Taarifa kwa Chaguzi za Kisasa
Kama ilivyotambuliwa mwanzoni mwa sehemu hii, dhana habari kwa mpiga kura inatumika mahususi kurejelea maswala muhimu ya chaguzi, yaani mahali pa kupiga kura, lini, na vipi. Fikra dhanifu kuhusu ufaafu wa mipango ya elimu kwa Wapigakura ya kudumu au shuku kuwa elimu kwa Wapigakura kwa njia fulani inaashiria kampeni zenye miegemeo au mapendeleo zimechangia katika hali mbalimbali ambapo wasimamizi wa uchaguzi wameamua kuwa kazi yao kimsingi ni ile ya kutoa habari kwa Wapigakura.
Utoaji wa Taarifa ni Jukumu la Halmashauri ya Kusimamia Uchaguzi
Licha ya kuwa tahadhari yoyote iliyotolewa inafaa kuwa kweli – elimu kwa Wapigakura inaweza kuwa fanifu na isiyo na mapendeleo – kuna maoni kuwa wasimamizi wa uchaguzi wenyewe wanafaa kumakinikia habari kwa mpiga kura na kuwacha kazi zaidi za utoaji wa elimu kwa Wapigakura, na kazi za utoaji elimu kwa raia kwa ujumla kwa mashirika mbalimbali.

Kwanza, wasimamizi wa uchaguzi ndio pekee walio na habari zinazohitajika. Wanaelewa zaidi sharia za uchaguzi, masharti na tamaduni. Na ni juu yao kueneza habari zinazo hitajika na wagombezi na Wapigakura. Uingiliaji kati ya elimu kwa upande mwingine unahitaji malighafi zaidi na kumakinikia juhudi ambazo zinaweza kuenda zaidi ya wajibu wa kiutawala wa wasimamizi wa uchaguzi. Kiasi ambacho wasimamizi wa uchaguzi wanaweza kuenda zaidi ya habari za kimsingi kwa Wapigakura na kuingia katika uwanja wa elimu inaweza kushurutishwa na kazi yao kulingana na sheria. Ikiwa wasimamizi wa uchaguzi ni lazima au kivingine wameamua kubakisha shughuli zao kwa utoaji habari kwa Wapigakura, bado itakuwa na kazi ya kutekeleza katika ukuzaji wa mikakati ya kuhimiza watu wengine katika jamii kuendelea na shughuli za utoaji elimu kwa Wapigakura. Kuhusiana na habari zinazohitajika vile vile inafaa kutokana na uelewa kamili wa mahitaji ya Wapigakura na kutokana na maoni mazuri na ya mara kwa mara.
Kuelewa Mahitaji ya mahali hapo
Kwa sababu habari mara nyingi huwa zinazohusiana na mahali pale – mahali palipo na vituo vya kupigia kura, orodha ya wagombezi, na kadhalika – mipango ya utoaji habari kwa Wapigakura inafaa kuunda njia ambazo inaweza kutumia, kuhitikia, mahitaji ya kimahali na ufahamu wa mahali. Katika nyingine, hii hufanyika kwa kuteuwa maafisa wa habari katika hali zingine, maafisa wasimamizi wana jukumu la kutoa maelezo ya kimahali.
Jukumu muhimu la vyombo vya habari
Njia yoyote inayochukuliwa, watu kama hao wanafaa kukuza uhusiano mwema na vyombo vya habari. Vyombo hivi vya habari huwa ndiyo njia ya pekee iliyopo yakupata habari kutoka kwa watu wengi katika muda mfupi wa wakati. Taarifa kwa waandishi wa habari na maelezo mafupi kwa waandishi wa habari yanapohusishwa na utoaji wa maandishi na vifaa vya kuandikia kwa waandishi wa habari inaweza kuwa mojawapo ya mahitaji muhimu ya Mpango wa habari za kimahali (Tazama Vyombo vya Habari kwa Jumla).
Upimaji wa wakati wa kutoa habari
Katika wakati ufaao
Kila mara huwa haiwezekani kusimamia Mpango wa utoaji habari kwa uangalifu zaidi ili watu wapate habari wanazozihitaji kwa wakati ufaao ili waweze kuzishughulikia. Katika mazingira imara ya uchaguzi, ambapo mipaka ya kanuni na ya kisheria au makataa na mikakati muhimu ya uchaguzi bado iko katika hali ya kubadilika nyakati za uchaguzi na pale ambapo miundo msingi ya mawasiliano inakosekana, hii italeta changamoto kubwa.
