Dhana ya “mtaji wa kijamii” inatoa maelezo ya kimuhtasari kuhusu raslimali za watu ambazo zinaweza kuwepo kwa mpango wa elimu kwa wapigakura. Kwa bahati mbaya, ni kauli ambayo imeibukia kuwa uvumi tu katika harakati za kisiasa kwa hivyo inahitaji majadiliano zaidi. Ikieleweka, inaweza kutumiwa kutoa habari zaidi kuhusu nchi.
Sehemu hii inaangazia vipengele vinavyojenga mtaji wa kijamii na jinsi mtaji huo wa kjiamii unavyoweza kutumika katika mipango ya elimu kwa wapigakura ili kuimarisha shughuli za kidemokrasia katika nchi na jumuia husika. Itaangazia pia japo kwa ufupi upungufu wa mtaji wa kijamii kama chombo cha kuifikia jumuia ili kupata viwango vya juu vya kidemokrasia.
Uingiaji wake katika siasa za wakati huu unakuja wakati ambapo vipengele vyote vya uwepo wetu mara nyingi vinapimwa katika misingi ya uwezo wa kiuchumi. Je, tunazalisha chochote kama wafanyakazi? Je, serikali inafanya kazi? Je, tunafanya ya kutosha katika shughuli zetu za kijamii?
Demokrasia za ulimwenguni kote zimekuwa zikijitathmini katika miaka ya 1990. Licha ya matumaini yaliyokuwepo katika miongo ya mwanzao mwanzo, sasa hivi kuna ukwepaji wa aina fulani kuhusu urefu wa demokrasia zinazochipuka.
Suala kuu katika siasa za siku hizi linazunguka jinsi tunavyoweza kuimarisha na kuunganisha demokrasia. Je, kufaulu kwa demokrasia katika eneo fulani, kunaweza kuhamishiwa kwa eneo jingine la dunia ambako haukufaulu au kuwepo kwa miongo mingi?
Mojawapo wa hoja zinazoibuliwa katika shughuli hii ni wajibu wa mashirika ya kutetea raia katika demokrasia ya nchi. Alivyosisitiza Robert Putman katika maandishi yake mengi na hasa katika Kuwezesha Demokrasia kufanya Kazi: Kaida za Kimsingi katika Italia ya Kisasa, viwango vya mahusiano kati ya mashirika kuhudumia raia na serikali ndivyo huonyesha viwango vya demokrasia katika nchi hiyo.
[1]
Hili linamaanisha kwamba kadiri viwango vya juu kabisa vya mahusiano vinavyoshuhudiwa ndivyo, demokrasia ya nchi hiyo itakavyoonekana kuwa juu na kinyume chake. Kaida za kitamaduni zilichunguza miaka ishirini ya maisha ya kisiasa na miungano katika Italia, na kulinganisha matokeo yake na sehemu za kaskazini hadi kusini. Putnam alihitimisha kuwa maeneo ya kusini yalikuwa na viwango vya chini sana vya kidemokrasia kushinda yale ya kaskazini kwa sababu ya uwepo mahusiano ya msimamizi – msimamiwa na mafia. Kaskazini kuliunga mkono mashirika na makundi mengi ya kutetetea raia.
Maelezo ya Mtaji wa Kijamii
Suala la mtaji wa kijamii lilianzishwa na James Coleman na kuendelezwa na Pierre Bourdieu. Coleman aliitumia kauli hiyo kufafanua raslimali za watu ambazo huibuka kutoka kwa mahusiano yao ya kijamii, na Bourdieu aliitumia kurejelea faida na nafasi zinazotokana na watu kuwa wanachama katika jumuia fulani.
