Hatua ya kimataifa wakati wa dharura (wakati wa hali ya hatari) sasa imeimarishwa. Mafunzo yaliyopatikana wakati wa kutoa msaada kwa wale walioadhiriwa baada ya kimbunga cha tsunami katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2005 sasa yamenakiliwa.
Si jambo la kushangaza kuwa matakwa ya juhudi hizi za utoaji wa misaada, iwe katika ulindaji wa wakimbizi, usambazaji wa vyakula na huduma za matibabu, au ujenzi wa mali na jamii zilizoharibiwa, zimezuia mahitaji mbalimbali ya kielimu ambayo hujitokeza na juhudi za mashirika kutimiza mahitaji haya.
Wakati ambapo jamii zilizopoteza makazi yao zinazimika kuishi kwa muda mrefu zaidi katika jamii za muda na makao mengine ya muda, mahitaji yao ya kielimu na kijamii huongezeka. Mipangilio mipya ya kisiasa (katika kiwango cha jamii na kuhusiana na tawala za mitaa na mashirika yoyote ya kutoa huduma za dharura), mianya katika uongozi wa jamii, kuvumilia michakato ya kijamii iliyo haribika, hasa miongoni mwa vijana na watoto, yote yatahitajika kushughulikiwa na jamii na mambo yanaweza kufanywa mepesi zaidi kupitia kwa mipango ya kielimu.
Katika baadhi ya hali, pale ambapo jamii zilizopoteza makao yao ziko katika hali ya kusahaulika, elimu inaweza kutoa suluhu kwa masuala ambayo huenda yakaleta utegemezi wa muda mrefu.
Waelimishaji ambao wanatarajia kutoa msaada wanafaa kuzingatia masuala kuhusu hali ya kuingia, kuwafikia na kuwa wa wenye manufaa. Mitalaa mwanzoni inaweza kuangazia mabadiliko mepesi kama vile namna ya kupata maelezo ya kimaandishi kuhusu namna ya kushughulikia huzuni na wasiwasi, na kuhusu ujengaji upya wa jamii. Kama jamii zinalazimika kuendelea kukaa kwa muda zaidi katika hali za muda, mahitaji ya kudumu za maendeleo ya kibinafsi, ujuzi wa kiraia na mafunzo au ujuzi wa kikazi au uboreshaji wa ujuzi yote yatahitajika. Kwa sababu ya umuhimu wa ujenzi wa jamii, waelimishaji wana weza kuchagua kutumia mbinu za elimu ya marika na michakato ya kujitawala.
Hata hivyo mipango ya elimu yenye upana wowote inahitaji wakati katika upangaji, afisi, na wafanyikazi – na uwekezaji mkubwa katika mipango hii inaweza kuboresha hali za watu ambao huenda wakarudi katika makao yao awali, au wanaweza kuwa na maoni yao kuhusu njia bora ambazo uwekezaji upya na ujenzi upya unafaa kufanyika.