Kuna ongezeko la idadi ya maajenti wa kimataifa na washirika wa kibinafsi ambao wako tayari, na radhi na wana uwezo wa kutoa usaidizi wa kusimamia uchaguzi na hasa elimu kwa raia na Wapigakura. Kupata usaidizi wa kimataifa kunahitaji ujuzi wa rasilimali hizi pamoja na majukumu mahususi ambapo kwamba usaidizi wa kimataifa unahitajika.
Mashirika ya Kiserikali ya Kimataifa
Usaidizi wa kiuchaguzi umekuwa shughuli kuu ya Umoja wa Mataifa ambao umeandaa vitengo vingi vya wataalamu wenye uwezo wa kuitikia shughuli mbalimbali –kutoka uchunguzi wa uchaguzi na usimamizi hadi elimu ya uchaguzi wa raia. Kwa kuchapishwa kwa matokeo ya warsha ya Mipango ya maendeleo ya umoja wa kimataifa kuhusu kiwango cha maendeleo ya binadamu, “Ripoti kuhusu Maendeleo ya Bianadamu:Kuimarisha Demokrasia katika Ulimwengi Uliosambaratika”, umoja wa kimataifa ulitambua mtindo wa kuendelea kwa wanachama wake wa kuunga mkono demokrasia na shughuli ya utawala kwa usambamba au kama misingi ya maendeleo. Kwa kuanzishwa kwa fedha za waungaji mkono wa demokrasia katika mwaka wa 2006, kumetokea makubaliano baina ya mataifa kuhusiana kwa pamoja katika kuendeleza demokrasia.
Ari hizi zimezinduliwa na au kuanzishwa na hamasisho za mashirika ya kimataifa. Umoja wa Afrika na shirika la mataifa ya kiafrika zilianzisha mikakati ambayo kwayo nchi zinapaswa kuwa na uwajibikaji wa kustawisha demokrasia.
Mipangilio hii imehimiza ushirikiano baina ya uungwaji mikono wa uchaguzi na elimu ya raia ya uchaguzi.
Upataji usaidizi
Licha ya ongezeko la mikakati ya asasi za kilimwengu za kuungana, mashirika ya kimataifa ya kiserikali bado wanaendesha shughuli zao katika maeneo mbalimbali pamoja na Makala mbalambali. Habari zaidi kuhusu mashirika ya kimataifa ya kiserikali zinaweza kupatikana kwenye ofisi zoa nchini na za kitaifa au kwenye wavuti wao.
Mashirika mengine kama vile Muungano wa Ulaya, Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya, Shirika la Mataifa ya Marekani, Muungano wa Afrika na Mashirika ya Kimataifa kama vile Muungano wa Jumuiya ya Madola na Umoja Mataifa, mashirika hayo yote yanatoa usaidizi wa uchaguzi kwa viwango tofauti tofauti kwa wanachama wao pamoja na kutoa usaidizi huo wakati mwingine kwa mataifa wafadhili na wale wenye kuomba usaidizi. Umoja wa Kimataifa unatoa mwongozo katika wavuti hltp:portal/undp/org/server/nis/4649027220113235. Baadhi ya mataifa ya kibinafsi pia hutoa usaidizi kupitia maajenti wa kiserikali, kwa mfano, Shirika la Ajenti wa Marekani wa Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Idara ya Ulaya ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), Ajenti ya Maendeleo ya Kimataifa ya Kanada, (CIDA), na Ajenti ya Mashirikiano ya Kimataifa wa Japani, (JICA), pamoja na ubalozi wao ughaibuni. Wakati mwingine mataifa binafsi wanaweza kuomba mashirika ya kimataifa ya kiserikali kuwawakilisha kimatendo. Kijumla, usaidizi kutoka kwa serikali sharti utafutwe na serikali au mtu anayewakilisha jumuiya jumla pamoja na matamanio yao katika nchi.
Mashirika ya Kimataifa ya Kiserikali
Mbali na serikali, kuna baadhi ya mashirika ya kibinafsi yanayotoa usaidizi wa kuendeleza demokrasia. Usaidizi huu unajumlisha wafadhili wa usimamizi na miradi ya gharama ya uchaguzi (ACE). Nyingi ya hizi ni pamoja na kutoa ufadhili mdogo, kutunza wavuti wa kutoa habari kuhusu mashirika ya wafadhili, usaidizi wa kitaalumu (uliopangwa na maeneo yenye kusaidia kama vile elimu ya uchaguzi) pamoja na rasilimali ya habari ya kimaeneo.
Tofauti na maajenti wa ufadhili wa kiserikali, mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali wanaweza kuchagua kufadhili miradi ambayo inatekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kama wao, hivyo kusaidia maendeleo ya sekta ya kibinafsi kwa sababu hiyo, itakuwa muhimu kwa wanaotafuta ufadhili kuelewa mienendo, malengo na vipao mbele vya shirika la kutoa ufadhili.
Kujiandaa kupata Usaidizi
Rasilimali zinaweza kupatikana tu iwapo shirika limebainisha kimahususi aina ya ufadhili unaohitajika na unaowiana na malengo ya kihalisia na vipao mbele vya shirika lenye kutoa ufadhili. Usaidizi unaweza ukawa usaidizi wa kitaalamu, kwa mfano ushauri kuhusu maendeleo, utekelezaji au kutathmini Mipango ya elimu ya uchaguzi kupitia mafunzo kwa wakufunzi, kupitia usaidizi huo, au vifaa hitajika, kwa njia ya ufadhili au kwa kugharamia shughuli fulani fulani kama vile kuchapisha na kunakili nyaraka. Baadhi ya mapendekezo yakisha andaliwa, mmoja wapo wa washiriki wa miradi ya gharama ya uchaguzi ambao watakuwa radhi kupendekeza watu kwa maeneo ya usaidizi.