Kuna nchi chache zinazokubali matumizi ya lugha moja. Hata nchi hizo ambazo zina lugha rasmi ya serikali, kwa faida ya kibiashara na urasmi wa elimu hiyo, na kwa faida ya umma, zinaweza kuwa na wananchi ambao hutekeleza shughuli zao katika lugha tofauti. Kunaweza kuwa na kundi kubwa la watu waliohamia katika eneo hilo. Au uwepo wa makabila mengi katika nchi unaweza kuhusisha uwepo wa lugha nyingi. Kwa vyovyote vile, waelimishaji watalazimika kuzingatia kiwango cha elimu inayotolewa katika lugha ya mama ya eneo hilo, tofauti na (ikiwa hii ndiyo hali) lugha rasmi ya nchi hiyo.
Kuna mazingatio kadhaa ambayo waelimishaji wanapaswa kuzingati. Kwa jumla, watu wazima husoma vizuri katika lugha ambazo wanahisi utulivu. Pale ambapo elimu hiyo inajumuisha kusoma, matini katika lugha ambazo watu husoma katika kazi nyingine (magazeti na vitabu) ni bora kabisa. Kunaweza kuwa na vizingiti, hata hivyo hivyo ni lazima vikabiliwe.
Mipaka ya Kisheria
Halmashauri za kiserikali za kusimamia elimu zinaweza kuwekewa mipaka ili zitoe nyenzo na elimu katika lugha rasmi peke yake. Sera kama hiyo inaweza kujengwa ili kuhimiza umoja wa taifa katika jamii iliyo na makabila mengi au kwa sera nyingine kama hizo. Ila pale ambapo kuna sera ya kitaifa kuhusu ufundishaji wa lugha na mwafaka kuhusu mwelekeo huu, hata hivyo wale wasiozungumza lugha inayozungumzwa na watu wengi wanaweza kupata kwamba elimu ya wapigakura inayowasilishwa katika lugha rasmi inaweza kuwa chapwa na isiyojumuisha watu wengi, hivyo basi ikakosa kuwa na mchango mzuri katika shughuli ya ujenzi wa taifa.
Hata nchi ambazo kwa kiwango kikubwa ni karibishi na huwaruhusu wahamiaji na wakazi wa muda kujifunza lugha rasmi hutoa habari kwa umma katika lugha mbalimbali au kutoa matini sambamba. Punde kunapokuwa na makubaliano ya kutoa nyenzo za kuelimishia katika lugha mbalimbali na pengine hata katika lahaja mbalimbali za kimatamashi au kimaandishi, matatizo hutokea mara moja na kuwatatiza waelimishaji.
Istilahi
Mengi katika maneno yanayotumiwa katika elimu kwa wapigakura, na vilevile katika elimu kwa raia, husukwa katika lugha kuu za kimataifa. Huenda maneno hayo yamekuwa ya kisasa katika lugha kuu ya biashara na serikali, au lugha hii inaweza kwa hakika kuwa lugha ya kimataifa. Lugha nyingine hata hivyo, huenda zisijumuishe dhana zote za demokrasia. Katika visa vingine haya yanaweza kutafsiriwa vibaya, mara nyingi katika kauli ndefu na zisizoeleweka rahisi badala ya dhana au maneno yenye uwazi, au huenda yasitafsiriwe kabisa. Moja katika athari mbaya za hili ni uwezekano kwamba watu wanaweza kuhisi kuwa dhana hizo si zao au wamelazimishiwa.
Jukumu kubwa hivyo basi huwa kwa waelimishaji kuhakikisha kwamba kuna kushirikishwa kwa dhana. Hili linaweza kupatikana kupitia tafsiri ya moja kwa moja au kwa tafsiri fiche kupitia kwa nahau na sitiari, kwa kubuni maneno na kauli katika lugha lengwa ambayo yana maana sawa, au kwa kuvumbua maneno mengine mapya na kauli mpya. Katika visa vingine, waelimishaji wanaweza kulazimika kutumia istilahi zinazopatikana katika sheria. Ili kuepuka kusababisha mchanganyiko mkaubwa, inaweza kuwa muhimu kwa mashirika yote na taasisi zote zinazohusika katika elimu kwa wapigakura, za kitaifa na za kimataifa, kutumia maneno yayo hayo, kauli, na dhana zizo hizo. Ili kurahisisha shughuli hii, waelimishaji wengine wamekuwa mstari wa mbele katika kujenga sherehe, kama makala za kujisimamia, ambazo hueleza, hutafsiri, na maneno ya kikundi, na ambazo zinaweza kutoa visawe na akronimu (tazama, kwa mfano Fungu lenye Matumizi mengi - Australia).
Zaidi ya kuibuka na istilahi za kujadili haki za upigaji kura na mchakato wa uchaguzi, tatizo moja lililomtatiza kila mwelimishaji katika hali ya ungi-lugha ni jinsi ya kupata kaulimbiu ya kuvutia. Mara nyingi kaulimbiu inaweza kufanya kazi vizuri katika lugha moja, na iwe au ionekane mbaya au ikose maana katika lugha zingine.
