Ushiriki Usioegemea
Elimu kwa Wapigakura inadhamiriwa kutokuwa na miegemeo yoyote. Ili kufanikiwa katika kuwapa uwezo watu na kuwahamasisha Wapigakura, Mipango inafaa kutokuwa na mapendeleo na kutomkuza mgombezi mmoja – awe mgombezi au chama cha kisiasa – dhidi ya kingine. Hii ni hoja muhimu sana ambayo kila mara huwa haipatikani katika jamii za mpito, ambapo utofautishaji mdogo sana hufanywa baina ya elimu kwa Wapigakura na propaganda za kampeni.
Ikiwa elimu kwa Wapigakura ni shughuli isiyopendelea, ni kwa nini basi wagombezi katika uchaguzi wakubaliwe kuchangia katika utengenezaji shabaha na mipaka ya Mpango wa elimu kwa Wapigakura? Kwa uhakika, wagombezi wote na vyama vya kisiasa vinafaa kuwa na nia ya kuhakikisha kuwa Wapigakura wanaelewa uchaguzi unahusu nini katika maana ya kawaida na vilevile ya kisiasa. Kwa kawaida, ni kwa manufaa ya wagombezi kuhakikisha kuwa Wapigakura wanasikiliza pande zote, wafanye uamuzi wao wenyewe, na waende kupiga kura wakiwa na uhuru na usalama. Huku haya yanapoweza kuonekana kutokuwa nia ya muda ya mgombezi mmoja au chama cha kisiasa, Wapigakura ambao wanaelewa masuala na kufanya uteuzi wa busara kwa kutegemea masuala hayo, mwishoni wataamini matokeo, kutambua uhalali wa maafisa na taasisi zilizochaguliwa, na kukubalia washindi kuongoza.
Kwa sababu uchaguzi huwa na ushindani mkubwa, hata hivyo, wagombezi wanaweza kuwa waangalifu zaidi kwa ushawishi unaoweza kuletwa na vyama vya kisiasa vingine au makundi maalum kuhusu shabaha na mipaka ya Mpango wa elimu kwa Wapigakura. Shughuli hii inaweza kuwa kubwa zaidi katika mazingira ya kisiasa yenye migawanyiko mingi zaidi ambapo pana uaminifu mdogo au hakuna uaminifu baina ya vyama vya kisiasa au pale ambapo hakuna upinzani wa kweli. Ikiwa chama cha kisiasa kinaamini wapinzani wake wamepewa ushawishi usiostahili juu ya Mpango wa elimu kwa Wapigakura, kinaweza kujitokeza kupinga au kupunguza uharibifu unaotazamiwa kwa malengo yake kwa kuhujumu Mpango huo, kuzuia Wapigakura kuufikia, kutisha Wapigakura, na kuweka vizuizi vingine kwa matokeo sawa na fanifu.
Katika miktadha mingi ya kimpito, kunaweza pia kuwa na imani kubwa miongoni mwa wagombezi kuwa Wapigakura wasio na habari za kutosha na mchakato wa uchaguzi wenye vurugu utawafaidisha. Katika hali hii, juhudi za kuwa wazi na kufafanua mchakato wa kupiga kura, na vilevile kuufanya kuwa bora zaidi, na kuwaelimisha Wapigakura kuhusu haki zao na jinsi ya kutumia haki hizo vizuri zinaweza kukabiliwa na upinzani mkubwa. Imani kama hizi zinaweza kusababisha aina za vizuizi vilivyonyeshwa hapo juu.
Kwa sababu hii, waelimishaji wa Wapigakura watataka kuweka uhusiano na wagombezi wote na vyama vyao kusaidia katika kuelezea jukumu la Mpango usio na mapendeleo, manufaa yake ya hatimaye kwa wagombezi wote, mipaka ya habari ambazo zinasambazwa, na uhusiano kwa kampeni za vyama.
Zaidi ya Vyama vya Kisiasa
Ni muhimu kuchukulia kwamba mkusanyiko wa wagombezi unatengewa vyama vya kisiasa vilivyosajiliwa kirasmi. Kwanza, vyama vya kisiasa vinashirikiana na makundi mengine yenye malengo maalum, jumuiya ya washauri wabingwa, taasisi, makundi muhimu na mengine ambayo, kwa sababu ya ujuzi wao mahususi, utaalamu, au haja inaweza kuwa muhimu katika majadiliano kuhusu Mpango wa elimu kwa Wapigakura. Kwa kutegemea vipengele vya kisheria, makundi mengine yanaweza kuwa katika nafasi ya kuteua wagombezi. Kunaweza kuwa na uteuzi wa kibinafsi kwa kutegemea mahitaji ya saini za Wapigakura, makundi ya Wapigakura yanaweza kuja pamoja kuteua wagombezi kadha, au mashirika ya umma yanaweza pia kukubaliwa kuteua wagombezi, au muungano wa vyama vya kisiasa na makundi mengine yanaweza kuundwa kushindania uchaguzi mahususi. Kwa sababu makundi haya yanaweza kuwa ya muda au kushiriki kwao katika uchaguzi kunaweza kuwa kwa mara moja moja, inaweza kuwa vigumu sana kuyafikia. Utathmini huenda ukahitajika kuhusu umuhimu wao mbalimbali. Hii itatofautiana kulingana na hali mahususi za uchaguzi.
Changamoto Zinazotokana na Ususiaji wa Uchaguzi
Miungano ya kususia uchaguzi ambayo ni mikubwa italeta changamoto fulani kwa waelimishaji wa Wapigakura na yanafaa kutiliwa maanani. Ikiwa upande fulani mahususi katika uchaguzi utagombea, kama inavyowakilishwa na baadhi ya vyama vya kisiasa, makundi yenye malengo maalum, na mashirika ya kupigania haki za raia, yakaamua kususia – na kuwahimiza wafuasi wao kususia – uchaguzi ambao unaonekana kutokuwa wa halali, basi juhudi za kufahamisha, kuwahimiza, na kuwahamasisha Wapigakura zinakuwa na mwegemeo. Hivi ni kusema kwamba jaribio lolote la kuwataka watu kupiga kura linaweza kutazamwa kuwa usaidizi kwa serikali au chama (au vyama) kilicho madarakani. Hali hii inaweza kuathiri mashirika ya kimataifa na mashirika ya kijamii, kwa kuwa wasimamizi wa uchaguzi wanaweza kushurutishwa na sheria kutoa elimu kwa Wapigakura licha ya hali iliyopo. Hata hivyo, makundi ya mashirika ya kijamii yanaweza kutofautiana kuhusu ikiwa kushiriki au kususia ndiyo njia bora ya kutekeleza mabadiliko ya kijamii, kisheria, au kisiasa. Kama ilivyoelezwa hapo juu, tathmini itafaa kufanywa kuhusu maana na umuhimu wa ususiaji. Kwa wale ambao wanaamua kuendelea na shughuli za utoaji elimu kwa Wapigakura licha ya ususiaji mkubwa, jitihada zinafaa kufanywa kukutana na pande zote na kuelezea Wapigakura waziwazi athari za uamuzi wao wa kupiga au kutopiga kura.