Manufaa ya BV
Block vote husifiwa kutokana na uwezo wake wa kuwapatia wapigaji kura uwezo wa kuchagua wagombeaji binafsi na kuruhusu uwepo wa wilaya kubwa kijiografia, huku ikiongeza jukumu la vyama ikilinganishwa na FPTP na kuimarisha vyama hivyo ambavyo vinaonyesha mshikamano zaidi na uwezo wa ushirikiano.
Udhaifu wa BV
Hata hivyo, Block Vote huweza kuwa na athari zisizotabirika na kawaida zisizopendeza kwenye matokeo ya uchaguzi. Kwa mfano , wakati wapigaji kura wanapopiga kura zao zote kwa wagombeaji wa chama kimoja, mfumo huu huelekea kubainisha mitazamo hasi ya FPTP, hasa ukosefu wake wa usawazishaji. Chama kinapomteua mgombeaji kwa kila nafasi kwenye mfumo wa Block Vote na kuwahimiza wapigaji kura kuchagua kila mgombeaji katika kundi lao, hali ambayo inawezekana. Kwa mfano, nchini Mauritius mwaka wa 1982 na 1995, chama cha upinzani kabla ya uchaguzi walishinda kila kitu katika bunge huku kikiwa na asilimia 64 ya viti na asilimia 65 ya kura zote. Hili lilisababisha matatizo makubwa katika kufanikisha shughuli nyingi bungeni kutokana na wazo la kuwa na serikali pamoja na upinzani. Mutumizi ya viti vya aliyeshindwa kabisa nchini Mauritius lilichangia tu udhaifu wake.
Huko Thailand, mfumo wa Block Vote ulionekana kuhimiza kutawanyika kwa mfumo wa chama. Kwa sababu unawawezesha wapigaji kura kupigia kura wagombeaji wenye zaidi ya chama kimoja kutoka wilaya moja, wanachama kutoka chama kimoja huhimizwa kushindania ufuasi. Mfano wa Block Vote kawaida huonekana kama wenye kuchangia maendeleo na ufisadi ndani ya chama.
Katika miaka ya hivi karibuni, nchi nyingi zimeacha kutumia mfumo wa Block Vote na kutumia mingine.Thailand na Philippines walibadilisha mfumo kutoka BV hadi mfumo mchanganyo katika miaka ya mwisho ya 1990. Katika hali hizi mbili, sababu tosha za mabadiliko zilikuwa ni umuhimu wa kupiga vita ununuzi wa kura na kuimarisha maendeleo ya vyama vya kisiasa.

