Utambulishaji wa jukumu maalum, au vigezo vya Mpango mahususi unahitaji washika dau wote wa elimu kuelewa na kujifunga kwa kanuni zinazohusika za uchaguzi huru na wa haki. Ili Wapigakura waweze kukubali matokeo na kuwapa kibali washindi, ni lazima waamini kuwa uchaguzi uliendeshwa kwa uhuru na usawa. Ili haya yaweze kutendeka, washika dau wote wanafaa kushiriki katika kuanzisha na kuendeleza fungu la sheria na tamaduni zenye mpangilio na wazi na katika kuanzisha na kuendeleza staha na maadili ya uchaguzi, hata wakati ambapo hazijaandikwa, ambazo zinaunga mkono sheria hizi.
Bila shaka kuna washika dau ambao wanaweza kuwa na malengo fulani katika matokeo ya uchaguzi, isipokuwapale ambapo wamedhihirisha nia ya watu, au Wapigakura. Lakini vyama vingine, makundi mengine ya kisiasa na Wapigakura binafsi watakuwa na malengo fulani katika mashindano wa uongozi. Miongoni mwa watu hawa watapatikana wengi wa waelimishaji wa mashirika ya kijamii na miungano. Hakuna aliye na kinga, na, kwa uhakika, kila mmoja anatarajiwa kupiga kura na kuunda maamuzi ya kisiasa kwa manufaa ya mgombezi anayempenda.
Inaweza kudaiwa kwamba ushindani unasababisha ugumu kwa kila mtu kutenda kwa pamoja kwa manufaa ya mchakato kuliko matokeo. Katika hali kama hizi, labda kizuri zaidi kinachoweza kutarajiwa ni hadhari kwa manufaa ya kibinafsi. Lakini hata matokeo yenye manufaa ya kibinafsi kama hayo katika mienendo ya pamoja, iwapo si uhamasishaji wa pamoja. Kama hii haiwezi kuafikiwa, basi uchaguzi unafaa kuendeshwa na mashirika au makundi ya nje. Na kuna nazoea ambapo chaguzi za kitaifa na za mashirika zimeendeshwa kwa misingi kama hiyo. Mpangilio kama huo na wa kudumu hatimaye, na nchi ambazo zinaendeleza demokrasia zinafaa kujitokeza na mikakati ya kuhamasisha ushirikiano baina ya wananchi na vyama vyao vya kisiasa, na wawakilishi. Ili kuweza kuendesha Mpango wa elimu kwa Wapigakura, mienendo kama hiyo inafaa kupanuliwa hadi kwa uundaji wa misheni ya elimu kwa Wapigakura ambayo inatengwa na propaganda ya chama.
Wapigakura ni Muhimu kwa Manufaa ya Wagombezi
Ni kwa manufaa ya wagombezi kuwa Wapigakura wanafahamishwa vyema na kuandaliwa, wanahamasishwa vizuri na wanafanya maamuzi baada ya kuyawazia. Ni kwa manufaa yao kuwa Wapigakura wengi wanajitokeza na kuwa matokeo ya uchaguzi yanaashria mchakato wenye usawa na haki. Katika mchakato huu, na katika kukubali matokeo, mpiga kura binafsi ni muhimu, na elimu kwa Wapigakura hao wote, Wapigakura, ni sehemu muhimu sana katika kuiafikia.