Kuna uhusiano baina ya elimu ya kijumla na elimu kwa raia, lakini si uhusiano sahili.
Elimu kwa wote kama Mahitaji kwa demokrasia
Mmoja wa wananadharia wakuu wa elimu wa karne ya ishirini, John Dewey, alitoa tasnifu kuhusu elimu yenye mada Demokrasia na Elimu. Kitabu hiki, na vingine kama hiki, kilielezea haja ya elimu kwa wote inayotolewa na serikali ili kuhakikisha kuwa demokrasia inadumishwa. Umuhimu wa elimu ya kijumla utahakikisha kufaulu kwa jaribio la demokrasia, ambalo huenda likashindwa au kupitwa na mifumo mbadala ya serikali za kijamii.
Wakati karne ya ishirini ilipokuwa ikiendelea, ilidhihirika wazi hata hivyo, wakati ambapo elimu kwa wote inaweza kuendeshwa katika misingi ya mifumo inayoruhusu mabadiliko na mifumo inayotambua mawazo au misimamo mbalimbali, na heshima kwa tajriba za kibinafsi za watu na kwa ukuzaji wa maarifa, haihakikishi moja kwa moja kuwa watu wanaweza kushiriki kikamilifu katika demokrasia ambazo zipo kwa sasa. Kwa hakika, kuna kumbukumbu kadha kuhusu mienendo na tabia za raia wa miaka ya nyuma (iliyopita) na kanuni za maisha za wale ambao walitetea na kukuza demokrasia kwa mara ya kwanza na, baada ya muda, wakatetea haki ya watu wote kupiga kura.
Elimu kwa Raia kama Nyongeza / Kijalizo
Kutokana na haya, elimu imekuja kuonekana kuwa shughuli ya kawaida ambayo inafaa kujalizwa na miundo kadha ya mitalaa bunifu au silabasi zaidi inayojulikana kama “elimu kwa raia”. Haya yanaweza kufanyika aidha katika mtalaa wote – kimsingi mjadala unazingatia zaidi taasisi za elimu rasmi katika kiwango cha shule za msingi na za upili – au kwa kuongezea somo kwenye mtalaa. Hatua hii ya mwisho ya kuongezea somo kwenye mtalaa inasababisha kutengwa kwa elimu kwa raia kutoka kwa shughuli zingine za maisha, na katika hali ambapo kuna mitalaa mingi inafaa kushindana na mahitaji mengine. Hata haya hayaangazii lolote kuhusu umuhimu wa ulinganishi ambao unatarajiwa kutika kwa masomo mengine na mahitaji ya elimu ya juu na mitiani ya nje.
Kwa upande mwingine, hatua zinazohusisha mitalaa mbalimbali hukosa kufaulu kwa uchangamano wao, kuhitaji uwezo wa kubadilika kwa urahisi wa mipango ya kielimu ambayo kila mara haupo katika shule na kifaa cha kielimu ambacho mara nyingi hakipo katika kitivo cha chuo kikuu. Kwa hivyo, kwa sababu hatua kama hizo ni wajibu wa wote, si wajibu wa yeyote.
Majaribio Yanaendelea
Kwa hivyo elimu kwa raia shuleni ni shughuli inayoendelea kuundwa. Mielekeo isiyo rasmi ambayo inahusishwa na maisha ya jamii na uratibu wa masuala ya kijamii inaoonekana kuendelea, kama yalivyo yale yanahusishwa na uchaguzi wakati ambapo demokrasia iko hai katika akili za watu. Kwa sababu elimu isiyo rasmi inashughulikia masuala ambayo yamepuuzwa, yamebaguliwa au yaliyo nje ya wajibu wa shule, elimu kwa raia inakuwa mfumo muhimu wa elimu ambao unaleta pamoja ujuzi wa kawaida ambao umetolewa na elimu ya kijumla na kuifanya iweze kufikiwa na watu wazima ambao wanajitahidi kushiriki kikamilifu katika jamii.
Elimu kwa Wote inaweka Msingi wa Ujuzi Unaohitajika
Kwa mantiki hii, inawezekana kuzingatia njia ambazo elimu ya kijumla / kawaida inaweza kuweka msingi wa elimu kwa raia, na jinsi ujuzu wa wananchi unaweza kupata nguvu zake kutoka kwa elimu rasmi pale ambapo inapatikana.