Waelimishaji watataka kupima kwa makini kinachoweza kusomwa kuhusu viwango vya elimu na kusoma vya wapigakura wao kwa kina iwezekanavyo, na watataka kupata taarifa za kitaifa au kieneo zitakazowasaidia katika kujenga mpangilio wao ili waweze kuwafikia wapigakura wasio na uwezo wa kusoma na kuandika.
Uwezo wa Kusoma na Kuandika
Waelimishaji wa wapigakura hawawezi kupuuza viwango vya uwezo wa kusoma na kuandika. Hata jamii zilizostawika kiviwanda au zilizoendelea na mfumo kubalifu wa kusomesha, kwa kawaida pia huwa na asilimia fulani ya watu ambao hana uwezo wa kusoma na kuandika au viwango vyao vya kiusomi viko chini sana. Katika maeneo ya kusini ya ikweta, viwango vya kutoweza kusoma na kuandika ambavyo mara nyingi ripoti zake si linganifu, hutofautiana kutoka kwa asilimia 10 hadi zaidi ya asilimia 70 ya watu. Takwimu hizi hufunika ukweli kwamba sehemu Fulani ya jamii hiyo inaweza kuwa na viwango tofauti vya uwezo wa kusoma na kuandika.
Katika nchi ya Peru “asilimia sabini na moja ya wanawake hawana uwezo wa kielemu – takribani mara tisa zaidi ya wanaume."
[1]
Mwelekeo huu unajirudia katika nchi nyingi zinazostawi. Ubaguzi wa aina hii dhidi ya wanawake hutoa mfano wa wazi wa mielekeo ya viwango wa kukosekana kwa elimu ambavyo waelimishaji watataka kugundua. Katikati ya mipaka ya nchi, kutakuwa na sehemu ambako viwango vya elimu vitakuwa chini ya vile vya maeneo mengine, kwa mfano katika sehemu za mashambani. Katika sehemu hizi, kutakuwa pia na tofauti ambapo baadhi ya makundi ya watu kama vile wanawake au wazee, wana viwango vya juu zaidi vya kutoweza kusoma na kuandika.
Kujenga mipangilio ya kielimu itakayoafiki wale wenye uwezo wa kusoma na kuandika bila shaka kutawatenga wale wasio na uwezo huo. Kujenga mipangilio inayojumuisha wasio na uwezo wa kusoma na kuandika haipaswi kuwatenga walio na uwezo huo. Kisha, ujenzi wa mipangilio inayosisitiza ushirikiano na usomaji wa ana kwa ana, utasaidia kuhakikisha kwamba walio na uwezo na wasio na uwezo wa kusoma na kuandika wote wanapata nasafi ya kujifunza.
Nchi zilizo na viwango vya juu vya uwezo wa kusoma na kuandika huwa na faida fulani. Zinaweza kutegemea maneno yaliyochapishwa haraka sana. Hata hivyo, hata katika nchi hizi, walionyimwa haki kitamaduni – mara nyingi vijana, wanawake, maskini – huenda wakakosa viwango vya juu vya uwezo wa kusoma na kuandika. Waelimishaji watahitajika kufahamu ari waliyo nayo watu ya kusoma na ari waliyo nayo ya kuelewa.
Kusoma
Kando na viwango vya uwezo wa kusoma na kuandika, waelimishaji wanaweza kuhitajika kueleza viwango vya kiusomi. Hapa bila shaka pana mwingiliano. Watu wengi hujifunza jinsi ya kusoma kutoka shuleni. Wale wasiojifunza jinsi ya kusoma mara nyingi hawakuweza kuenda au kukaa shuleni kwa muda mrefu.
Viwango au miaka ya kusoma inaweza pia kuwafafanulia waelimishaji mambo mengine kuhusu viwango vya uwezo wa kusoma na kuandika. Kusoma huathiri jinsi watu watakavyoielewa mifumo mingine ya elimu. Hutokeza, ama kwa uzuri au ubaya, thamani waliyo nayo watu kwa masomo na mbinu wanazoweza kwa kiwango kikubwa wa kuhusisha na mipangilio ya kielimu.
Kwa wakati huo, elimu kwa wapigakura inaweza kutekelezwa kivyake, kuondolewa darasani na hivyo basi kupata uhuru dhidi ya mifumo fulani ya masomo, ujenzi na utoaji wa elimu, na ushindani wa kupata taarifa pamoja na kufaulu kunakohusishwa na mfumo rasmi wa elimu.
Waelimishaji wa wapigakura hufanya kazi vizuri katika jamii zinazothamini elimu, hasa mafunzo ya kudumu. Hunufaika katika tamaduni ambamo kusoma kumechochea maamuzi ya kidemokrasia na uhuru wa kibinafsi. Wanaweza pia kuanzia kwenye mifumo ya masomo ambamo mipango ya elimu kwa wapigakura au raia imeingizwa katika mtaala rasmi au usorasmi.
Uelewa wa mielekeo iliyojengwa na mifumo ya shule katika nchi husika, hivyo basi, itatoa mwangaza katika hamasisho na ujuzi wa jumla ya wapigakura. Wasiwasi ya hivi majuzi kuhusu elimu kwa raia katika kiwango cha shule, hata katika demokrasia zilizokomaa, inapendekeza kwamba mafunzo katika mazingira ya kitamaduni na hata bunifu au ya kisasa, huenda yakakosa kuwatayarisha raia vilivyo kwa demokrasia kukikosekana mitaala iliyotungwa maalumu kwa shughuli hiyo. Kwa hivyo waelimishaji wa watu wazima huenda wakakosa kupuuza jamii yenye usomi na iliyoelimika inaelewa uchangamano wa demokrasia za kisasa, hata kama wanaweza kuchukulia kwamba wataweza kusoma vijitabu vitakavyoeleza jinsi ya kujisajili, ni wakati na mahali pa kupigia kura. Bila shaka, huenda wakakosa kuchukulia kwamba kusoma huimarisha uchangamfu na ujuzi wa kushiriki kwa raia (kwa maelezo zaidi kuhusu hili tazama Uhusiano kati ya Elimu ya Kawaida na Elimu kwa Raia)
Tanbihi:
[1] M. Kidron & R. Segal, The State of the World Atlas (Middlesex: Penguin, 1995).