Kuhakikisha kuwa watu wanaelewa orodha ya Wapigakura (rejista ya Wapigakura), wamamua kusisajili, wanaweza kujisajili na wanaweza kujisajili kwa njia sahihi kunaleta changamoto kubwa kwa waelemishaji. Usajili wa Wapigakura umukuja kuwa hitaji muhimu kwa shughuli ya upigaji kura.
Pamoja na mabadiliko machache pale ambapo inatazamiwa kuwa usajili wa Wapigakura unaweza kuafikiwa, au pale ambapo uamuzi ulifanywa kimakosa kwa kuhusisha, Wapigakura wanafaa kusajiliwa ili kupiga kura. Uandaaji wa orodha ya Wapigakura na kisha kuikuza katika njia sahihi kuna changamoto kadha kwa Wapigakura, wagombezi, na wasimamizi.
[1]
Kutokana na haya, waelimishaji watazingatia kwa makini kanuni na mifumo ambayo inaundwa kusimamia mchakato wa usajili wa Wapigakura. Katika hali nyingi, usajili unafaa kuandamana na kuhitimu.Katika siku zilizo pita, hii ilitumika mara nyingi kuwanyima haki ya kupiga kura baadhi ya Wapigakura waliohitimu. Lakini katika nchi ambapo uamuzi wa kujisajili ni wa mtu binafsi, na wala sio serikali, hata mipango ya kiusimamizi au kiutawala inaweza kuunda vizingiti ambavyo hatimaye vinaweza kuwa na athari ya kufutilia mbali baadhi ya Wapigakura. Haya yanaweza kuhitaji uhamasishaji wa kiwango cha juu ili kuepuka.
Baadhi ya uhamasishaji huu unaweza kuhimizwa kupitia kwa elimu, mwingine unafaa kupitia kwa maandalizi ya kisiasa, na mwingine utaweza tu kupatikana wakati ambapo mfumo wa uchaguzi na serikali unaonekana kuwa unafaa, pale ambapo uwakilishi unaleta tofauti. Bila ya vishawishi vya kujisajili, na njia za kujisajili, na uwezekano wa kuwa na usajili wa mtu kunakiliwa kwa njia sahihi, mipango ya elimu ambayo inahimiza Wapigakura binafsi kujisajili inaweza kuwa na athari chache. Kwa uhakika, ushawishi wa kisiasa na vilevile elimu kwa wasajili na maafisa wengine wanaohusika inaweza kuwa muhimu tu kama ulivyo Mpango wa wenyewe wa elimu kwa Wapigakura.
Mara tu mifumo ya usajili wa Wapigakura imeamuliwa, waelimishaji wanaweza kuanzisha Mpango. Mpango huo unafaa kujishughulisha na:
- sababu za usajili
- manufaa ya usajili
- namna ambavyo usajili unafanyika
- jinsi ya kuangalia maelezo ya kina kuhusu usajili
- jinsi ya kusahihisha usajili wa mtu iwapo si sahihi
- ratiba ya kujisajili au kusahihisha usajili wa mtu
Watu binafsi pia wanapatikana katika vyama vya kisiasa, na pia kwa makundi ya wananchi, na kwa hivyo watataka uelewa:
- namna ambavyo orodha ya Wapigakura inawalinda dhidi ya unyanyasaji wa kiuchaguzi
- namna ya kuthibitisha orodha
- namna orodha itakavyotumika katika siku ya uchaguzi
- mahali ambapo orodha itabandikwa
- namna ya kusoma na kufasiri orodha
- ratiba ya kuthibitisha orodha au ya kuomba mabadiliko
Katika hali ambapo usajili ni endelevu, elimu kama hiyo itafaa kufanyika kupitia kwa mifumo ya elimu na uongozi iliyopo. Kwa sababu orodha ya Wapigakura haziruhusiwi kufanyiwa mabadliko kwa wakati fulani kabla ya uchaguzi, wananchi watahitaji kukumbushwa kila wakati kuwa wanafaa kujisajili au kuangalia usajili wao. Hii inafaa kuwa sehemu ya elimu kwa Wapigakura yoyote ambayo inawalenga vijana wataokuwa wakijisajili au wakipiga kura kwa mara ya kwanza.
Pale ambapo usajili hufanyika katika vipindi maalum au sajili inaweza kufanyiwa mabadiliko muhimu kabla ya uchaguzi, kunaweza kuwa na maoni ya kuendesha Mpango wa kitaifa wa elimu kwa Wapigakura ili kuhimili mchakato wa usajili. Mpango kama huo unafaa kufikiriwa katika hali zote kama Mpango wa kielimu na hivyo waelimishaji wanafaa kupitia katika kipindi kizima cha Mpango wa elimu. (tazama Muhula wa Mpango)
Kampeni za Kielimu Kabla ya Uchaguzi
Kuna mambo kadha maalum yanayofaa kufikiriwa kwa sababu ya hali ya kipekee ya Mpango wa usajili wa Wapigakura na udharura wa kampeni ya kielimu inayoweza kutokea. Mifano ya kampeni za usajili inaweza kuonekana kwenye mtandao katika Budapest, Hungary-Local Government Election Registration. (Haya ni maandishi ambayo yanaweza kuchukua muda fulani kuyapakua / kuyadondoa kutoka kwa mtandao).
Hasa, waelimishaji watafaa kujaribu kuhakikisha kuwa Wapigakura watarajiwa wanafika katika sehemu za kujisajili kwa wakati ufaao. Pamoja na hayo, Wapigakura watafaa kuelewa umuhimu wa usajili wa Wapigakura. Na hili si jambo la kawaida wakati ambapowatu waonufaika pakubwa kutokana na usajili wa Wapigakura ni viongozi na wala sio Wapigakura wenyewe.
Uhamasishaji, kwa hivyo, unakuwa sehemu muhimu ya Mpango wa elimu. Tofauti na chaguzi ambapo pana ushindani ambao unatarajiwa kuwapa nguvu Wapigakura, usajili ili kupiga kura unaweza kukabiliwa na mwitiko wa kuhuzunisha na kusababisha Wapigakura kukosa kufikia makataa muhimu.
Maelezo:
[1] Maelezo ya kina kuhusu jinsi ya kuunda na kuendeleza sajili ya Wapigakura yanarejelewa katika
Usajili wa Wapigakura.