Kuna majaribio kadha ya kuunda mtalaa wa kitaifa au silabasi ya elimu kwa raia. Hii inaendelezwa kupitia kwa falsafa ya elimu ilyopo na istilahi na mifumo mahususi ya elimu – kuweka viwango, matokeo bayana, silabasi yenye msingi kwa yaliyomo na vitabu vya kusoma, na, katika baadhi ya hali finyu zaidi, viwango vya mtihani.
Wale wanao chagua kutaasisha elimu kwa raia kupitia kwa uamuzi wa mtalaa na usimamizi wa elimu wanafaa kutilia maanani masuala yanayohusiana na uanzishaji wa mtalaa. Masuala haya ni kama vile matokeo yanayotarajiwa, mambo ya kufunzwa, walimu, maeneo ambayo yanafaa kutumiwa kufundishia, vifaa vya kusaidi na uhimili wa walimu na wanafunzi, na tathimini.
Wanafaa kuzingatia ikiwa mtalaa huu ni nyongeza katika maeneo yanayofunzwa masomo mengine au itakuwa kivyake, na iwapo itasimama peke yake, itahusiana namna gani na maeneo mengine ya masomo yaliyopo hasa kwa kuzingatia uwezekano wa mwingiliano na urudiaji.
Vizingiti vikuu katika ukuaji wa mtalaa wa kitaifa vinahusiana na mada, ingawa kuna changamoto kadha kuhusiana na haya ambavyo vimeorodheshwa katika sehemu zingine. Changamoto hizi zinapatikana katika utafutaji wakati na mahali, utoaji wa mafunzo na kuwasaidia waelimishaji, na katika utathimini wa wanafunzi.
Elimu Rasmi
Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya upanuzi wa elimu ya kimsingi kwa wote na mchakato wa kuleta demokrasia. Baadhi ya watu wamedai kuwa wajuzi wa hesabu, wenye ujuzi wa kusoma na kuandika na watu walielimika ndio wanachangia kupatikana kwa demokrasia zaidi. Wengine wameangalia kudumu kwa demokrasia na wamesisitiza kuwa hii inaweza kufanyika tu ikiwa wale ambao wamepata haki ya kupiga kura kwa wote pia wapokee elimu wastani ya msingi.
Kihistoria, imechukuliwa kuwa, bila ya kuhusisha baadhi ya masomo ambayo yasiyo ya lazima ambayo yanalenga kuwaingiza wanafunzi katika miundo ya kisiasa naya kijamii iliyopo, shughuli nzima ya elimu katika ufafanuzi ni elimu kwa raia. Katika baadhi ya vitabu vya kimajaribio vilivyoenezwa sana, jamii ndogo ziliundwa ili kuhakikisha kuwa watu wanasoma kutoka darasani na pia katika taasisi inayojitawala yenyewe.
Lakini kwa kawaida wakati shule zinapoendelea kutaasishwa, na wakati ambapo silabasi inaendelea kuwa kubwa na kufanywa kuwa maalum na wakati jamii ilipodhaniwa kuwa changamano zaidi, elimu kwa raia au neno lingine lolote lililotumiwa kurejelea dhana hii ilikuja kuwa somo lililong’ang’ania nafasi katika siku shuleni.
Mengi ya masomo haya yameshushwa hadhi na kudharauliwa, sio tu kwa sababu ya maudhui yake, ingawa kuendelea kuwepo tofauti kati ya maudhui haya na tajriba za maisha ya mwanafunzi kuna athari, lakini huenda kwa sababu masomo kama hayo yanadhaniwa na walimu na vilevile wanafunzi kama yasio na umuhimu sana kama masomo mengine magumu katika mtalaa – lugha, hiasabati, na sayansi, na masomo mengine makuu.
Kinyume na haya, elimu kwa raia imeingizwa katika maisha ya kawaida ya shule kupitia kwa shughuli za nje ya masomo kama vile uchaguzi wa wanafunzi, usimamizi wa kibinafsi wa vilabu nje ya chuo, na mikutano ya mzazi-mwalimu-mwanafunzi. Watalamu wa masomo wamehimizwa kuingiza dhana za elimu kwa raia katika masomo yao, kutambua na kuingiza dhana hizi kupitia historia, lugha, sanaa na huigizaji, sosholojia na uchumi, usimamizi wa biashara na maarifa ya maisha.
