Elimu kwa demokrasia haihitaji taifa la kidemokrasia. Kwa hakika, baadhi ya hatua bunifu zaidi za kielimu zisizo rasmi zimefanyika katika mataifa ya kimabavu. Kama ilivyoelezwa katika utangulizi, elimu kwa raia mara nyingi huwa ni sifa ya mataifa ya kimabavu ambayo yanalenga kujenga umoja wa kijamii miongoni mwa wananchi wao. Jamii fulani kwa hakika zinaongozwa na imani kuwa mfumo wa serikali ya kimabavu, hata ikiwa ulianzishwa kupitia kwa uongozi wa kitamaduni, kama hatua iliyotokana na mizozo ya kivita au kutokuwepo kwa maendeleo, aukupitia kwa mitizamo jumla, mitizamo jumla na kubalifu ya kidini na kimaoni, njia mwafaka ya kulitawala/kuliongoza taifa. Hapa si mahala pa mjadala huo, lakini eneo la mada halizungumzii muundo huu wa elimu kwa raia, ingawa nyingi ya vipengele vya Mpango vinaweza kutumika katika hali tuli kama hii.
Mataifa dhaifu au yanayofeli na yaliyofeli yana matatizo fulani kwa sababu ya ukosefu wa usalama wa kibinafsi na wakati mwingine kuwepo kwa ugaidi na vita ambavyo vinaleta ugumu katika kushughulikia mipango ya elimu. Hata hivyo, watu wanaoishi katika hali hizi wanastahili kupewa kila usaidizi katika kuhimili hali ya maisha yao na katika ujenzi wa nchi zao. Katika baadhi ya hali juhudi hizi zinafaa kusubiri hadi wakati ambapo kuna hali shwari ya usalama, lakini ikiwa waelimishaji wanatengwa na uundaji wa mipango katika kipindi hiki, taasisi na michakato inaweza kuazishwa ambayo inahujumu jitiada zao za baadaye.
Waelimishaji wa raia ambao wanajishughulisha na ujenzi wa mataifa ya kidemokrasia watapata nafasi ya elimu katika yale mashirika ambayo yamekubaliwa kuwepo au ambayo yanajipa nafasi yenyewe. Mashirika kama hayo yanaweza kuwa na misingi ya kiimani (kidini), miungano ya kujitolea ya misaada, makundi ya kujisaidia na vyama vya ushirika, au makundi ya majadiliano ya kinyumbani. Katika baadhi ya hali, makundi kama haya yanaweza kuwepo nje ya nchi inayohusika.
Mipango ya elimu kama hiyo inatarajiwa kuambatana na hatua za kisiasa, hata yakishurutishwa / kulazimishwa na muktadha, na hii huyafanya kuwa na nguvu zaidi. Mipango ya vijana hasa ni muhimu sana katika hali hizi. Katika baadhi ya hali mipango hii hutoa nafasi salama kwa vijana ambao bila ya mipango hii wangekuwa hofu kwa serikali. Lakini hata pale ambapo vijana wanahusika katika kitendo fulani cha moja kwa moja dhidi ya serikali, au katika mzozo wowote unaohusu raia, elimu inaweza kuweka wazi ubora wa maisha na matendo yao na kuleta uwezekano wa kuwepo kwa matokeo ya kidemokrasia kwa hali hizi za kimzozo.