Sehemu hii inaweka njia ambazo habari muhimu ya kuvumbua mahitaji ya elimu zinaweza kukusanywa. Njia hizi ni kama:
- Kuelewa kundi la walengwa
- Kutekeleza ukaguzi
- Kutafuta habari ambazo tayari zipo
- Kuelimika kutoka kwa washiriki na waamuzi
Wananchi na Wapigakura wana mahitaji mengi ambayo katika uchaguzi hujitokeza kama maudhui, maswala, dhana, mahusiko ama matatizo na ambayo wagombeaji katika uchaguzi watayajibu kupitia kampeni zao.
Kwa upande mwingine, waelimishaji wana shauku kwa mahitaji ambayo yana uwezo wa kutimizwa kupitia masomo na mikakati mingineyo ya kielimu.
Huenda kuna mahitaji mengine ambayo yanaweza kutimizwa kwa mabadiliko ya kimamlaka au katika mazingira ya uchaguzi. Mfano mzuri ni hitaji la mpiga kura katika kituo cha kupiga kura. Waelimishaji wanaweza kufafanua mipangilio inayoandaliwa, lakini mipangilio yenyewe yatimiza mahitaji.
Katika mfano huo wakufunzi kutoka mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yanaweza kuchagua mipango inayokwenda zaidi ya ufafanuzi wa Mipango hadi hatua ambayo inaweza kuchukuliwa na Wapigakura kuhakikisha usalama wao. Hata hivyo, kubainisha seti ya mahitaji tu hakutapunguza chaguo la makini na mitazamo ambayo waelimishaji sharti wachukuwe katika kubainisha malengo au matokeo ya mipangilio mwafaka.
Hata hivyo, ni muhimu kupiga hatua kutoka maelezo sahihi ya usuli wa mpiga kura au uelewa wa maswala ya kisiasa ya sasa, hadi kutambua na kuelewa wa orodha nzima ya mahitaji yanayopaswa kutimizwa kwa moja au zaidi ya Mipango ya elimu ya Wapigakura. Hili linaweza kutekelezwa kwa kuunda makundi lengwa au maeneo ya wale wanaojifunza. Na, wakati ambapo welimishajii watataka kuandaa mipango ambayo ni jumlishi, kutakuwepo na hali ambapo maeneo ambayo kwayo Mipango imeandaliwa yanahitaji njia na habari mahususi. Elementi nyingi zilizofafanuliwa katika mada hii zina ufaafu wa kijumla, lakini kwa baadhi ya makundi kuna mazingatio mengine.
Sehemu nyingine tofauti ya idadi hiyo (tazama Malengo ya Kielimu) inaangalia tena ni kwa jinsi gani orodha kama hiyo ya mahitaji inaweza kugeuzwa ili iwe seti ifaayo ya malengo ya kielimu.