Kimuundo, List PR huhusu kila  chama  kikiwakilisha  orodha  ya  wagombeaji kwenye  tume  ya uchaguzi  kutoka kwa kila  wilaya yenye  uanachama  zaidi ya  mmoja. Wapigaji kura huchagua chama na vyama hupokea viti kulingana na mgao wake  wa kura  katika  wilaya  ya  uchaguzi. Wagombeaji wanaoshinda  hutolewa  kwenye  orodha  kulingana  na  nafasi  zao  kwenye  orodha . Uteuzi wa List PR hauelezi bayana   mfumo wa uchaguzi: habari zaidi lazima zielezewe. Mfumo unaotumIwa  kuhesabu  utoaji wa  viti baada ya  kura  kuhesabiwa  huweza kuwa ya mbinu ya Highest Average  au Largest Remainder. Fomula  inayochaguliwa  huwa  na athari  ndogo lakini  wakati  mwingine  huwa muhimu kwenye  matokeo ya uchaguzi chini ya PR. Huko Cambodia mwaka wa 1998, badiliko kwenye  fomula  wiki  chache  kabla  ya siku ya  uchaguzi  lilikuwa  na athari  ya kupatia  chama  kikubwa  viti 64, badala ya  59 kwenye bunge  la  wawakilishaji 121. Badiliko hili halikuwa limetangaziwa umma ilivyohitajika, na upinzani ulikubali matokeo shingo upande. Mfano huu hueleza kwa uwazi umuhimu wa wapangaji wa mfumo wa uchaguzi kudhihirisha maelezo yote hata yale madogo.

Karatasi ya Kura ya List PR iliyo Funge huko Cambodia 
Kuna masuala mengine muhimu ambayo yanahitaji kushughulikiwa katika kueleza kwa uwazi jinsi mfumo wa list PR utakavyofanya kazi. Kiwango cha  juu rasmi huhitajika  kwa uwakilishaji  bungeni: kiwango cha juu (kwa mfano asilimia10 kama inavyotumika Turkey) huweza kutenga vyama vidogo, huku  kiwango cha  chini (kwa mfano asilimia 1.5, kama inavyotumika Israel) huweza kuimarisha uwakilishaji wao. Huko Afrika Kusini, hakuna kiwango cha juu rasmi na katika mwaka wa 2004 chama cha African Christian Democratic Party kilishinda viti sita kutokana na viti 400 kikiwa tu na asilimia1.6 ya kura za taifa. Mfumo wa list PR pia  hutofautiana  kutegemea  jinsi na vile mpigaji kura huweza kuchagua wagombeaji  pamoja  na  vyama yaani ikiwa orodha  ni funge  au wazi, uteuzi  huu  huwa  na  athari  kwenye  uchangamano wa  karatasi ya kura. 
Teuzi zingine  hujumlisha  mipango rasmi au isorasmi ya ‘uletaji  pamoja  wa  kura’; upana wa makubaliano kati ya vyama, kama ule unaotolewa  na  mifumo yenye  kutumia uwazi: na  kuweka  wazi mipaka  ya wilaya. 
 
