Katika nchi ya Afganstan bunge za kitamaduni zimeundwa upya na vijana ili kuwahimiza wananchi na kuwatia motisha watu kushiriki katika chaguzi za serikali ya mitaa kama wagombezi.
Nchini Iraq, kazi nyingi ilikuwa ikifanywa na makundi ya wanawake katika kuwatambusha kwa mijadala ya kikatiba na kuwawezesha kutembelea nchi zingine muda mfupi kabla ya katiba yao ya baada ya vita, kura ya maamuzi na uchaguzi.
Katika nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa kiasi kikubwa lengo lilikuwa kwenye uchaguzi, lakini pia kiasi fulani cha elimu ya kikatiba pia ili shughulikiwa.
Katika nchi ya Bosnia, Civitas walihasisi Mpango wa elimu kwa raia ambao ulitekelezwa shuleni kwa kutumia waratibu wa mashinani.
Jamii za baada ya vita ambazo zimekuwa na uwezo wa kuanzisha mipango ya ujenzi-upya wa kimataifa au wa kieneo zinaweza kuanzisha mipango ya elimu mbalimbali.
Mipango hii huwa mara nyingi inaungishwa, kama ilivyo katika nchi ya Angola, kwa mashirika ya mipango ya kuimarisha mashirika ya kijamii – ambapo mashirika ya kinyumbani huanza kuchukua nafasi ambayo imeundwa na makubaliano ya kuleta amani au kukoma kwa vita. Katika baadhi ya nchi mipango hii inaunganishwa na uundaji wa tume mpya wa kusimamia uchaguzi au taasisi zilizoanzishwa na sharia za bunge. Bila shaka ni muhimu kuwa mipango ya elimu kwa raia iwe sehemu ya shughuli zozote za kuruhusu majeshi kwenda kwao baada ya vita, hasa na wala sio wanajeshi watoto pekee.
Mipango hii yote inapigana dhidi ya hali katika nchi baada ya vita – watu walioumia na miundo msingi, taasisi changa, na upiganaji usioepukika ambao bado unaendelea katika maeneo fulani. Hali hizi hazikuwa tofauti baada ya vita vya pili vya dunia, na kuna mafunzo ambayo yanaweza kupatikana kwa kuangalia Ulaya na Ujapani katika siku za mwanzoni baada ya vita hivi – labda kwa hatua za kielimu, mijadala na michakato ya kikatiba au ya kuunda maono ya imani katika jamii ambazo bado zimeathirika na mizozo yao ya hivi punde.
Elimu mara nyingi itaangazia mipango ya amani na mikataba ya amani, katika ujenzi wa uvumilianaji kati ya makundi ambayo yalishiriki vita hapo awali, na katika mipango ya kimpito iliyopendekezwa. Mara nyingi mipango hii ni pamoja na ongezeko la chaguzi na kura za maamuzi – kuhusu ratiba zifaazo ili kulinda mkataba lakini ambao kila siku unatishiwa, hali ambayo inaongeza wasiwasi na ukosefu wa usalama miongoni mwa wananchi.