Pale ambapo pana mifumo ya kisasa ya utangazaji na magazeti iliyoimarishwa na sekta ya utangazaji ya kisasa na miundo msingi bora ya mawasiliano inawezekana kutengeneza taarifa katika muda mfupi na kuiwasilisha katika wakati unaofaa.
Pale ambapo mifumo hii inafanya kazi katika mazingira ambapo idadi ya juuya watu wanasoma na kusikiliza au kutazama vyombo vya habari vinavyotangaza, basi habari hizi zinafaa. Mengi yanawachiwa bahati, hatahivyo hii inaweza tu kukabiliwa na mifumo ya habari ambayo inajirudia na imejenga katika uhifadhi na uziada.
Kuwafikia watu kwa njia bora na kwa wakati ufaao
Katika jamii masikini, umiliki wa radio na televisheni ni mdogo. Nguvu za umeme huenda zisiwe hoja. Katika jamii za kisasa na zilizoendelea hadhira imetawanyika katika sehemu mbalimbali. Katika hali hizi zote ni hatari kuwa na njia moja ya usambazaji wa habari.
Kwa upande mwingine, habari ambazo zina uwezo wa kuhifadhiwa – vijitabu na vifaa vingine vilivyo chapishwa, taarifa zilizonakiliwa, na vinginevyo ambavyo vinaweza kusambazwa na kuwekwa kwa Makala ya baadaye – lazima vibakie kuwa sahihi na vinavyopatikana kwa wakati ufaao.
Kwa hivyo kila mara kutakuwa na haja ya kusawazisha utoaji wa habari bora kwa watu na utoaji habari kwa watu walio wengi zaidi.
Kuandaa Ratiba yenye maelezo ya Kina
Katika upana wake, mipango inayohusiana na utoaji wa habari kwa Wapigakura inafaa kuzingatia wakati kwa umakini na Mpango wenye maelezo ya kina na toshelevu utahitajka. Ikiwa habari kwa mpiga kura ni ngeni, kwa sababu ya mabadiliko muhimu katika taratibu za upigaji kura au kwa sababu ya uchaguzi wa kwanza, basi kutakuwa na haja ya kuwa na kukagua vilivyo sehemu zote za mipango zinazohusika. Ukaguzi huu unaweza kutekelezwa kwa kuhakikisha kuwa kuna maoni yenye manufaa kutoka kwa mashirika na waelimishaji ambao wanafanya kazi nyanjani; au kutoka kwa habari na malalamishi yaliyotumwa kwa njia ya mtandao. Ni jambo la kushangaza kuwa, wasimamizi wa uchaguzi mara nyingi uchukulia kuwa watu wana habari iliyo katika hali nzuri kwa sababu tu imetolewa kwa umma.
Hata Ratiba za Wakati mwafaka Huhitaji Muda wa kutosha Kuzipanga
Hatimaye, pamoja na matatizo ya kijumla yaliyoelezewa kuhusiana na utoaji wa habari kwa watu kwa wakati ufaao, uundaji na usambasaji wa vifaa vya maandishi pia nao unachukua wakati na miundo mingine ya vifaa hivi vya maandishi itahitaji wakati zidi kuliko mingine. Utengenezaji na upeperushaji wa matangazo ya kibiashara kwenye redio unaweza kuafikiwa haraka zaidi, kwa mfano kuliko utayarishaji, utoaji wa nakala, ukunjaji, upakiaji, usafirishaji, na usambasaji wa vijitabu.
Taarifa za Elimu kwa Wapigakura
Hakuna taarifa za wastani ambazo zinafaa kutolewa katka Mpango wa utoaji wa habari kwa mpiga kura. Taarifa zote zinafaa kuwa mahususi kwa uchaguzi mahususi. Kuna hata hivyo, seti ya kategoria ambazo zinafaa kuzingatiwa.
Wakati na Tarehe ya Uchaguzi
Kipande cha habari chochote ambacho kinaweza kutokea katika kifaa chochote kilicho chapishwa kitahusisha masaa na tarehe za kupiga kura. Ingawa haya yanaweza kuwa sawa kote nchini, huenda isiwe hivyo katika mataifa makubwa. Kwa hivyo taarifa hizo zitahitajika kutayarishwa kulingana na maeneo.
Ingawa habari zinaweza kuanza kwa msukumo wa chini, wakati ambapo tarehe inakaribia, kunauwezekano kuwa habari hizo zitapewa umuhimu mkubwa katika mawasiliano kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi na pia wagombezi.