Kuna mabishano kadha kuhusu jukumu la shule katika elimu kwa raia. Inaweza kuonekana kuwa ya kisiasa zaidi na hivyo inayoweza kuleta mizozo na miegemeo. Kwa upande mwingine jamii huenda sizikubali shule ambazo zinaendeshwa na serikali kuingilia ukuaji wa kisiasa wa watoto wao, kwa kuogopa kuwa itakuwa propaganda au kuwafunza mambo yaliyo kinyume na maadili na mahitaji ya jamii ile.
Katika mtazamo huu, elimu kwa raia haina uhusiano na mijadala inayoendelea kuhusu jukumu la dini au elimu ya kidini katika shule. Hata hivyo, katika jamii za kidemokrasia pale ambapo wananchi wameanzisha na kugaramia kupita kwa ushuru wao mfumo wa kitaifa wa shule, kuna matarajio kuwa, kama ilivyo tarajiwa mwanzoni wakati ambapo elimu kwa wote ilikuwa ikikuzwa, shule zikuze wananchi waajibikaji na wakuitikia.
Kazi nyingi imefanywa Marekani hivi maajuzi katika ukuzaji wa mtalaa sanifu na katika kujaribu kuifanya ifunzwe – wakati mwingine kama sehemu huru mbadala ya elimu ya kisiasa. Kwa mukhtasari wameangazia vipengele vitatu na sharti moja la kimethodoljia:
- Ufahamu muhimu wa kiraia, ukiwemo ukuzaji wa demokrasia ya kikatiba na kanuni zake.
- Ujuzi muhimu wa kiraia, ukiwemo ujuzi wa kitaalam na wa kushiriki na tamaduni zake, na
- Maadili muhimu ya kiraia, kama vile sifa za uajibikaji na heshima kwa wengine.
Sharti moja kwa hili ni mwalimu wa kidemokrasia, aliyejazwa na bidii na uzingatifu kwa mazingira ya darasa yanayochukuana na nadharia na utamaduni wa demokrasia na uhuru.
Katika Afrika Kusini, Mpango mkubwa wa Elimu na Maadili umeanzishwa na kutaasisishwa katika idara ya kitaifa kuhusu elimu ili kulinda, kuundeleza na kuipanua demokrasia ya kikatiba iliyoanzishwa mwaka wa 1994.
Katika muda wa kugeuza mataifa ya Mashariki ya Ulaya na kuyafanya kuwa huru, demokrasia na, katika hali nyingi, kuingia katika Muungano wa Ulaya, elimu kwa raia kupitia kwa mfumo wa shule uliopo au kupitia kwa michakato sambamba na taasisi ilikuwa mojawapo wa aina za zamani za usaidizi wa kidemokrasia na jamii ya kimataifa.
Elimu isiyo rasmi
Baadhi ya nchi zimeanzisha mtalaa wa kitaifa wa elimu kwa raia ambao unatolewa kitaifa kwa kutumia mbinu za kielimu zisizo rasmi. Kupitia kwa mchakato wa mashauriano au mwelekezo na tume ya kusimamia uchaguzi au taasisi nyingine sawa na hiyo, mengi ya mashirika na taasisi zilizopo yamekubali kutoa mtalaa wa pamoja.
Nchi ya Kenya ni mfano bora wa hizi. Mtalaa wake uliochapishwa ulitayarishwa na kutolewa katika kipindi kilichotangulia uchaguzi wa kitaifa wa mwaka 2002.
Mtalaa huo ulitayarishwa baada ya utafiti wa kitaifa kuhusu mitazamo ya wananchi na mahitaji ya kielimu. Ilitolewa na muungano wa mashirika 70 yasiyo ya kiserikali yaliyoratibiwa na ofisi ndogo iliyosimamia mradi, na kugharamiwa na fedha za maendeleo ya kimataifa kupitia kwa aina fulani ya ugharamiaji wa pamoja. Tathmini za Mpango huu zimewatia moyo wagharamiaji na washiriki wake kupangia mkondo wa pili wa utafiti.
