Ni muhimu wakati wa tathmini ya mazingira kuhakikisha kwamba wale waliopewa jukumu la kupangia mpango wa elimu kwa wapigakura, wana ufahamu wa kina kuhusu changamoto za kifedha na wakati. Hivi huwa si vya kawaida au kujitokeza kwa ukamilifu kila mara. Kunaweza kuwa pia na mabadiliko muhimu kwenye mazingira ambamo mpango wa elimu kwa wapigakura unafanywa au kwa hadhira ambayo inaelekezewa. Mabadiliko haya yanaweza kuathiri wakati na pesa zitakazohitajika kwa shughuli ya kisasa ikilinganishwa na bajeti iliyowekwa awali. Kwa hivyo, waelimishaji watataka kuchunguza undani wa hayo mapema iwezekanavyo. Waelimishaji wa muda watakushauri kuwa hakuna wakati wa kutosha na pesa huwa chache kila mara za kutekeleza shughuli hiyo.
Kuokoa Wakati na Pesa
Mipango ya elimu itahitajika kuzingatia njia za kupunguza gharama na kuokoa wakati. Mara nyingi, hili hufanywa kwa kuongeza idadi ya wasaidizi wa kujotolea na idadi ya mashirika yanayochangia kwenye shughuli hii. Ilivyodokezwa kwingine, suala la kujenga ushirikiano kati ya halmashauri za kusimamia uchaguzi, mashirika ya kutetea raia na sekta ya kibinafsi husaidia kupunguza gharama huku usaidizi wa kifedha unaweza kutafutwa kutoka kwa mashirika ya kimataifa. Shughuli hizi pia zinaweza kurahisishwa katika mikakati ya kupanga na kutekeleza. Hili linaweza pia kufanywa kwa kuzidisha raslimali na idadi ya wafanyakazi. Tukio moja la mafunzo au mwongozo wa mafunzo unaweza kujaza hitaji moja au kufikia zaidi ya hadhira moja.
Kupunguza gharama ili kuafiki mahitaji
Kwa bahati mbaya, shughuli zinazohusiana na uchaguzi haziwezi kucheleweshwa au kupewa makataa mapya kwa sababu ya hisia za mwelimishaji kwamba wakati uliopo hautoshi. Badala yake, malengo ya mpango huo yanapaswa kuwa kunyooshwa na matokeo yake kuelezwa kwa mteja, iwe mdhamini, halmashauri ya kusimamia uchaguzi, idara ya serikali au kundi la wasomaji. Matarajio yao pia yatapaswa kutunzwa katika muhula mzima wa mradi huo. Hizibila shaka ni moja katika sehemu ngumu sana kwa watu wasio waelimishaji kushika–kwa kusoma kunategemea wakati. Utengenezaji wa nyenzo, utoaji, na usambazaji pamoja na kutanguliza mafunzo hayo kwa waelimishaji, na wakati wa elimu hasa hugharimu muda mwingi na mara nyingi huwa shughuli ngumu kutekeleza katika wakati uliotengwa. Wale wanaotekeleza mipango hii yenye mizunguko mingi bila shaka watarahisishiwa kukamilisha kwa wakati mzuri kuliko wale wale wanaojitayarisha kuanzia chini kabisa au mwanzoni mwa kampeni za uchaguzi au wakati wa kufanyika kwa uchaguzi.