[2]
Kijelezi cha mtaji wa kijamii ni rahisi sana. Ni sarafu inayoiwezesha jamii kuendesha shughuli zake ipasavyo. Hili ni pamoja na vipengele vya wazi kama kaida, mila, hisia, imani, mitandao na vingine kama hivyo. Putnam anasema mtaji wa kijamii unajumuisha vipengele vinavyopatikana katika jumuia fulani, ambavyo hurahisisha usimamizi na ushirikiano ili kupata faida za kuridhisha. [3] Hili linamaanisha kwamba ikiwa mtu anafanya kazi katika jumuia iliyo uaminifu, maadili, mitandao na vingine kama hivyo, matokeo yake yatakuwa bora zaidi ya katika jumuia isiyotumia vigezo hivyo. Hili lina athari kubwa kwa mahusiano ya mashirika yasiyo ya kiserikali na jumuia kwa mujibu wa elimu kwa wapigakura.
Francis Fukuyuma, mwandishi wa The End of History and The Last Man, Trust, the Social Virtues and the Creation of Prosperity, na idadi nyingi sana ya makala anaamini kwamba “uthabiti wa [mtaji wa kijamii] ni muhimu katika utendakazi wa masoko na demokrasia.” [4] Hili linamaanisha kwamba serikali na jumuia nyingine zinapaswa kuhakikisha kwamba kuna viwango vya juu vya uaminifu, mila, na desturi vinatunzwa na kukuzwa katika jamii hiyo ili kazi yao iwe rahisi na yenye ufanisi.
Elimu kwa wapigakura huratibiwa ili kusambaza ujumbe kuhusu upigaji kura na chaguzi kwa makundi ya wapigakura stahifu kabla ya siku ya uchaguzi. Ni zoezi ghali. Kwa sababu hii, njia ambazo zingepunguza gharama hutumiwa na wale walio katika shughuli hiyo mipango ya elumu kwa wapigakura. Ikiwa mtaji wa kijamii unarahisisha ushirikiano basi vipengele vile kurahisisha elimu kwa wapigakura na bora kabisa katika shughuli yake.
Mila na Desturi
Mila na desturi katika jumuia hurejelea hisia miongoni mwa raia zinazofanya mahusiano kati yao kuwa rahisi. Ikiwa wananchi wote katika jumuia fulani, kwa mfano, wanaamini kwamba kila mtu anapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa kama mshirika, jumuia hiyo itahusisha kila mtu katika mijadala kuhusu masuala yanayoathiri raia wote. Hisia hizi zitadhihirika katika mila za jamii hiyo. Watu huheshimu mali, mitazamo na haki za kila mmoja wao. Tunaweza pia kusema kwamba raia hawa watajua na kuelewa kwamba wanapswa kulipa ushuru, kulipia huduma wanazopewa, na kushirikishwa katika mijadala ya kidemokrasia.
Shirika linapotekeleza mipango ya elimu kwa wapigakura katika jamii hiyo, kazi yao itakuwa rahisi sana kwa sababu ya mila na desturi zilizopo. Waelimishaji hawatalazimika kuingia katika ukina wa shughuli kuhusu kuruhusu tofauti zikijiri, kuweka mazingira huru ya mijadala na kuwaalika watu kushiriki katika jukumu la raia kwa kupiga kura. Jumuia hiyo tayari idesturi na mila.
Mtaji wa kijamii wa jumuia hii unaweza kutumiwa kurahisisha usambazaji wa habari kuhusu upigaji kura. Waelimishaji wanapaswa kutumia mila na desturi zilizopo katika jumuia hiyo ili kurahisisha kusoma. Mila na desturi hizo zinapaswa kuangaziwa kwa mifano ya majukumu ya raia katika mchakato wa upigaji kura.
