Orodha ya mwisho ya wapigakura huundwa kupitia kwa mchakato wa tarakilishi ama kwa kuandika kwa mikono tu taarifa kutoka kwenye orodha asilia ya wapigakura, pamoja na taarifa kutoka kwenye mahakama ya urejelezi. Vyovyote vile orodha hivo hutolewa kwa vitengo vidogo vya usimamizi ambavyo vinaweza kuwa 100 au zaidi katika kila eneo la uchaguzi. Kisha orodha hiyo itapangwa ama kijiografia (k.v. kwa kurejelea makao) au kialfabeti, au kwa kuambatanisha mifumo yote miwili.
Utoaji wa Orodha katika Kituo Kikuu au katika eneo la matumizi
Katika sehemu nyingine halmashauri kuu ya kusimamia uchaguzi huunda orodha ya mwisho ya wapigakura, hasa kama ilihifadhiwa kwenye tarakilishi. Halmashauri za kieneo za kusimamia uchaguzi hutuma faili kwa halmashauri kuu ya kusimamia uchaguzi ambayo huiweka deta hiyo pamoja katika orodha moja ya wapigakura. Hii inaweza kuchapishwa katika ukamilifu wake na halmashauri yenyewe au eneo pana la kusimamia uchaguzi au kituo cha kupigia kura. Mara nyingi hata hivyo, orodha hiyo huchapishiwa pamoja. Changamoto ya wakati ndiyo hutatiza utoaji wa pamoja wa orodha ya muda ya wapigakura na kwa ambapo kutokana nazo usajili hufanyika katika kipindi cha uchaguzi. ikiwa orodha za wapigakura zinatunzwa na kuchapishwa katika maeneo ya utumizi wake, ofisi za kieneo zinapaswa mifumo ya tarakilishi na mashine za kuchapisha vinavyohitajika katika kukamilisha shughuli hiyo ipasavyo.
Kituo cha kupiga kura, au tarafa, kwa kawaida ndicho huwa kitengo kidogo cha uchaguzi na mara nyingi huwa na takribani wapigakura 400. Katika masuala ya kiusimamizi, ndicho kitengo cha kutayarisha na kuchapisha orodha ya wapigakura.
Katika sehemu nyingine, ofisi za kieneo za kusimamia uchaguzi hutengeza orodha ya mwisho ya wapigakura inayopawa kutumiwa katika eneo hilo. Ofisi ya kieneo inaweza kutuma nakala ya orodha hiyo kwa halmashauri kuu ya kusimamia uchaguzi japo inachukua jukumu la kutengeneza orodha hiyo.
Hakuna Orodha Tofauti za Wapigakura na Sajili ya Raia
Nchi zinazotumia sajili ya raia hazina idara tofauti au mashirika tofauti ya kushughulikia orodha ya wapigakura kivyake katika sajili, na na huenda hata zikakosa orodha yenyewe kabisa. Katika nchi moja ofisi ya kieneo ya kushughulikia ushuru hutunza rekodi kwa wakazi wote katika eneo lake. Kuna wajuzi wanaoshughulikia kwa wafanyakazi wake lakini haina kitengo tofauti cha usajili. Isitoshe, hakuna orodha yoyote maalumu ya wapigakura inayochapishwa. Badala yake, orodha hiyo ya wapigakura ni sehemu tu ya rekodi zinazowekwa katika rejista ya watu. Rejista hiyo haifungwi kwa sababu hutekeleza wajibu muhimu katika kutoa taarifa kwa idara na mashirika ya serikali, na vilevile kwa sekta ya kibinafsi (k.m. benki na makampuni ya utoaji bima). Hata hivyo, kunaweza kuwa na tarehe ya mwisho ya kutambua ustahifu wa mtu kupiga kura na eneo pana la uchaguzi ambapo mtu anaweza kupigia kura. Mabadiliko yoyote baada ya tarehe hii yanaweza kunakiliwa katika sajili ya raia lakini haitaathiri uwezo wa mtu kushiriki katika uchaguzi huo au kituo cha kupigia kura ambako atapigia kura.