Ucheleweshaji wa kukamilisha kwa mabadiliko ya kikatiba, ambayo uandishi wa kielelezo chake ndio uliokuwa kichocheo cha utafiti wa mkondo wa kwanza, umekuwa na athari kwa hii – na ni mfano mzuri wa jinsi mipango ya elimu ya kijamii inaweza kuwekewa msingi na mahitaji mengine nje ya uwezo wao.
Pia nchi ya Malawi imeendesha mtalaa wa kitaifa ambao uliendeshwa, hasa kwa nchi hiyo ya Malawi kupitia kwa Mpango wenye akronimu NICE - National Initiate for Civic Education. Mpango huu umetegemea waelimishaji wa kijamii na maktaba za kijamii zilizoandaliwa na NICE yenyewe na wala si muungano nchini Kenya.
Katika hali zote mbili, mtalaa umepokea usaidizi wa kitaifa na kisheria ingawa ulianzishwa na juhudi za pamoja za jamii ya wafadhili ya kimataifa na jamii isiyo ya kiserikali. Ni vigumu kujua ikiwa mtalaa tofauti ungeundwa, au ikiwa shughuli hiyo ingeanzishwa, kwa pesa zingetolewa tu kwa mfumo wa kitaifa wa elimu.
Wale ambao wanatengeneza mtalaa kama huo usio rasmi na unaotolewa kitaifa wanakabiliwa na matatizo kadha kuhusiana ukuzaji wa Mpango na umiliki wa Mpango.
Nchini Kenya, matatizo haya yaliepukwa kupitia kwa utafiti wa kimsingi na uuandaji wa vifaa (vya kimaandishi) vilivyonakiliwa na kuchapishwa kirasmi kabla ya kuanzishwa kwa Mpango. Pamoja na hayo, Mpango ulitolewa kama kampeni iliyobanwa kiwakati katika hali ya kisiasa yenye mapendeleo, na wala sio kuundwa kama mtalaa uliosanifiwa ambao utaweza kudumu.
Nchini Uganda mtalaa kama huo ulitengenezwa na baraza la kusimamia uchaguzi katika miaka ya mwanzoni mwa 1990 na ulidhamiriwa kuwa haja yoyote ya kuendeleza elimu kwa umma itafuata mtalaa huu.
Baadhi ya nchi huwaidhinisha mawakala na kuwapa vifaa (vya kimaandhishi). Zingine huidhinisha mawakala na kuwakubalia baadaye kuunda vifaa(vya kimaandhi) vyao wenyewe kwa kufuata tu miongozo fulani.
Katika Ujerumani, uundaji wa vifaa vya kinadharia na vifaa vya kusaidia mtalaa, ingawa si lazima, hutumika kama kirekebishaji kwa kuwahimiza wengine kutumia kile ambacho tayari kipo kuliko kufanya uundaji wao ghali.
Elimu isiyo rasmi katika hali yake ya kawaida hutekelezwa katika mazingira mbalimbali (na hivyo kuibua matatizo ya lugha, kuzoea kwa vifaa na usaidizi wa vifaa vya sauti na picha, uzingatiaji wa wakati na viwango vya kuingia na mapendeleo ya wanaosoma. Elimu hii hutolewa na waelimishaji na wasaidizi mbalimbali, na, licha ya uwezekano wa mafunzo mengi yatolewayo kwa muda mfupi, inatarajiwa kuwa wataukabili Mpango na mitindo na ujuzi wao. Na hatimaye, elimu isiyo rasmi hufanyika mara nyingi ghafla, na hivyo kupunguza uwezekano kuwa vifaa vilivyokwisha andaliwa vitakuwa muhimu.
Gharama za mtalaa uliotolewa kitaifa, uwe wa hali finyu uliojaribiwa katika baadhi ya nchi au wenye hali pana unaotumiwa nchini Kenya, ni za juu, na uharibifu unaweza kufikiriwa. Hatari kuwa vifaa vitapoteza ubora wake na nafasi yake kuchukuliwa na kozi zilizotengenezwa katika nchi kunaongeza uwezekano wa uharibifu.
Baseline Study on Civic Education in Kenya
Thanks,
Joel Mabonga
Nairobi, Kenya