Mila pia ni mienendo inayofanana katika jumuia au mashirika. Watu wanaweza kuwatabia fulani ambazo zinatambuliwa kitamaduni. Katika jumuia za Kiafrika, kwa mfano, Chifu ndiye mtu mwenye mamlaka makubwa sana. Ikiwa chifu hakuhusishwa, jumui hiyo inaweza kukosa kuzingatia mpango huo ama kimwili au kisaikolojia. Wafanyakazi wa mpango huo wanaweza kuzuiwa dhidi ya kuingia katika eneo hilo, raia wanaweza kuhisi kwamba wafanyakazi hao wa mpango wa elimu kwa wapigakura hawaheshimu tamaduni na desturi zao na hivyo basi watasusia kusikiliza taarifa inayotolewa. Ni muhimu kwa waelimishaji kujua kuhusu desturi za jumuia, kuheshimu desturi hizo na kuzizingatia wanapofanya kazi katika eneo hilo.
Maeneo mengine pia yanaweza kuwa na viongozi wasio rasmi. Watu hao wanapaswa kuhusishwa ili waweze kurahisisha utendakazi katika jumuia hiyo. Wakati mwingine viongozi wa kidini ndio wenye hadhi hiyo, sawa na walivyo walimu au watoa huduma za afya. Ni uhimu kwa waelimishaji kujua watu hao na kuheshimu mila na desturi zilizo katika kila jumuia.
Mitandao
Kipengele cha pili katika mtaji wa kijamii ni mfumo wa mitandao. Kila jamii ina mitandao. Hii inaweza kuwa ya kikazi, kanisa, mchezo, na klabu ama kundi lolote linalopatikana katika jamii hiyo. Mitandao inaweza kutumiwa ili kufanya mipango ya elimu kwa wapigakura kuwa nafuu na ya kufikia watu wengi kwa mchango mdogo tu wa waelimishaji. Mitandao huhusisha idadi kubwa ya watu wenye utambulisho, lengo au nia moja. Mtandao huo pia huwaruhusu watu kusambaza ujuzi wao katika sekta fulani na kuusambaza ujuzi huo.
Mitandao inaweza kuenea na kuifikia idadi kubwa ya watu kutoka kwa sekta mbalimbali za jumuia hiyo na wale nia mbalimbali. Waelimishaji wa wapigakura wanaweza kutumia miatandao hiyo kusambaza habari zao. Nafasi moja ya kuingia katika jamii fulani ndiyo tu inayohitajika. Klabu ya soka inaweza kuwa na mkutano mara moja kwa wiki. Waeklimishaji wa wapigakura wanaweza kukutana na kundi hilo la watu mara moja. Taarifa kutoka kwenye mkutano huo kisha zinaweza kuenezwa kwa wanachama hao kupitia kwa mitandao yao. Mwanachama mmoja anaweza kuwa katika kundi jingine la kusoma ilhali mwingine anaweza kuwa katika kundi jingine la wahudumu wa kujitolea. Taarifa hii itasambazwa katika jumuia hiyo kupitia kwa mitandao kama hiyo.
Waelimishaji wa wapigakura wanapaswa kutumia mitandao hii kimikakati na kusambaza habari za kutosha (zilizochapishwa au kwa njia usimulizi) katika nafasi itakayokuwa na athari kubwa kwenye jumuia hiyo. Karatasi za uujmbe huo zinapaswa kutolewa mwanzoni katika viwango vya kutosha ili watu waende nazo nyumbani. Habari hiyo inapaswa kuwekwa pia kwenye kumbi kama vile maeneo ya masoko, makanisa, shule, na shemu za kufanyia mazoezi ili kupiga jeki usambazaji wa kisimulizi. Katika jumuia za mashambani ambako usimulizi wa hadithi uganlipo na viwango vya kutojua kusoma na kuandika viko juu, mitandao inaweza kutumiwa vilivyo. Waelimishaji wa wapigakura wanaoweza kukaa katika eneo kwa muda mrefu hivyo basi wanapaswa kuwaarifu watu hao walio na mawasiliano makubwa na watu wengi katika jumuia hizo kama vile walimu, viongozi wa kidini, wafanyakazi kwenye matibabu, na hata wamiliki wa maduka.
