Waelimishaji wanalazimika kujenga mikakati ya kukabiliana na shaka ambayo wanafunzi wao wanaweza kuwa nao kuhusu shughuli ya upigaji kura na kuhusu watu wanaoitekeleza shughuli hiyo.
Shaka inastahili
Waelimishaji katika hali zinazokumbwa na migogoro, mabadiliko, na kukosa utulivu kisiasa wataulizwa kujitambulisha kuwa wao ni nani, wanakotoka, na ujumbe wao unavyoweza kuaminika. Katika hali ambapo uhusiano mwema ni kaida muhimu, maswali haya yanaweza kunyamaziwa, japo yataulizwa. Na ikiwa hilo haiwezekani kupata jibu la kuridhisha, iwe shughuli hiyo ya kuelimisha inapokelewa vizuri au la, itakuwa na athari ndogo sana. Katika visa vingine, inaweza kusababisha kutoelewana ambako hutatiza shughuli nzima na kuzuia uendeshwaji wake kabisa.
Maswali haya ni halali kabisa. Watu wazima hutarajia kwamba mafunzo ni kitu ambacho mtu anapaswa kukiingia kwa hiari na hivyo hutaka wajichagulie wenyewe. Pale ambapo uhusiano unajengeka moja kwa moja kati ya mwelimishaji na kundi la wanaosoma, inawezekana kuwa rahisi kukabili shaka yoyote ambayo huenda ikajitokeza. Mara nyingi hata hivyo, shughuli za elimu kwa wapigakura huwa ama hatua za watu kujiteulia kwa hiari katika jamii au huenda zisiwakilishe mawazo ya kundi linafundishwa au hadhira hiyo. Hili linaonekana wazi katika hatua za kielimu zilizoanzishwa na waajiri kwa wafanyakazi wao – hasa wale wasio katika miungano ya wafanyakazi – umbo jingine la shaka linaweza kujitokeza katika mazingira mengine pia.
Kujenga Kuaminiana
Imani inaweza kujengwa katika mazingira ya karibu kwa kuhakikisha kwamba matukio yote ya kielimu yanajumuisha utangulizi mwafaka wa waelimishaji na mashirika wanamotoka. Katika visa vingine hili hufanywa vizuri na mdhamini wa tukio hilo mwenyewe. Waelimishaji watataka kuwapa washiriki nafasi ya kuuliza maswali kuhusu shughuli hiyo, na kutalii matarajio yao na kiwango ambapo wataweza kuafiki haya. Baada ya kukamilisha shughuli, watawaomba washiriki kutathmini kufaulu kwake na kutoa mapendekezo kuhusu jinsi ya kuuimarisha. Pale ambapo shughuli za elimu hazina uhusiano wa moja kwa moja na wanaofundishwa, waelimishaji watalazimika kuanzisha mikakati mingine, na hii mikakati hii ya jumla itaimarisha mawasiliano ya moja kwa moja.
Kutopendelea Upande wowote
Wale wanaogombea nyadhifa za kisiasa wana kila haki ya kujenga mipangilio ya kuchochea na kuwaelimisha wapigakura. Idadi inayoendelea kuongezeka ya shughuli za elimu kwa wapigakura Marekani kwa mfano, inaonekana kimsingi kama suala lilioanzishwa na lililoratibiwa kuwachochea wapigakura (kama hadhira lengwa) badala ya kutoa elimu iliyojikita katika kusaidia uchaguzi au michakato ya kidemokrasia. Hata hivyo wale wanaonuia kutoa elimu isiyoegemea upande wowote na kuruhusu watu kufanya uamuzi wao wa kibinafsi kuhusu wagombea wa mamlaka na mbinu wanazoazimia kutumia kukabiliana na masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, watalazimika kutafuta mbinu za kujitofautisha na wale walio na miegemeo katika shughuli hiyo. Ili kufanya hivi wanaweza kuamua kushughulikia malengo yasiyoegemea upande wowote ambayo ni wazi kwa umma na maadili ya kikazi. Wanaweza pia kutaka wafanyakazi wanaofikisha viwango fulani watakavyoweka na kutangaza hilo wazi.
Wakati mwingine mwelimishaji anaweza kuwa analipwa kutekeleza shughuli hii, si na wapokezi wa shughuli hiyo bali na mtu mwingine, kama mwajiri au idara ya serikali. Udhamini wa shughuli yoyote ya elimu kwa wapigakura au kipande cha habari fulani maalumu au shughuli ya kielimu vinapaswa kuwepo. Katika visa vingine, hili linaweza kuhitajika na sheria.
Ili kukuza umuhimu huo, watatumia nyenzo na mbinu za kidemokrasia na ambazo zinaunga mkono kaida zinazokuzwa kama sehemu ya yaliyomo katika shughuli hiyo ya kielimu. Miongoni mwa haya kutakuwa na kujumuishwa kwa sauti mbalimbali, mijadala ya kuhimiza, na usawazisho wa mamlaka kati ya wanafunzi na waelimishaji.
Kuaminika kwa Shirika
Waelimishaji wanaowakilisha mashirika, au yanayochukuliwa kuwakilisha shirika jingine, yatataka kuhakikisha kwamba kuaminika kwa shirika lao ni kwa hali ya juu. Hili linahitaji kuzingatia viwango vya utaalamu katika kukabiliana na umma, katika kumudu fedha, na katika kushughulikia wafanyakazi wake. Itahitaji kuwa shirika hili linaendelea kuhakikisha kwamba linatekeleza yaliyokuwa katika mamlaka yake na malengo ya mpango wa elimu kwa wapigakura. Isitoshe, waelimishaji watatilia maanani mbinu wanayotumia kumudu mahusiano yao na mashirika, wauzaji, na wateja. Mashirika yatazingatia malalamishi yao na hasa kwa yanayosemwa kuhusu mpango huo wa elimu. Mwisho, kutokana na umuhimu wa machapisho yaliyopo ya kubadilisha mitazamo, waelimishaji watataka kuhakikisha kwamba hizi ni linganifu, za haki na zilizotokezwa vilivyo.
Uhalali
Chaguzi huzipa serikali uhalali. Mipango ya kielimu inapaswa kuhakikisha kwamba imepata uhalali huu kwa miafaka unganishi kuhusu kuanzishwa kwa mpango huo na uendesshaji unaoendelea kwa mujibu wa utekelezaji wa mpango huo na washiriki.
Kuhakikisha kwamba mamlaka yao yamethibitishwa na kwamba mikataba yoyote imezingatiwa kwa makini ndiko huanzisha mchakato huu (tazama Jukumu la Kielimu), lakini hata hivyo kuna uwezekano wa kuwa na migogoro kuhusu iwapo mpango wa elimu unapaswa kufanywa na shirika fulani maalumu au mashirika kadhaa. Hii inaweza kuhusisha hata halmashauri ya kusimamia uchaguzi.