Kutokana na kuongezeka kwa elimu ya kitaifa ya umma, hasa kuhusiana na afya, japo pia katika nchi nyingine, kuhusiana na maswala ya kikatiba, maendeleo, kisiasa, kiuchumi na haki za binadamu, sasa hivi kuna mifano ya kutosha kutoa mapendekezo ya mabadiliko kuhusu mienendo bora. Mipango ya kitaifa ya elimu kwa wapigakura ni mfano mmoja tu. Mipango mingine inajumuisha harakati za kuelimisha kuhusu ukimwi na kampeni dhidi ya uvutaji, dawa za kulevya na kutochafua mazingira. Hili huwa kweli haswa kwa kampeni zinazohusu mazingira, japo katika siku za hivi karibuni mtu anaweza pia kuangalia kuhusu mipango ya kukabiliana na uchimbaji wa migodi na hatua nyingine mbalimbali.
Mipango ya elimu kwa umma ni shughuli za kufurahisha, katika umbo lake la sasa, la kuongezeka kwa kuzifanya habari hizi ziwe za kidemokrasia na za kitandawazi. Serikali na asasi za kibinafsi zinalazimika kutegemea mipango ya elimu badala ya kulazimisha au kutumia habari za uongo ili kubembeleza raia kubadilisha tabia zao. Mabadiliko ya haraka hutatiza uwezekano wa kufanya hivi polepole kupitia kwa mfumo rasmi wa elimu, pale ulipo; na kwamba mabadiliko kama hayo ya kielimu na habari pia hupunguza uwezekano wa miundo ya mahusiano ya kijamii kukamilika. Licha ya kuhitajika kwake katika miktadha mingine, hata hivyo uchache wa kifedha, kujitolea kisiasa, na mfano halisi vinaweza kudhibiti kiwango na ubora wa mipango ya kuupa umma habari, ikiwa ipo.
Kundi la mienendo bora lilipo hapa chini ni finyu kiupana. Linaweza kubadilishwa na liko huru kuchunguzwa na kutathminiwa. Isitoshe, kunaonekana kuwa na vipengele na mbinu sawazishi ambazo ni bora kushinda nyingine. Hivi ni pamoja na:
- Kupanua mtandao na kujenga mashirika ili kuhakikisha mazingira bora ya kuanzisha na kutekeleza mpango
- Kuhakikisha uwepo wa mikakati ya umuliki na kupatikana kwa majibu
- Kutambua, kuelewa na kutumia mashirika na asasi kuwasiliana na maeneo ya uwakilishi, ukihakikisha kwamba
- Uwezo wa kufikia makundi maalumu lengwa ni kupitia kwa makundi yaliyopo yanayoaminika
- Mawasiliano yanafanywa na wale wanaoelewa na ambao tayari hutumia lugha na vyombo mwafaka vya habari, ikiwa ni pamoja na mawasiliano ya ana kwa ana ikihitajika
- Ujumbe wa elimu kwa umma huenezwa haraka kwa makundi lengwa mengi katika muda mfupi
- Kupanga vizuri malengo na ujumbe wa mafunzo pamoja na watu na mashirika ambayo ni wakilishi ya makundi lengwa kwa misingi ya mahitaji halisi bali si mahitaji ya mpango peke yake
- Kujenga mazingira mwafaka ili mazingira ya kisheria, kitamaduni, na ya shirika yaweze kukuza badala ya kutatiza mienendo inayopendekezwa na malengo ya wanafunzi
- Kutoa usaidizi unaohitajika wa kielimu na kiusimamizi kwa kutayarisha nyenzo mwafaka za kutekelezea elimu ili kuelimisha kundi moja baada ya jingine
- Kutoa mafunzo kwa wafundishaji, kuwatambulisha kwa nyenzo hizo, na matukio ya kusaidia watumizi wake
- Kupeana makundi rejelewa ya kitaifa na ya kieneo na kuimarisha kampeni
- Kujenga usaidizi wa kitaifa wa vyombo vya habari, hasa kupitia matangazo ya redio na nyenzo nyingine za ziada zitakazofaa kwa vyombo vilivyopo vya habari vya kutangaza na vya kuchapisha
- Kujenga uhusiano wa kiasasi ili kuhakikisha uwajibikaji wa kifedha, uongozi na utekelezaji bora, na kuwajibikia umma
Kila mojawapo ya kanuni hizi zimeelezwa zaidi katika sehemu nzima ya mada ya Elimu kwa Wapigakura.