Uaminifu
Uaminifu ni kipengele kikuu katika kufaulu kwa demokrasia. Francis Fukuyama anaamini kwamba watu wasioaminiana wataishia kushiriki tu chini ya mfumo wa kanuni na masharti rasmi ambayo yamejadiliwa, kukubalika, kuendewa mahakamani na kutekelezwa wakati mwingine kwa njia za lazima. [5] Uaminifu unaweza kupatikana tu kwa njia mienendo ya muda mrefu. Watu huaminiana tu ikiwa wamekuwa na uhusiano kwa kipindi cha muda mrefu. Uaminifu unahitajika kujengwa kutokana na tajriba na marudio ya kufanya shughuli pamoja. Ukimwambia mtu siri na mtu huyo anaiweka kwa mfano, uaminifu mkubwa utajengeka kati yenu. Na wakati ujao, kiwango kikubwa cha uaminifu kinaweza kuwekwa katika mtu huyo.
Mtiririko wa habari utakuwa bora zaidi katika jamii zilizo na kiwango cha juu cha uaminifu. Watu watamwamini msemaji au mwelimishaji kutowaelekeza vibaya na hivyo basi, wataamini kwa kiwango kikubwa taarifa hiyo. Uaminifu ni kitu cha lazima katika mitandao na hivyo basi, vipengele vyote vinakuzana. Katika mtandao ni nia ya kundi hilo kuweka viwango vya juu vya uaminifu. Waelimishaji wa wapigakura wanaweza kuweka viwango hivyo vya juu imani katika shughuli yao. Waelimishaji wanapaswa kuwasiliana na kufanya kazi na watu wa jumuia hiyo ambao huenda wakaaminika sana na watu wengi wa jumuia hiyo. Jumuia nayo huwaamini watu hawa na itawasikiliza bila shida au kutoamini.
Waelimishaji wa wapigakura wanapaswa kutumia mtaji wa kijamii unaopatikana katika jamii hizo. Unaweza kuwasaidia kwa shughuli muhimu ya kuwaarifu watu kuhusu chaguzi.
Ijapokuwa mtaji wa kijamii una mazuri mengi, kuna mambo hasi yanayoweza kuzuka.
Matatizo
Mila na desturi huchukulia kwamba watu wanazijua na hivyo kuzifuata. Ikiwa mtu mgeni anakuja katika jumuia fulani hata hivyo, atapaswa kufunzwa mila na desturi hizi na kukubaliwa katika jumuia hiyo kabla ya kuidhinishwa kukaa nao. Hili linamaanisha kwamba kwa wakati wowote ule lazima kunaweza kuwa na watu katika jumuia hiyo wanaoweza kutengwa au kukosa kufahamu mila zilizokubaliwa. Wakati mwingine mila hizo si za kawaida na hivyo waelimishaji wanaweza kuzipuuza bila kujua ama kupuuza tu hivyo basi kuikasirisha jumui hiyo. Huku desturi za kitamaduni zikiwa maalumu, zinaweza pia kuwa changamano sana.
Mitandao pia inaweza kumaanisha kutengwa. Ikiwa mtu ni mmoja katika kundi la mtandao fulani, inamaanisha kwamba kuna watu wengine nje ya kundi hilo wasio kwenye mtando huo. Miundo hii huelekea kusaidia tu watu walio kwenye mtandao huo. Kukosa kuwa mwanachama hivyo basi, hutatiza sekta nyingine za jumuia hiyo. Jumuia zilishikamana ni ngumu sana kupenya bila shaka kuliko zile ambazo ziko huru kupata shinikizo kutoka nje. Waelimishaji wanapaswa kupima jumuia kwa uangalifu ili kujifunza ni mitandao ipi jenzi na mwafaka. Hiyo inaweza kuwa ile iliyo na watu wengi wanaowasiliana nao.
