Maadili yanayoshikiliwa pamoja na tajriba na msingi wao utakuwa na athari kwa sehemu ambapo elimu hii itapatikana, nani anayepata elimu hii na mahusiko ya elimu yenyewe. Katika hali ambapo kuna rasilimali tosha hili huenda si tatizo, lakini katika nchi zenye rasilimali duni, ungalifu utabidi uwepo ili kuhakikisha baadhi ya Wapigakura hawakubaguliwa.
Waelimishaji ambao wameajiriwa na mamlaka ya uchaguzi hawatakuwa na uwezo wa kuwapuuza makundi fulani ya wale wanaoelimishwa kwa kuwapenda au kwa kuwachukulia kama watu wasiofaa. Lakini hata wao hawajakingwa kutokanana mapendeleo ya kibinafsi. Waelimishaji wasio wa kiserikali hufanya uamuzi kila mara kuhusu makundi ya kufanya kazi na yale ya kutenga. Katika hali nyingi maamuzi haya hutolewa kutegemea maadili tekelezi yaliyo wazi na yanayoweza kutabiirwa. Lakini haiwi hivyo kila wakati. Wakati mwingine mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kijamii wanaweza kuwa vipofu kwa mapendeleo yao wenyewe.
Kutoka na maadili haya na mapendeleo, huenda ikatokea kuwa makundi fulani lengwa na maeneo watapata kushughulikiwa na wengine wakakosa. Wakati kuna uwazi katika mipango wakufunzi huweza “kuziba mianya”. Au wanaweza kubaini seti mahususi ya Wapigakura kwa msingi wa maadili yanayoshikiliwa na mamlaka ya uchaguzi au kusimamia taratibu ya uchaguzi kwa ujumla na kunhitajika kwamba makundi yasiyo ya kiserikali “wazibe mianya” ya makundi lengwa ya watu wenye mahitaji maalum. Swala kuu hapa ni kuweka wazi maadili na mapeneleo ambayo kwayo maamuzi hutolewa.
Aidha kwa chaguo kuhusu makundi fulani, maadili ya mwelimishaji yanaweza kuathiri uchaguzi wa mahitaji ya elimu. Mara nyingi mamlaka ya uchaguzi huweza kuchaguliwa kwa msingi wao wa kisheria au hata kuungwa mkono na idara ya mahakama. Wanaweza kuwa na tajriba kuhusu umangimeza wa serikali pamoja na uelewa wa sheria husiika taratibu na kanuni. Wakati huo huo huenda hawafahamu mahusiko ya usimamizi wa wafanyikazi wa uchaguzi [pamoja na kutoa habari ifaayo kwa Wapigakura wa kawaida.
Wakati kuna idadi kubwa ya mikakati ya elimu na rasilimali pungufu, haitakuwa bora kuwa na wasiwasi sana kuhusu maswali haya. Mipangilio inaweza kutumia mivuto inayowasilishwa na waelimishaji wa elimu kwa Wapigakura kuhakikisha elimu imewafikia watu wote. Lakini haitakuwa hivyo siku zote, hasa katika nchi zinazoendelea na zile zilizo katika harakati za mabadiliko, hivyo uangalifu unahitajika ili kuepuka matatizo ya kimfumo (kama mianya inayotarajiwa kuangusha mipango) kwa sababu waelimishaji kuamua kutoa elimu hiyo katika lugha fulani, au kwa makundi fulani lengwa au kwa kijiji fulani au hata kwa stesheni fulani ya redio au gazeti.
Uangalifu pia lazima uwepo kuhakikisha kwamba chaguo hazitoi rasilimali tu kwa kundi fulani na kutenga kundi lingie kwa sababu wanajua kupiga kura au huwa hawapigi kura au hata mbaya zaidi “kwa sababu watawapigia kura badala ya kutupigia sisi”.