Nyakati na Tarehe za Usajili wa Wapigakura
Kwa sababu ya tofauti kubwa zinazo tarajiwa katika maeneo na mipaka, habari zinazotolewa kuhusiana na wakati na tarehe ya usajili wa Wapigakura huenda zikawa changamano zaidi. Katika hali halisi, kunaweza kuwa na vishawishi (potofu) vya kutoa habari zote kuhusianana usajili kupitia kwa njia moja. Vishawishi hivi vinafaa kuepukwa, na Wapigakura wanafaa kupata habari ambazo wanazihitaji na habari zingine za kina zinazohusiana na matarajio, changamoto, ukaguzi wa orodha, na kadhalika inafaa kutokea katika machapisho tofauti na changamano zaidi.
Haifai kuchukuliwa kuwa kwa sababu ya kuwa na habari zozote kuhusu kampeni, na hasa bila ya usajili wa Wapigakura, kuwa notisi ya kisheria kama inavyohitajika na sheria nyingi inatosha. Habari zinafaa kuwa mahali watu walipo, katika muundo ambaounavutia makini yao, na katika hali ambayo wanaielewa.
Mahali pa kujisajili
Labda sehemu ya usajili ya Wapigakura inayokanganya zaidi, isipokuwa ikiwa inawezekana kufanya hivyo kupitia kwa barua au kupitia kwa njia nyingine za mawasiliano ya posta, ni kupata mahali pa kujisajili. Isipokuwa wenye mamlaka wamechagua kutambua vituo spesheli ambavyo baadaye vinaweza vilevile kutumika kama vituo vya kupiga kura, kunawezekana kuwa usajili utafanyika katika maeneo mengi mbalimbali. Kutokana na hayo bango wastani ambalo linaweza kuonyeshwa hadharani linafaa kuweko kuashiria mahali pa kujisajili. Mabango kama hayo pia yanagutusha umma kuwa usajili unafanyika. Pamoja na haya, njia zingine za mawasiliano zinafaa kutumika. Labda njia ambayo haiwezi kutegemewa sana miongoni mwa hizi ni njia ya posta na simu, kwa sababu kunaweza kukosekana njia ya kuthibitisha kuwa ujumbe ulipokelewa na mpiga kura. Mahamasisho ya usajili yanalenga kushughulikiwa na ukweli kwamba kila mara watu wanatoka mahali pamoja kuelekea mahali pengine (wanahamahama).
Mahali pa Kupigia kura
Mahali pa kupigia kura kila mara huweza kutambulika kwa urahisi, mara tu mpiga kura anapoonekana. Hata hivyo, kituo cha kupigia kura kinachoonekana huenda kisiwe cha mpiga kura huyo. Katika miji ambako kuna vituo vingi vya kupigia kura, kilicho karibu huenda kisiwe ndicho kinachofaa. Jambo hili linaweza kuleta mkanganyiko mkubwa. Mkanganyiko pia unaweza kutokea wakati ambapo vituo zaidi vya kupigia kura vinapatikana katika mahali pamoja.
Pale ambapo uchaguzi umefanyika mara kwa mara katika kituo kile kile, na pale ambapo usajili umefanyika katika kituo ambapo mtu huyo anahitajika kupiga kura, habari kama hizo huenda zisiwe na umuhimu mkumbwa. Pale ambapo vituo vya kupigia kura bado vinaandaliwa baada ya usajili kufanyika, habari kama hizo ni muhimu na lazima zitolewe. Hata hivyo si rahisi kwa habari hizi kutolewa kwa watu, kwa sababu ni tofauti kwa kila seti ya Wapigakura. Mbinu mbalimbali zinatumiwa kukabiliana na hali hii, kama vile:
- kutuma kwa njia ya posta kadi ambazo zinathibitisha usajili na kuonyesha kituo cha kupigia kura
- kuweka Vibandiko na Mabango katika maeneo jirani
- kutoa habari kwa vyama vya kisiasa
- kutumia vituo vya redio vya kijamii (Tazama Vyombo vya Habari vya Kijamii)
- Kuchapisha habari katika magazeti ya kienyeji, moja kwa moja au kupitia kwa habari za vijalizo (habari zinazotolewa kama sehemu ya habari nyingine)
- kutangaza nambari za utoaji habari na vituo vya habari vya kienyeji na kimaeneo,
- ambapo maelezo ya kina yanaweza kutolewa kupitia kwa simu
Katika kila mojawapo wa hali hizi ainafulani ya mawasiliano ya kibinafsi yanahitajika, na kuna mikakati ya kutoa taarifa mara tu inapoombwa.
Mipango ya kijumla ya utoaji habari kwa mpiga kura itataka kutangaza mapema zaidi kuwa watu wanafaa kuthibitisha pale wanapotarajiwa kupigia kura, na wanafaa kuwapa habari zinazohusu namna ya kutekeleza haya.