Uaminifu pia unaweza kuwa mgumu kutambua kwa watu kutoka nje kama vile mwelimishaji kutoka shirika moja kama vile la kisheria ambalo haliwakilishwi katika jumuia hiyo. Katika hali hii, mipango ya mafunzo inapaswa kujengewa wafundishaji katika jumuia hiyo. Wafundishaji hao asilia wanapaswa kuwa wanaokubaliwa na kuaminika na jumuia hiyo na hivyo basi kurahisisha uenezwaji wa taarifa kwa kundi hilo la watu.
Mtaji wa kijamii ni suala lililo na uwezo mkubwa wa kuwawezesha waelimishaji kufikiria njia mwafaka za kuwasiliana. Wale wanaohusika katika elimu kwa raia watataka pia kuzingatia njia ambazo wanaweza kutumia kwa ukamilifu manufaa ya mtaji wa kijamii.
Kutathmini Mitandao ya Kijamii
Kila nchi ina mtaji wa kijamii sawa tu na ilivyo na raslimali nyingine. Lengo la kufanya tathmini au uchunguzi kuhusu mitandao ya kijamii ni kutokeza visivyonekana kuonekana. Hili huruhusu wale wanaoshughulikia upangaji na utekelezaji wa mipango ya elimu kwa wapigakura ili kuweza kufikia uhusiano wa kitamaduni unaoweza kuimarisha demokrasia na kupanga vizuri njia za kuweza kukabiliana na nguvu ambazo huenda zikatatiza shughuli hiyo.
Huku kukiwa na njia kadhaa za kutekelza tathmini hiyo, rahisi kabisa inaweza kuwa kuweka timu moja au zaidi katika uwanja huo ili kufanya mahojiano na kujaza taarifa katika kiziodeta chepesi au mfumo wa kadi zenye nambari. Timu hizi zitaanza kwa kuteua idadi ya mashirika yanayopatana katika eneo la kijiografia na kuomba taarifa kutoka kwao. Kundi la pili la mahojiano litafanywa na watu au mashirika yanayorejelewa katika kundi la kwanza la watu.
Kundi zima la watu wa kuwasiliana nao linapokusanywa – jumuishi kwa kiwango cha kuridhisha na katika wakati na fedha zilizotengwa na wapangaji wa shughuli hiyo kielimu – timu kutoka nyanjani itasaidia kujenga deta ya uwakilishwaji wa mitandao ya kijamii katika vikao vya kutoa taarifa. Hili hufanyika kwa kutumia karatasi pana, kuandika orodha ya watu wa kuwasiliana nao na kisha kutumia muunganishi kuweka majina hayo kwenye mtandao au ramani. Hili linaweza kuhusisha Makala sahili kama vile “Inayorejelewa na[mtu fulani]” au “inayomrejelea [mtu fulani]” au “linafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na [mtu fulani]”, au yoyote iwezekanayo. Mtandao kama huo unaweza kusaidia waelimishaji katika kuelewa “mfumo huo wa kijamii” wa eneo hilo la kijiografia.
Habari hii kuhusu watu wa kuwasiliana nao hivyo basi itapigwa jeki na deta ya uchunguzi kuhusu desturi na mila za kisiasa na kijamii. Waliofanya tathmini hiyo wanaweza kuwa hivyo basi kutaka kutayarisha ripoti ya kisimulizi kwa wale waliotwikwa jukumu la kupanga mpango wa elimu kwa wapigakura, ambao unajumuisha habari muhimu zikiwemo sitiari, hadithi za kweli, picha za wale waliohojiwa na maelezo yanayotoa nafasi nzuri. Ripoti kama hizo hutoa mtazamo wa kina ambamo mpango unaingizwa na unaweza kusaidia hata kwa wale wanaoishi katika sehemu husika.
