Huku halmashauri ya kitaifa ya kusimamia uchaguzi ikiwa na uwezo wa kisheria kushughulikia elimu kwa wapigakura, pia zinawakilisha moja katika raslimali za kwaiada zilizopo kwa shughuli zisizo rasmi za elimu kwa wapigakura. Kunaweza pia kuwa na nafasi ya kufanya shughuli za pamoja za elimu kwa wapigakura kupitia kwa ujenzi wa ushirikiano maalumu kati ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi na mashirika ya kushughulikia raia, miongoni mwa mengine. Wajibu wa maofisa wa kusimamia uchaguzi umeelezwa kwa mapana katika Maafisa wa Uchaguzi katika Elimu kwa Wapigakura. Kando na maafisa wa halmashauri ya kusimamia uchaguzi waliopewa jukumu la kusimamia jukumu hili hata hivyo, kunaweza kuwa na mashirika mengine ya kiserikali ambayo mara nyingi hupuuzwa kwa mfano kwa wizara za habari na elimu, mashirika yanayoshughulika na usajili wa wapigakura, kamati za utendaji na kisheria zinazoshughulika na elimu kwa raia, au huduma za msaada wa serikali nikitaja baadhi tu.
Matawi mengine ya serikali yanapaswa kuzingatiwa pia kama raslimali za ziada. Yanaweza kutoa waelimishaji na wawasilianaji wenye ujuzi, makundi makubwa ya wahudumu wa kujitolea au angalau wafanyakazi wasiopendekezwa, na pengine uwezo wa kupata taarifa na tajriba inayoweza kuwa muhimu wakati wa upangaji na utekelezaji wa mpango wa elimu kwa wapigakura.
Vitabu vya serikali vya majina ya anwani vinaweza kutoa habari muhimu za kiasili za kutumika kwa tathmini, japo kupatika kwa uwezo wa kuwafikia wafanyakazi na raslimali za idara za serikali huhitaji kujuana kibinafsi na usaidizi kutoka mawaziri wa umma au wa serikali, na muhimu kabisa, kutoka kwa maofisa wakuu wa serikali au wafanyakazi wa serikali.
Wapangaji wa uchaguzi watataka kufanya kazi na halmashauri za kusimamia uchaguzi katika kuhakikisha kwamba idara za serikali na wafanyakazi wake wakuu wanapashwa taarifa na kuhisi kuchangia katika mpango wa huo kuanzia mwanzoni. Hili huwa muhimu hasa ikiwa, kwa sababu fulani, wafanyakazi wa serikali walioshughulikia uchaguzi hapo awali, elimu kwa wapigakura, au mipango pana ya elimu kwa raia, wamekosa kujumuishwa katika mpango uliopo au kusambazwa kwa idara nyingine katikati ya uchaguzi mmoja na mwingine.
Inaweza kuwa kwamba kuna hofu kidogo kuhusu kutumiwa kwa wafanyakazi wqa serikali katika hali za mabadiliko ya kiuongozi hata katika mazingira ambamo shirika hilo la huduma kwa raia limekuwa likipendelea upande mmoja wa uongozi. Ikiwa hii ndiyo hali, uangalifu mkubwa unapaswa kuchukuliwa katika kutathmini ushauri uliotolewa na wafanyakazi walioajiriwa. Hata hivyo, tajriba ya serikali haipatikani kwa wepesi na katika visa vingi haiandikwi katika mfumo unaoweza kutumiwa na watu wasio na uzoefu.
Ilivyo katika tathmini zote za mipango, ni lazima kutakuwa usawazishaji wa faida za raslimali hizo katika kwa mujibu wa malengo ya mpango huo, vilevile pamoja na athari ambayo matumizi ya raslimali hiyo kwenye gharama, ufaafu na uhalali machoni pa raia.