ujuzi wa kupiga kura na kukubali matokeo ya uchaguzi.
Kwa wakati uo huo, huenda ukaweza kujenga hali kama ilivyo kwa kuhimiza ukubali wa mfumo wa serikali. Elimu ya kisheria inaweza kuwa njia ya kimsingi ya kukubali siasa zilizodumu na utamaduni wa kiuchumi. Utamaduni huu unaweza kuwa wa kidemokrasia lakini maana ya elimu ya kisheria inaweza kufanywa kuwa inazuia uchunguzi katika mawazo ya utamaduni huu.
Kwa upande mwingine, elimu inaweza kuchochea maswali ya kufikirisha kuhusu mfumo wa kisiasa na uchumi. Elimu kwa wapigakura inaweza kulenga kuwapa washiriki mdokezo katika mbinu ambamo matokeo ya uchaguzi yatatoa idhini kwa kundi fulani la wagombea na athari ya idhini hiyo kuhusu jinsi zitakavyosimamiwa. Maswali yanaweaza kuulizwa kuhusu hali ya uchaguzi, na maana ya maneno “uhusu na haki”, kuhusiana na hali fulani. Wapigakura wanaweza kupewa ujuzi unaohitajika kuteua miongoni mwa wagombea hao.
Ndani ya maswali haya ya kujuana na kuwezesha, waelimishaji wanaweza kuchagua programu zitakazofanya wananchi kuhitaji kuwepo kwa muelimishaji au huenda wakachagua programu zitakazowawezesha watu kujisomea wenyewe na kutotegemea muelimishaji.
Waelimishaji huwa watataka kutathmini malengo yao wenyewe na yale ya programu ambazo wanatayarisha. Huenda watataka kudhukuru programu halisi pamoja na namna zinazonuiwa kuutmiwa ili kuhakikisha kuwa ni sawa.