Ili kutayarisha mipango ifaayo, waelimishaji wa Wapigakura lazima wafahamu khusu Wapigakura au Wapigakura watarajiwa. Wanahitaji kufahamu wanachofahamu watu (au wanafikiri watu wanajua). Wanahitaji kujua hisia za watu kuhusu uchaguzi na upigaji kura. Na mwisho wanahitaji kujua himizo yao au pingamizi yao ya kupiga kura.
Habari hii inaweza kupatikana vipi? Mtu anaweza kuangalia kwenye mpira angavu. Mtu anaweza kukisia. Inaweza kunufaisha kutazama tajriba za awali. Kuzungumza na wahusika katika uwanja huo ni muhimu. Je, kuwauliza Wapigakura wenyewe? Lakini haiwezekani kuzungumzia kila mtu. Hivyo mtu atahakikishaje kwamba habari kutoka baadhi tu ya watu inathamani yoyote? Habari hizi zitakuwa zitawakilisha maoni ya Wapigakura watarajiwa?
Kutumia uchunguzi
Ukaguzi ni muhimu kwa kusoma maono, maadili, motisha na hali na tabia za watu. Ukaguzi pia ni muhimu wakati ambapo matokeo yanafaa kuwa jumlishi kwa watu wengi.
Makundi yaliyochaguliwa
Kwa idadi ndogo ya watu kwa mfano wachache tu, ni bora kutekeleza utafiti wa kina kutumia makundi ya watu waliochaguliwa yanayowapa watu muda mrefu wa kuzungumza kwa kina kuhusu hisia zao. Kisha mtu anaweza kukagua miswada ya mjadala wa watu ili kujua mawazo yao. Makundi yaliyochaguliwa hutoa habari kubwa kuhusu mada fulani. Utajiri wa miswada kama hiyo huwa mgumu kujua, lakini kwa idadi ndogo jambo hilo huwezeshwa kwa urahisi.
Ni muhimu kugundua hata hivyo kwamba, makundi yaliyochaguliwa siyo tu mikutano na mazungumzo yasiyopangwa. Makundi yaliyochaguliwa hutumia methodoloji mahususi kwa mujibu wa uchaguzi wa watu wa kuwa kwenye kundi. Makundi yawe fanani iwezekanavyo, na makundi yapangwe vizuri kuakisi tofauti kuu za mitazamo ya Wapigakura watarajiwa. Kundi moja linaweza kujumlisha wanaume wadogo ambao ni mara yao ya kwanza kupiga kura, kwa mfano, na kundi lingine lijumlishe wanawake wadogo ambao pia ni mara yao ya kwanza kupiga kura. Habari itatokana na mpangilio mzuri wa mazungumzo katika kila kundi, pamoja na tofauti za makundi haya. Habari zinazopatikana kutoka kwa makundi yaliyochaguliwa ni muhimu katika kubainisha maswala ya kuzingatia katika ukaguzi unaojumlisha watu wengi au kuchunguza maswali yaliyovumbuliwa na uchaguzi huo kwa kina zaidi.
Kuandaa Chunguzi
Mjadala huu unalenga kuzisaidia aina mbili za watu. Kwanza, watu wengi wanaweza kutaka kufanya uchunguzi kibinafsi na hivyo wanaweza kuupata huu kuwa mwongozo muhimu, au msingi muhimu kwa hatua zote muhimu watakazolazimika kufanyia kazi. Hata hivyo, hautatoa habari elekezi za kutosha kupitia kila hatua kwa kina zaidi.
Maelezo mengine yamejumuishwa katika sehemu hizi ili yeyote atakayekuwa na nia ya kupata yaliyomo katika mada hii awe na mwongozo kamilifu kwa kile ambacho huenda ndicho sehemu ghali sana ya mpango wa kitaifa wa elimu kwa wapigakura. Wasomaji wengine wanaweza kupuuza habari muhimu zifuatazo:
Sehemu mbalimbali zinazohusishwa na uchunguzi mara nyingi huwa zaidi ya raslimali au uwezo wa shirika au mtu yeyote binafsi. Kwa hivyo, mashirika mengi yanaweza kutaka kuliajiri shirika la kitaalamu kuhusu utafiti lililo na uzoefu mkubwa wa kufanya uchunguzi ili kuyafanyia kazi hii. Hakuna wakati wowote hata hivyo ambapo udhibiti wa mchakato huu unapaswa kuachwa. Ufafanuzi huu unalenga kuziwezeshea halmashauri za kusimamia uchaguzi kudumisha udhibiti muhimu katika kuangalia mradi huo.
Ili kupata uchunguzi bora kunahusisha mnfululizo wa hatua:
- Kuratibu uchunguzi
- Uundaji wa Maswali
- Maandalizi ya kufanya Uchunguzi
- Ukaguzi
- Kuteua Washiriki
- Kuingia Nyanjani