Ikiwa kushindwa katika uchaguzi hakutaishia katika kubadilishana mamlaka kwa amani na, badala yake kusababishe vurugu, mapigano, au kukataa kwa mwanasiasa aliye mamlakani kuachilia uongozi, na pale ambapo chama cha kisiasa kinatumia njia chafu, vitisho vya watu, au mbinu nyingine chafu kama mbinu zake za kushinda uchaguzi, suala halitakuwa ikiwa raia wenyeawe wataelewa demokrasia bali litakuwa ikiwa viongozi wao wanaelewa demokrasia. Elimu kwa wapigakura, na vilevile elimu ya raia, hueleka kulenga watu wa kawaida. Nia huwa kwamba wanapaswa kujifunza kuzingatia demokrasia, kupiga kura, kuchagua viongozi, kuelewa jinsi michakato ya kisiasa inavyofanya kazi, kuhusu majukumu yao kama raia na kuhusu uongozi wa serikali.
Machache husemwa kuhusu ikiwa wale walio mamlakani wanaelewa kanuni za demokrasia na wamejitolea kuzizingatia. Ni machache sana yanayosemwa kuhusu kile ambacho huenda viongozi hawa wakahitaji kusoma punde wakishachaguliwa na kile ambacho huenda wakapuuza ingawa watajua kuhusu jinsi ya kuyawakilisha maeneo bunge yao, kuhusu jinsi ya kuongoza, kuhusu maamuzi ya kidemokrasia, na kuhusu haki zao na majukumu yao katika katiba.
Viongozi ni Kundi lenye Athari kubwa
Pamoja na umuhimu wa elimu ya uongozi katika kutekeleza demokrasia, kuna faida nyingine kwamba viongozi ni kundi lenye athari kubwa. Kubadilisha tabia, mienendo, na kiwango chao cha elimu kunaweza kuwa na athari kubwa kwa wafuasi wao na kwa jumbe watakazowaeleza wafuasi hao.
Makundi mbalimbali ya viongozi yanaweza kutambuliwa na mipango kujengwa nyakati za uchaguzi na katikati ya chaguzi. Katika nchi ambamo uongozi wake unaelekea kuwa wa kisasili na unachukuliwa kuwa wa kurithishana, mipango kama hiyo hasa inaweza kuwa muhimu na kuwekwa siasa nyingi.
Viongozi wa jamii, wawe wameteuliwa, wamechaguliwa, wamekabidhiwa, au wamezaliwa, ndio mwanzo wa moja kwa moja. Pamoja na mahitaji yao wenyewe ya kielimu, wao pia hutoa nafasi ya kuweza kuzifikia jamii wanazowakilisha. Viongozi wa kitamaduni wana uhusiano wa kiimani na jumuia zao ambalo hufanya iwe vigumu kufanya shughuli yoyote ya kielimu bila kupata idhini au usaidizi kutoka kwao.
Kwa ufupi, kutoa mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa kisiasa, kijamii, au kitamaduni, kujenga uhusiano wa kuaminiana, kuwapa habari iliyo muhimu kwa wakazi wa maeneo yao ya uongozi, na kuwapa nafasi ya kuchangia, kutaongeza imani yao ya kumiliki sehemu ya mipango ya elimu kwa wapigakura, hivyo basi kuongeza uwezekano wa kufaulu.
Kupata Nafasi za Kielimu
Katika maisha ya kisiasa ya nchi hiyo, viongozi waliochaguliwa katika viwango vya mitaa, maeneo, au vya kitaifa mara nyingi huingia kwenye shughuli inayofanya kuwa vigumu kabisa kwao kujielimisha au kubuni mipango ya kujielimisha, wenzao, makao makuu ya vyama au kamati za bunge. Isitoshe, kuna mwelekeo unaoongezeka wa mipango ya utangulizi na mafunzo iliyoidhinishwa au kupangwa na vyama vya kisiasa na asasi wanamochaguliwa.
Sehemu za Mafunzo
Mafunzo ya uongozi wa vyama vya kisiasa siku zote utakuwa na uwili mtindo, na hivyo huenda waelimishaji wakapata ugumu kutenganisha viwili hivyo. Cha kwanza ni haja ya kushindana vilivyo katika chaguzi na kuhakikisha kwamba wana upeo wa juu zaidi kuliko vyama. Cha pili ni dhana ambayo mara nyingi huelezwa kama upinzani zingatifu, k.m. pande zote mbili ziwe mamlakani au nje ya mamlaka zinapaswa kuwa na jukumu la kuhakikisha uhalali wa matokeo ya uchaguzi na usimamizi wa asasi na watahitaji kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuafiki lengo hili.
Mipango ya mafunzo ya mawakala wa vyama kwa mfano, yamefanywa ipasavyo katika vyama vyote vya kisiasa. Mingine iliyofaulu ni mipango ya kutoa habari ili kuhakikisha kwamba maafisa wote wa vyama wanakuwa na uelewa sawa kuhusu kanuni za uchaguzi na hatua za upigaji kura na kwamba wanaelewa wajibu wao kuzingatia sheria au kutozwa faini na adhabu nyingine wakizikiuka. Shughuli hizi hufanya kazi zaidi ya kupitisha ujumbe tu kuhusu uchaguzi: hujenga ushirikiano na uaminifu kati ya wapinzani na kujenga uhusiano kati ya viongozi ambavyo ni muhimu migogoro inapozuka. Mwisho, mipango kama huhakikisha kwamba kuna kundi kubwa la viongozi walio na habari kamili kuhusu masuala ya uchaguzi ili waweze kutoa habari kuhusu chaguzi na kwa wakati huo huo wanavyoshughulika katika kung’ang’ania mamlaka.
Halmashauri za kusimamia uchaguzi inapaswa kuhakikisha kwamba taarifa zao kuhusu:
- sheria ya kuongoza uchaguzi au sheria zozote zinazoongoza uchaguzi
- kanuni kuu za uchaguzi
- mienendo bora wakati wa uchaguzi
- wajibu, haki, na majukumu ya wagombea na mawakala wao
- mipango inayofanywa kuhusu upigaji kura, kuhesabu kura, kutayarisha na kutangaza matokeo, na usalama
- hatua za kuongoza malalamishi na utatuzi
- wajibu wa halmashauri ya kusimamia uchaguzi
Hili linaweza kuchochea ujenzi wa elimu ya jumla kuhusu demokrasia kwa viongozi wa kisiasa wanaoshughulika na masuala ya utamaduni wa kidemokrasia, wajibu wa upinzani, na mipango ya kubadilishana mamlaka ambako kutafuatia baada ya uchaguzi, hasa uchaguzi wa kwanza. Hatua kama hizo zinaweza kutolewa na mawakala badala ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi, japo halmashauri hiyo inaweza kuzianzisha na kuendelea kushiriki katika viwango mbalimbali.