Uchapishaji
Uchapishaji pia hukabiliwa na tatizo maalumu katika jamii za ungilugha. Kutayarisha machapisho sambamba huzidisha gharama, kuongeza wakati wa matayarisho na wakati wa kutoa, na hivyo hakushughulikii vilivyo tatizo la istilahi. Katika visa vingi, wale wanaosoma lugha ya kiufundi wanaweza kuchagua kutumia lugha yenye uzungumzaji mpana. Kuna mifano mingi ya machapisho yaliyo yenye maana nyingi ambayo hayajasomwa.
Aidha, machapisho ya lugha sambamba mara nyingi hutolewa mara ya kwanza katika lugha moja na kisha kutafsiriwa katika lugha nyingine. Hili husababisha kuchelewa, kutolingana kwa viwango vya ubora na upangaji wa lugha hizo tofauti tofauti, na kuendelea kwa urazini wa wanafunzi.
Kumekuwa na majaribio ya kukabiliana na matatizo haya kwa kuanzisha machapisho mengine katika lugha tofauti tofauti, kwa kuanza na lugha tengwa na kisha kuitafsiri katika lugha yenye uzungumzaji mpana, au kwa kuwaweka katika kundi moja wandishi ili kutengeneza matini sambamba katika njia zinazolingana. Mwelekeo ambao umefaulu kabisa unaonekana kuwa kutayarisha chapisho moja katika lugha mbalimbali. Hili lina faida ya kuonyesha umuhimu wa lugha hizi
Njia Mbadala ya Uchapishaji ambayo ni Nafuu
Mwelekeo mwingine ni kuteua lugha inayoeleweka na watu wengi na kisha kutayarisha matini ya kimsingi katika toleo jepesi la lugha hiyo pamoja na sehemu ya sherehe ambamo istilahi muhimu hutafsiriwa katika lugha moja au nyingine zaidi. Umbo hili hukusudia kuwarahisishia watu uwezo wa kukubali uwepo wa lugha ya pili au ya tatu.
Mafunzo ya Waelimishaji
Waelimishaji wanaweza pia kukubaliana katika lugha tofauti tofauti. Kwa sababu hii, na kwa sababu ya ugumu wa kutekeleza kozi za kiufundi katika lugha nyingi au kutengeneza matini maalumu katika lugha nyingi, inawezekana kupata linguafranka. Waelimishaji wawa hawa hata hivyo, watahitaji kutekeleza mipango yao katika lugha yao ya nyumbani. Kwa sababu hii, ratiba za mafunzo zinapaswa kushirikisha mazoezi ambamo lugha mbalimbali hutumiwa, na nyenzo zilizotayarishwa ili zisambazwe zinapaswa kutafsiriwa ama wakati wa kozi hiyo au kabla ya kozi yenyewe, ili ziweze kuwasilishwa na kutolewa kwa lugha mwafaka.
Elimu ya Ana kwa Ana
Katika baadhi ya jamii zenye wingilugha, inawezekana kumhusisha mwelimishaji na kundi shiriki. Hii bila shaka ndiyo njia bora kabisa, ingawa haiwezekani siku zote. Huenda mikakati kadhaa ikalazimika kuanzishwa ili kuhakikisha kwamba watu wanaelewana.
Njia moja, na ambayo pengine ndiyo ghali sana, ni kutoa tafsiri za papo kwa papo. Ikiwa haiwezekani kutoa vifaa na watafsiri kumpa kila mtu mtambo wake wa kusikiliza, inawezekana kuwaweka watu katika makundi kutegemea lugha zao na kuwa na mtu wa kuwasaidia hapo karibu nao. Inawezekana pia kutoa tafsiri ya kauli kwa kauli punde baada ya mzungumzaji. Zaidi ya hayo, mkalimani anaweza kutoa muhtasari. Mbinu hizi zote zinahitaji watafsiri wenye ujuzi; na pale ambapo mitambo ya hali ya juu inatumika, watafsiri hawa wanaweza kutaka mafunzo zaidi.
Hata hivyo, wakalimani waliojifunza kufanya kazi hiyo huenda wakakosa kuelewa tofauti ndogo za kimaana katika lugha ya kisiasa, na wakalimani wa kijamii wa eneo hilo wanaweza kufanya kazi nzuri hapo. Kama shida ni vifaa vya lugha ya maelekezo badala ya ufahamu wake, inawezekana kutoa maelekezo katika lugha moja na kuwa na maozezi katika lugha nyingine, huku watu wakigawika kutegemea lugha. Maswali yanaweza kutokezwa katika lugha moja na kusambazwa kwa karatasi au vijitabu vilivyo na lugha zote. Mjadala unaweza kuwepo kwa misingi ya ungilugha huku watu wakizungumza lugha yao na kutoa muhtasari wenyewe au kuwa na mshiriki mwingine anayetafsiri hayo.
Pale ambapo mwelimishaji ni mgeni katika eneo hilo, inaweza kuwa bora kwa mtu huyu kuwa na mkalimani badala ya kuhusishwa tu katika mfumo huo. Cha ajabu, kuweza kufikia kila wanachosema watu kunaweza kufanya shughuli nyingine wazi kabisa kwa waelimishaji, kama vile maingiliano na maswali baina ya makundi na ambayo, kwa sababu ya haja ya tafsiri, huishia katika mjadala wa kidhana.