Wasimamizi wa uchaguzi wanafaa kuzingatia njia ambazo afisi zao wenyewe zinaweza kutumika kuendeleza uchaguzi na kuchangia katika elimu kwa Wapigakura na imani ya umma.
Makao makuu ya wasimamizi wa uchaguzi huenda yakaonekana kama ishara ya mchakato wa uchaguzi. Jinsi jengo linavyonekana kutoka nje na mapambo ya ndani yanaweza kuashiria mtazamo zingatifu, usiopendelewa na wa kitaalamu ambao ni muhimu kwa uchaguzi. Sehemu wazi ambazo zinaonekana kutokuwa na mpangilio, zisizodumishwa vizuri, zinazotisha au kubwa kupita kiasi zinaweza kuibua mitazamo hasi kuhusu mamlaka ya kusimamia uchaguzi na mchakato mzima wa uchaguzi.
Ujumbe wa Jengo na Wafanyikazi
Huku mamlaka za kusimamia uchaguzi katika mazingira yanayoendelea au yanayopitia mabadiliko yanaweza kuwa na udhibiti mdogo au yakakosa kuwa na udhibiti juu ya majengo ambayo wamepewa na yanaweza kuwa na vifaa vichache vinavyodhamiriwakufanya mahali hapo kuwa katika hali nzuri ya kufanyiakazi, uwezo wa kufikiwa kwa urahisi na umma na kuwa na wafanyikazi waliotalamika na wenye manufaa yanaweza kusaidia sana katika kutoa ishara chanya.
Pamoja na ujumbe huu ni wazi kabisa, wasimamizi wa uchaguzi wanaweza vilevile kutaka kufikiria njia wazi zaidi ambazo wanaweza kutumia kusaidia katika Mpango wa elimu. Njia wazi kama hizo zinaweza kuhusisha kubandika mabango na bendera nje ya afisi katika mbao za notisi, vituo vya kusambazia vifaa, au vituo vya habari katika maeneo ya umma ndani ya jengo na ratiba za wageni pale ambapo mipango ya elimu inaendelezwa katika eneo hilo.
Mahali pa Elimu
Pale ambapo panawezekana afisi za wasimamizi kuwa na mahali pa kutoa elimu, mipango hii huenda ikawa tofauti tofauti kuanzia kwa warsha ndogo ambazo zinazohitaji tu utangazaji kwa umma, chumba cha kutoleamafunzo na hata maonyesho na mipango ya kuwafikia watu. Mipango kama hiyo hutoa mahali endelevu na pa nyakati zote kwa mipango ya elimu kusaidia uchaguzi. Zile mamlaka za kusimamia uchaguzi ambazo zina uwezo wa kuafikia bajeti kwa mipango hii zina bahati kubwa.
Hata afisi iliyo ndogo zaidi, hata hivyo, inaweza kubandika bango, inaweza kuweka hazina ndogo ya vifaa vya uchaguzi na elimu kwa Wapigakura, au inaweza kuwa na dawati la kutolea habari ambapo umma unaweza kupata vijitabu au vifaa vingine vyenye kutoa habari. Ni muhimu kuwa njia inayochukuliwa kuweka maonyesho kama hayo iwe ya kielimu na wala sio ya kirasimu tu.