Huduma Maalumu za Upigaji kura
Kwa kutegemea vibali vya kisheria, huenda kukawa na huduma mbalimbali maalum za upigaji kura ambazo zinatolewa kwa Wapigakura. Huduma hizi zinaweza kuhusisha upigaji kura na mtu bila ya lazima yake kuwepo, upigaji kura mapema (kabla ya siku rasmi ya kupiga kura, au kupiga kura kupitia kwa sanduku la kupigia kura la kutanga ( linalotembezwa kutoka mahali moja hadi kwingine) siku ya kupiga kura. Ili kuweza kutumia moja wepo wa huduma hizi, inawezekana kuwa Wapigakura watahitajika kufanya maombi kupitia kwa njia ya mdomo au maandishi. Na, huenda kukawa na muda mahususi ambao ombi hili linafaa kufanywa. Kwa sababu hii, itakuwa muhimu kwa waelimishaji kufahamisha Wapigakura kuhusu kuwepo kwa huduma muhimu, kutambua ni wapiga gani ambao wanaruhusiwa kutumia huduma hizi, na kutoa ratiba na njia ambazo huduma kama hizi zinaweza kuombwa.
Makala Zinazohitajika
Baada ya watu kujua mahali pa kupigia kura, wanafaa kufika kwenye vituo vya kupigia kura na nyaraka au hati zinazihitajika na zitakazowatambua na kuthibitisha kuhitimu kwao kupiga kura. Wasimamizi mbalimbali hutumia nyaraka tofauti, na uchaguzi wa nyaraka zifaazo kumtambua mtu ili aweze kusajiliwa kama mpiga kura huenda zikawatofauti na zile zinazohitajika siku ya kupiga kura.
Kuweka alama kwenye Kadi ya kupiga kura kwa njia sahihi
Wakati Wapigakura wanapoingia katika kituo cha kupiga kura, pia watahitajika kujua namna ya kutia alama inavyohitajika kwa kadi ya kura ili hatimaye iweze kuhesabiwa. Katika nchi ambapo kuna njia moja iliyozoeleka ya kutia alama kwenye kadi ya kupiga kura ambayo imetumika kwa muda fulani na pale ambapo hapajakuwa na marekebisho yoyote makubwa kwa muundo wa kadi, juhudi hizo bila shaka zitahitajiwa na wale ambao watakuwa wakipiga kura kwa mara ya kwanza.
Katika nchi ambapo kuna njia zilizozoeleka za kutia alama kwenye kadi ya kupiga kura katika aina tofauti za chaguzi, na pale ambapo njia mpya za kutia alama kwenye kadi ya kupiga kura zimeanzishwa, pale ambapo kumekuwa na mabadiliko makuu kwenye muundo wa kadi ya kupigia kura, pale ambapo viwango vipya vya serikali vimepigiwa kura kwa mara ya kwanza, au pale ambapo matumizi ya teknolojia mpya yameathiri utaratibu wa kutia alama na kupiga kura, kutakuwa na haja ya kuwa na Mpango wa elimu unaolenga Wapigakura wote.
Na kama kuna masharti ya jinsi ya kushughulikia karatasi za kupiga kura zilizoharibika, njia ambazo Wapigakura wanaweza kurudisha karatasi ambalo limetiwa alama visivyo na kulibadilisha na jingine lipya zinafaa kuelezwa.
Hatua za Kulinda kura
Kwa baadhi ya chaguzi, kunaweza kuwa na haja ya kuweka hatua mpya za kuhakisha usalama wa karatasi za kupigia kura ilikuhakikisha uhalali wa mchakato (shughuli) wa kupiga kura na matokeo ya uchaguzi. Kuna sababu kadha kuhusu ni kwa nini Wapigakura wanafaa kufahamishwa kuhusu hatua za kutoa usalama kwa karatasi za kupigia kura. Sababu ya kwanza ni kuwa baadhi ya hatua hizi zitaathiri moja kwa moja namna watakavyo shughulikiwa mara tu watakapoingia katika kituo cha kupigia kura. Mfano mmoja utakuwa ni matumizi ya wino usiofutika na matumizi ya mashine za kutazamia kura ili kutambua Wapigakura ambao tayari wamepiga kura. Kwa kuwa shughuli ya aina hii inaweza kuwa ngeni kwa utamaduni fulani, mitazamo fulani hasi au hata woga utafaa kuepukwa ili kuhakikisha kuwa hatua za kiusalama kwa karatasi za kupigia kura hazisababishi kuzuia watu kupiga kura.
