Vyama vya kisiasa hushindana. Elimu kwa Wapigakura huchukuliwa kuwa shughuli isiyoegemea upande wowote au isiyopendelea. Kwa hivyo kuna uchukulio wa kijumla unaoongoza shughuli hii kuwa elimu kwa Wapigakura haihusiki na vyama vya kisiasa. Dai hili si kweli kwa sababu mbili. Kwanza, watu binafsi na makundi ya watu hujifunza mambo mengi kuhusu uchaguzi na kuhusu demokrasia kutoka kwa mwingiliano wao na serikali na tajriba zao za kisiasa. Pili, vyama vina malengo yao ya kibinafsi wakati wanapowaendea Wapigakura na hivyo, inaweza kuwa njia nafuu ya kuhakikisha kuwa Wapigakura wanapata habari zifaazo na wanazozihitaji ili waweze kupiga kura. Kwa hivyo, vyama vya kisiasa na wafuasi wao, maafisa wa kuendesha kampeni, na wafanyikazi wa kawaida kwa hakika wanaweza kuwa waelimishaji. Kazi ya mwelimishaji wa Wapigakura ni kusimamia malighafi haya muhimu na yasiyoweza kuzuilika kwa njia ambazo zinawanufaisha wananchi.
Hakikisha kuwa Vyama Vina Habari Sahihi
Vyama vya vya kisiasa vina haja katika kuhakikisha kuwa wafuasi wao wanawasili katika eneo la kupigia kura linalostahili na kwa wakati ufaao na wapige kura yao ili iweze kuhesabiwa. Huenda wasiwe na haja ya kutoa habari hizi kwa watu ambao si wafuasi wao au hawawaungi mkono, lakini watu hao huenda wakafikiwa na vyama vya kisiasa vingine. Kwa hivyo, waelimishaji watataka kuunda mikakati ili kuhakikisha kuwa vyama vya kisiasa vyote vina habari sahihi kuhusu mchakato wa upigaji kura uliopo.
Hizi si habari pekee ambazo vyama vina haja ya kuwafahamisha Wapigakura kwa njia sahihi. Vyama vyote vitataka wafuasi wao kujua:
- kanuni ambazo huenda zikavunjwa na vyama vingine
- jinsi ya kukagua na kutathmini orodha ya Wapigakura
- nini kinaweza kusababisha kuondolewa au kufutwa kwa mtu kama mgombezi au mpiga kura
- wapi na vipi pa kuwasilisha malalamishi au kukata rufaa / pinga uamuzi
- ni nini kinachofaa kuchunguzwa wakati wa kampeni, siku ya kupiga kura, na kipindi kinachofuata baada ya uchaguzi
Ili kutekeleza haya, vyama vya kisiasa vitataka kuunda uelewa wa ndani kuhusu sharia na kanuni zote zinazotawala kampeni na mchakato uchaguzi na huenda wakataka kutoa uelewa huu kwa wanachama na wafuasi wao.
Kwa kweli, kunaweza kuna na baadhi ya vyama vya kisiasa ambavyo vina nia ya kuhakikisha kuwa watu hawana ufahamu wa haki zao za kikatiba na kimahakama, kuhusu mchakato wa uchaguzi, na kuhusu kanuni za demokrasia. Hata hivyo, elimu kwa Wapigakura iliyo pana nay a kina na ambayo ni sahihi na ya kuwapa nguvu, itakuwa haja ya baadhi ya, kama si vyama vya kisiasa vyote.
Usiviachie Vyama vya Kisiasa Kila Kitu
Kuna baadhi ya watu ambao wanaonelea kuwa shughuli zinazohusika na upigaji kura (kama vile habari za kimsingi kwa mpiga kura na uhamasishaji) zinafaa kuwa wajibu wa vyma vya kisiasa pekee. Kwa hakika, huu ndio utaratibu katika demokrasia zilizoimarika. Mamlaka ya kusimamia uchaguzi hawana wajibu wowote katika kuwaandaa watu kwa uchaguzi. Wajibu wao unasalia kwa utoaji wa habari kuhusu wapi, lini, na jinsi ya kupiga kura.
Hata hivyo, kuna baadhi ya sababu nzuri kuhusu ni kwa nini elimu kwa Wapigakura haiwezi kuwachiwa vyama vya kisiasa peke yao na pia ni kwa nini mipango isiyoegemea na isiyopendelea upande wowote ni muhimu. Huenda vyama kuwa na uwezo mdogo. Au, hasa katika jamii zinazopitia mabadiliko, vifaa na uwezo wa vyama vya kisiasa havitakuwa toshelevu. Katika hali kama hii, vyama vilivyo katika uongozi au vile ambavyo vilirithi mabaki ya mfumo wa uongozi wa chama kimoja vinaweza kuwa na viongozi wengi wa mashinani ambao wanaweza kutumiwa kusambaza habari. Huenda kukakosekana vyama vya kisiasa miongoni mwa sehemu kubwa ya watu. Au, hali inaweza kuwa imeharibiwa kiasi kwamba hali ya ushirikiano inayokuwepo katika siasa za uchaguzi hijaeleweka na vyama au na wananchi. Katika hali hii, chanzo cha habari kinachoaminika kinahitajika ambacho kitatoa habari zitakazotumiwa kupimia ukweli wa habari zinazotolewa na vyama. Wakati ambapo kampeni za uchaguzi zinavyoendelea kuwa ghali na changamano mno, wengi wa watu wanaoweza kuwa Wapigakura wanapuuzwa tu na vyama vya kisiasa. Mbali na kuwa watu fulani hawataweza kufikiwa na wagombezi, huenda kukawa na habari ambazo vyama havitaki kuwajulisha watu. Kwa hivyo, mipango isiyo na mapendeleo au miegemeo inafaa kueneza habari hizi.
Kuhakikisha Kuwa Vyama Vinatoa Mafunzo Chanya (mazuri)
Kuchunguza mwenendo wa chama na ukuzaji wa nidhamu bora kupitia kwa sharia, kanuni, tuzo na adhabu huenda lisionekane kuwa jukumu la kielimu. Lakini ni jukumu la kielimu. Linaweza kutekelezwa na wasimamizi wa uchaguzi wenyewe (na bila shaka baadhi ya sehemu zitakuwa wajibu wa wachunguzi wa uchaguzi, mabaraza, na mahakama), au inaweza kutekelezwa na makundi ya wananchi baada ya kupata mafunzo ya kutosha. Au inaweza kufanywa na mawakala wa vyama baada ya kupewa mafunzo ya kutosha. Pia inawezekana kuhusisha katika habari za elimu kwa mpiga kura ambazo zinatolewa kwa umma majukumu ya vyama wakati wa uchaguzi taratibu ambazo zinaweza kutumika kuwataka kuwajibikia matendo yao. Wakiwa na habari kama hizo, hata wananchi wanaweza kusaidia katika kufanya vyama kuwa viaminifu. Na uaminifu huu unasaidia Mpango wa elimu kwa Wapigakura, na mipango yoyote ya elimu kwa raia, kwa kukuza imani ya Wapigakura katika demokrasia na kuzidisha misimamo yao kwa siasa za uchaguzi.