Ubainifu wa hadhira inayofaa zaidi kwa elimu haupo wote mikononi mwa waelimishaji wa elimu ya uchaguzi. Siasa, katiba na sheria huzuia au huongoza mipango hiyo.
Wajibu wa Siasa
Elimu ya uchaguzi huwawezesha Wapigakura. Huwahimiza kujisajili na iwapo wamejisajili tayari, wapige kura. Huwapa mwongozo wa kutia alama ifaavyo kwenye karatasi ya upigaji kura ili kuhakikisha kura hazikuharibika wakati wa kuhesabu kura. Huwahimiza kuamua wanayetaka kumpigia kura, na inawapa mbinu za kupima chaguo lao. Hizi ni shughuli zenye athari za kisiasa. Si ajabu kuona kuna ushawishi wa kisiasa ama kupanua uwezo wa waelimishaji wa elimu ya uchaguzi au hata kupunguza uwezo huo kupitia njia rasmi na njia zisizo rasmi.
Katika hali ambapo uchaguzi umeanza kufanywa kila mara na pale kuna makubaliano ya kijumla ya kijamii kuhusu manufaa ya uchaguzi na uwezo wa kubadilika kwa serikali, wakuu wa uchaguzi wanaweza kuandaa mipango ya elimu iliyo na kina na jumlishi.
Katika hali kama hizi, itakuwa muhimu kushughulikia maingiliano katika elimu ya uchaguzi kutaka kuhujumu Wapigakura na mizozo iliyolenga waelimishaji na washiriki na jaribio la kuzuia Wapigakura kufikia haki zao za uchaguzi, kuwapuuza wakufunzi na mipango yao na maamuzi kuhusu bajeti, sheria, saa ya kupiga kura na maswala mengine yaliyo mikononi mwa serikali.
Katiba hutoa maamuzi na haki
Wakati kuna katiba, na hasa katika jamii zinazoendeshwa chini ya kifungu cha haki za kibinadamu, kuna uwezekano wa kuwa na maswali kuhusu usawa. Katika jamii nyingine kuna uwezekano wa mipango ya elimu kulenga makundi maalum. Lakini mashirika mengine yataweza kukumbana na mahitaji kwamba Wapigakura wote wanapaswa kushughulikiwa kwa usawa. Hili linaweza kuwa motisha kwa Wapigakura. Lakini pia linaweza kuwazuia kutoa habari msingi zaidi kwa msingi wa ubia.
Chochote zaidi ya mipango ya elimu msingi kitahitaji kutofautisha. Hili litahitaji uangalifu ili kuepukana na mawazo yatakayohujumu mipango hii katika hali ambapo hakuna katiba. Hili linaweza kutokana na jamii ambazo zinaendeshwa kwa seti ya nyaraka za kihistoria na tamaduni nyingine kama Uingereza. Au, inaweza ikawa nchi iko katika harakati za kubadilisha katiba yake au katiba ya zamani imejuhumiwa na vita. Katika hali hizi wakufunzi wa elimu ya uchaguzi, wanaweza kuwa na ubora wa kupata mamlaka mengine kulenga makundi katika elimu kama makundi ambayo walibaguliwa hapo awali au makundi pingamizi, au kabila lenye watu wachache na mengineyo. Kwa vyovyote vile waelimishaji hawatataka kupuuza ukweli kwamba huduma bia ni njia bora na muhimu katika elimu ya uchaguzi.
Sheria Huweka Majukumu na Mipaka
Wakuu wa uchaguzi hupatia majukumu mahususi au katika hali nyingine kwa ari tekelezi. Uwezo huu unaweza kujumlisha majukumu ya kutoa habari au elimu kwa Wapigakura. Wakuu wa uchaguzi katika nchi nyingine kama vile Russia, Ukraine, Australia, Kanada, Mexico na Paraguay wana majukumu ya kuendesha elimu kwa Wapigakura na au elimu kwa raia.
Katika nchi nyingine, hasa zile zinazoendela au zipo katika mabadiliko wakuu wa uchaguzi huenda hawana majukumu kuendesha elimu kwa Wapigakura. Ingawa hitaji la elimu ya uchaguzi rasmi linaweza kuwa wazi, wakuu wa uchaguzi, hasa wale walio katika mazingira ya siasa kali, wanaweza kusita kutekeleza majukumu yao ya kihalali, au wanaweza kuwa waangalifu sana katika maswali hayo. Katika hali ambapo sheria inawafunga waelimishaji wa elimu ya uchaguzi, inaweza kuwa bora kwao kutumia uhusiano wao na waelimishaji katika sekta ya mashirika ya kiraia au kupanua mipango yao au kuhakikisha kwamba majukumu ya elimu ya uchaguzi yanatimizwa na watu waliohitimu. Hata hivyo, ni sheria itakayoamua kama upanuzi huu au kazi mbadala itapata ufadhili rasmi.