Wakati huo huo, hatua zingine za kiusalama kwa karatasi za kupigia kura- kama vile matumizi ya karatasi maalum, pete za mihuri, vishina vilivyokatwa kutoka kwa karatasi za kupigia kura, au mistari maalum iliyozungushwa kwenye kingo za kura – inaweza kuonekana kuwa shughuli ya wafanyikazi ya wanoendesha uchaguzi peke yao. Hata hivyo, suala nzima la hatua za kiusalama kwa karatasi za kupigia kura linaongeza kiwango cha uaminifu wa mchakato wa upigaji kura na imani ya Wapigakura kuwa kura zao zitahesabiwa (mara moja tu) na kuwa matokeo yatahashiria matamanio ya watu. Kwa hivyo ili kuongeza kiwango cha imani ya umma, itabidi juhudi za pamoja zifanywe ili kuwafahamisha watu kuhusu hatua za kiusalama kwa karatasi za kupigia kura, Na juhudi hizi zinafaa kufanyika kabla ya siku ya uchaguzi kama njia ya kuwahimiza watu kujitokeza kupiga kura.
Wagombea
Wasimamizi wa uchaguzi watafahamisha watu orodha ya wale wagombezi ambao wameteuliwa au kusajiliwa kihalali kugombea uchaguzi, orodha hiyo inaweza tu kuwekwa kwenye ubao wa notisi nje ya afisi ya hakimu au ile ya afisaa anayesimamia uchaguzi. Lakini kunauwezekano kuwa inaweza kuchapishwa kwa wengi kupitia kwa vyombo vya uandishi wa habari.
Baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi hutoa chapisho ambalo hutoa habari za kimsingi kuhusu vyama vinavyogombea uchaguzi, ambayo huwa wamekabidhiwa na vyama vya kisiasa vyenyewe. Habari hizi hutarajiwa kuwafahamisha kimbele kuhusu propaganda na uchafulianaji majina ambao huenda vyama vya kisiasa vikazua. Hii pia inaweza kutekelezwa kupitia kwa maandishi yanayoandikwa katika vituo vya kupigia kura siku ya kupiga kura. Hatua ya hii sehemu muhimu ya uchaguzi wowote unaofanyika katika nchi ambapo mizozo ya kikabila au kimadhehebu imesababisha utengano wa vyama kijiografia na maeneo ambako watu wengine hawakubaliwi kuenda.
Viwango vya serikali vya kupigia kura
Wapigakura ambao hawaelewi sababu ya kufanywa kwa uchaguzi, na athari zinazotarajiwa kutikana na matokeo ya uchaguzi wako katika hali ya upungufu, Ni vigumu kwao kufanya maamuzi mazuri na pia ni rahisi kwa wao kupotoshwa au kupewa habari zisizofaa. Kwa hivyo habari zifaazo kuhusu afisi inayopigiwa kura na majukumu na wajibu, namna ambavyo kura zitahesabiwa katika baadhi ya hali kuchangia katika nafasi, na mfumo wa serikali ambao utakuwepo yote ni muhimu katika Mpango wa utoaji habari kwa Wapigakura. Ingawa Mpango wa kuelemisha wapigakura unaweza pia kusaidia wananchi kuelewa mifumo hii, Mpango wa utoaji habari unaweza tu kutoa habari za kimsingi ambazo zimepatikana kutoka kwa idara zingine za serikali.
Kanuni za Maadili mema
Hatimaye, chaguzi ni vinyang’anyiro vya mamlaka. Kwa hivyo, sheria nyingi za uchaguzi huweka kanuni za maadili mema kwa vyama vya kisiasa. Au wanaweza kuorodhesha namna ambavyo sharia ya uchaguzi inaweza kusemekana kuwa imevunjwa na adhabu zinazohusika. Wananchi ndio walinzi bora zaidi dhidi ya makosa yanayoweza kufanywa na mgombezi, lakini wakiweza tu kufahamu ni nini cha kutarajiwa kutoka kwa vyama. Usambazaji mpana wa kanuni za maadili mema utasaidia kupunguza mizozo.
Vilevile, chaguzi ni huduma ambazo zinatolewa na nchi, au kwa niaba ya nchi, na tume huru. Wanachi wanahaki ya kujua aina ya huduma ambayo wanafaa kutarajia; na uchapishaji wa habari hizo pia unalinda dhidi ya usimamizi mbaya na uwezekano wa matendo yaliyo kinyume na sharia au udanganyifu.
Picha:
Ujerumani, Berlin: taarifa kuhusu uchaguzi Bunge la Ulaya imeidhinishwa chini ya Creative Commons Attribution-Noncommercial-No Derivative Works 2.0 Generic License.