Sehemu za Kuchunguza
Tathmini ya mitandao ya kijamii inaweza kuanzia popote, almuradi maswali mazuri yanaulizwa kuhusu wale waliohojiwa. Kuna watu na mshirika mengine ambayo huenda yakawa na uhusiano na mitandao hiyo ya kijamii. Miongoni mwa haya kutakuwa na miungano ya kidini au kitamaduni, vilabu na makundi yaliyo na wanachama wengi, na mashirika ya wakazi, wafanyakazi, wafanyabiashara na wataalamu wengine. Itakuwa muhimu kuhakikisha kwamba timu ya kwenda nyanjaini inapenya katika mashirika hayo ya kawaida na hata yale ambayo huenda wakazi wa maeneo wakapuuza.
Mashirika unganifu ni yale ambayo pamoja na kazi yake au ili kutekeleza kazi yao wenyewe, na kuunganisha mtandao mmoja ua zaidi kwa kushirikisha, huduma za kihazili, na kinyumbani kwa mitandao hii. Mashirika kama haya yanaweza kutajwa mara kwa mara na wahojiwa. Mashirka unganifu hayapaswi hata hivyo, kuchukuliwa kama wasemaji wa jumuia au kubadilisha mitandao wanayounga mikono.
Maswali ya Kuuliza
Timu za kwenda nyanjani zitataka kupata taarifa ya kimsingi kuhusu watu wa kuwasiliana nao kutoka kwa kila mmoja wanayemhoji. Taarifa hii inapaswa kujumuisha:
- utamkaji mwafaka wa majina, vifupisho na kanuni zote za kawaida za kutoa majina ya shirika ambalo mtu huyo anawakilisha. Katika jamii nyingi, mashirika hutajwa kwa majina mbalimbali, na hivyo wafanyakazi wa nyanjani wanaweza kuishia kuamini kuwa mashirika tofauti tofauti ndiyo yanayojadiliwa.
- taarifa yote kuhusu watu wa kuwasiliana na ikijumuisha anwani mwafaka posta pamoja na nambari za simu na nambari za faksi na anwani za barua pepe ikiwezekana. Katika kisa cha mashirika yasiyo rasmi, taarifa ya ziada inaweza kuhitajika kama vile jina la mahali ambako ujumbe wa simu unaweza kuachwa au anwani ya posta ambako herufi ya pili inahitajika ili kumwomba aliyepokea ujumbe huo kuuwasilisha kwa kwenye herufi ya mwanzo na kadhalika.
- maelezo ya kina (kwa kiwango kinachokubalika) kuhusu watu na makundi maalumu ambao anayehojiwa hufanya nao kazi au kuhusiana nao kila mara. Taarifa hiyo inapaswa kujumuisha majina ya mashirika ambamo mtu huyo na shirika ambamo mtu huyo ni mwanachama.
Uziada
Kuna uwezekano kwamba tathmini ya mitandao ya kijamii itafanyika wakati mmoja na shughuli nyingine za mpango huo. Shughuli hizi nyingine zinweza kujumuisha utafiti kuhusu kundi lengwa, mitalaa ya mwanzoni, na harakati za usajili. Kwa sababu ya umuhimu wa kuelewa mfumo huo wa kijamii mapema kuhusu hatua za mpangilio hata hivyo, linaweza kuwa wazo la busara kuchukulia hili kama hatua ya mapema kwenye shughuli zaidi za tathmini ya mpango huo.
Maelezo:
[1] Robert D. Putnam, Making Democracy Work: Civic Traditions in Modern Italy (Princeton: Princeton University Press, 1993).
[2] A. Portes and Landolt, "Downside of Social Capital" in The American Prospect, no. 26 (May/June 1996), 18 -21.
[3] Robert D. Putnam, "The Prosperous Community: Social Capital and Public Life" in The American Prospect, no. 13 (Spring 1993).
[4] Francis Fukuyama, The End of History and the Last Man (New York: Free Press, 1992) or Francis Fukuyama, Trust: The Social Virtues and the Creation of Prosperity (New York: Free Press, 1995).
[5] Francis Fukuyama, Trust: The Social Virtues and the Creation of Prosperity (New York: Free Press, 1995).