Kipimo cha Kiafrika, uchunguzi mpana kuhusu hisia za watu kuhusu demokrasia na uongozi katika nchi 15 za Afrika, kinachambua deta yake kutokana na mambo yanayohusu watu – lugha, jiografia, umri, hali za kiuchumi na kijamii miongoni na kadhalika. Jinsia ni moja katika haya japo kila mara huwa na takwimu chache za muhimu katika uchambuzi huu – wanaume na wanawake katika Afrika wana desturi na mitazamo sawa, na wanaenenda au wameelekea kutenda mambo sawa wakikabiliwa na hali fulani. Tofauti kubwa zinapatikana katika jiografia na hivyo basi historia na utamaduni.
Waelimishaji wanaojaribu kuelewa mazingira watakamofanyia kazi hawawatazami wanawake kama kundi tenge la watu. Wanachojaribu kuelewa ni jinsi ya kuwafikia wanawake ikichukuliwa kwamba wamezuiwa kutofika katika sehemu nyingine na mazingatio ya njia bora ya kuwasaidia katika kutekeleza haki zao binafsi na kama kundi na majukumu yao katika njia zinazowaimarisha na kuwaweka salama.