Muda unaotumika kuelewa Wapigakura ambao wanastahili kushirika katika shughuli ya uchaguzi unasaidia kuhakikisha kuwa Mpango wa elimu kwa Wapigakura unatosheleza mahitaji ya Wapigakura kikamilifu, na hili ndilo hasa lengo la shughuli hii, na wala sio tu kuzingatia maono fulani ya awali ya wale wenye wajibu wa kuelimisha Wapigakura.
Hata kama kuna chaguzi za mara kwa mara, waelimishaji hawawezi kuchukulia kuwa wanajua kila kitu ambacho wanastahili kukijua kuhusu Wapigakura fulani wa uchaguzi mkuu ujao. Kwanza, daima kutakuwa na watu ambao watakuwa wakipiga kura kwa mara ya kwanza. Hawa huenda wakajumuisha vujana ambao wamefikisha tu umri wa kupiga kura. Pia wanaweza kujumuisha watu ambao wamepewa uraia hivi maajuzi na wanahitimu kupiga kura kwa mara ya kwanza. Au pia kundi hili linaweza kuhusisha Wapigakura ambao walikuwa wamedinda kupiga kura kwa kipindi fulani lakini sasa wamepata ari za kupiga kura kutokana na suala fulani, mgombezi, au hamasisho za chama cha kisiasa kwa watu kujitokeza na kupiga kura.
Pamoja na hayo, aidha kundi fulani la Wapigakura au mfumo wa uchaguzi wenyewe unafaa kuchukuliwa kuwa usiosonga mbele. Hata wale ambao hupiga kura kila mara wanaweza kuwa na masuala mapya au wanaweza kuwa wamepata mitindo mipya ya maisha ya kijamii na kiuchumi. Mambo kama hayo yanaweza kuleta tofauti kwa aina ya habari ambazo zinahitajika kuwasilishwa na njia ambayo inatumiwa kuziwakilisha. Pia kunaweza kuwa na mabadiliko kwa mfumo wa uchaguzi, kama vile kutumia teknolojia mpya au mabadiliko katika muundo wa karatasi ya kupigia kura kumudu ongezeko la idadi ya wagombezi au shughuli za umma, ambazo zitahitajika kutiliwa mkazo na kuelezwa kupitia kwa elimu.
Matukio ya hivi maajuzi katika jimbo la Florida, wakati wa uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2000 katika Marekani, unadhihirisha jinsi ambavyo hata katika taifa lililoimarika katika mfumo wa uchaguzi, elimu kwa Wapigakura isiyokamilifu kwa Wapigakura wenye tajriba na Wapigakura wa mara ya kwanza unaweza kuwa na athari kubwa kwa kutegemea ubora wa utawala wa uchaguzi, ufaafu wa kila kura, na uamuzi wa matokeo ya uchaguzi.
Katika jamii za kimpito na mataifa yanayoendelea kutakuwa na sababu mbalimbali maalum za kuendesha Mipango ya elimu kwa Wapigakura. Kutokana na hali ya ujana ya watu, kupanua idadi ya Wapigakura, au hata upya wa uchaguzi katika viwango vyote au kadha, kutakuwa na idadi kubwa ya Wapigakura wa mara ya kwanza. Na mfumo wa kikatiba na kisheria wa uchaguzi na vilevile taratibu za kujisajili kupiga kura na shughuli yenyewe ya kupiga kura, unaweza kuwa tofauti sana kuliko ulivyokuwa awali.
Pamoja na habari mahususi za kimsingi ambazo zitashughulikiwa katika sehemu ya Kutathmini Mahitajiya Wapigakura, waratibu wa shughuli za elimu watataka kupata habari za kuaminika kuhusu watu ambazo ni pamoja na:
- mahali watu wanaishi
- ni watu wangapi wanaishi huko
- kaida za kitamaduni na kidini
- viwango vya watu wanaojua kusoma na kuandika na kwenda shule
- viwango vya watu kushiriki katika chaguzi zilizopita