Kuamua Aina ya Habari Inayohitajika
Kwanza, uamuzi utahitajika kufanywa kuhusu aina ya habari inayopaswa kukusanywa na ni kwa sababu gani. Mchakato huu unaweza kuanzishwa kwa kuuliza maswali kadhaa: “Ni mitazamo gani au tabia gani unazohitaji kujua kuzihusu?” Katika istilahi changamano za sayansi ya kijamii hili huitwa kigezo tegemezi. “Unafikiria ni nini visababishi vyake?” Hivi ni vigezo huru. Majibu yatatoa misingi fulani muhimu kwa yaliyomo katika uchunguzi huo.
Chukulia kwamba mtu alitaka kujua kuhusu sababu za wapigakura kujitokeza, au kigezo tegemezi. Uamuzi hufanywa kupima athari mbalimbali za vipengele ambavyo huenda ndivyo vilivyosababisha kama vile:
- habari
- kichocheo/mwamko
- ufaafu
- mitazamo kuhusu kiwango cha ushindani katika uchaguzi miongoni mwa vyama katika uchaguzi fulani
Hivi vitakuwa vigezo huru. Kimsingi, hivyo basi vipengele vitano muhimu vimetambuliwa ambavyo ni muhimu na huhitaji kupimwa. Kila kinachosalia ni kueleza kila moja wapo wa dhana hizi, au vipengele hivi ili kuwe na mwafaka kuhusu kinachomaanishwa katika kauli kama vile “ushindani katika uchaguzi” au “mwamko.”
“Mfumo wa Kimawazo”, unaopaswa kuwa kama msingi wa mradi mzima hivyo basi, hujengwa. Wakati wowote katika mradi huo, mtu anapaswa kuwa na uwezo wa kupima ikiwa kile kinachofanywa kinasaidia kupima kilichotambuliwa katika mfumo huu. Ikiwa hakifanyi hivyo, mtu anaweza kugundua kuwa amepotoka (ambacho ni rahisi sana kufanya), na kwamba anashughulikia kitu ambacho ni kando kabisa na kile alichonuia.
Kwa wakati uo huo, huku akiandika maswali ya uchunguzi, inaweza kutokea kuwa wazi kwamba kuna vitu fulani muhimu ambavyo mtu hana budi kuvijua, na ambavyo kwamba havikujumuishwa katika msingi huo. Wakati huo, mtu anapaswa asiandike maswali jingine mpya katika mtindo wa dharura, bali arejelee na kuliweka wazo hilo jipya kitika msingi huo.
Ujenzi wa mawazo hutokana na:
- ufahamu wako wa mazingira ya eneo hilo;
- kurejelea kile kinachojulikana na ambacho kimewahi kuchapishwa kuhusu mada hiyo, k.m. kujitokeza kwa wapigakura;
- Kushirikiana na wataalamu wengine katika uwanja huo.
Kabla ya Huduma ya Maoni ya Umma (POS) ya Idasa kufanya uchunguzi kwenye Majengo ya Cape kuhusu mitazamo ya umma kuhusiana na makosa ya jinai, usimamizi na hatua ya kijumla, kwa mfano, ilialika wanakriminolojia, wanasosholojia, wahudumia jamii, na wanahabari waliokuwa na tajriba pana kuhusiana na hali hiyo pamoja na maandishi ya kutosha ya kiakademia kuhusiana na suala hilo. Hili lilisaidia katika kutambua sehemu muhimu za mawazo, na hivyo basi, vigezo vya kuweka katika hojaji.
Uendeshaji
Katika kiwango hiki, lengo ni kuanza kutengeneza hojaji yenye muundo mzuri kwa kupanga maswali maalumu ya kupima hali halisi ya “ulimwengu halisi” au mitazamo katika mfumo huo wa mawazo. Yaani, mfumo wa mawazo hubadilishwa katika hojaji yenyewe.
Kimsingi, maswali mengi yanapaswa kutengenezwa ili kupima kila wazo muhimu. Suala moja linaweza kuwa kuhusu ishara ya kutoegemeka kwa mitazamo ya watu katika eneo hilo. Lengo moja kuu ni kuweza kusawazisha majibu ya maswali yote kuhusu wazo fulani ili kutoa kipimo thabiti na cha kutegemewa au orodha ya mawazo (kama vile “nia”). Mfululizo wa maswali haupaswi kupima tu kitu hicho kimoja, bali inase sehemu au vipengele mbalimbali vya “nia ya kisiasa”.
Swali faafu, mfululizo wa maswali ni ule unaopima maana halisi ya ufaafu. Sura moja ya ufaafu inaitwa “Ufaafu wa Taswira”. Yaani, kwa kusoma maneno kwenye swali halisi, maneno yaliyomo kwenye swali yanaelekea kuafikia lengo la swali hilo. Sura nyingine inaitwa “Ufaafu Jengwa”. Hivi ni pale ambapo swali, au mfululizo wa maswali, yanaelekea kuhusiana ndaniu kwa ndani, au pengine na maswali mengine yanayopima mambo ambayo huenda mtu angetarajia kuyahusisha na nia za kisiasa.
“Kutegemeka” kunamaanisha kiwango kwamba yataweza kupata majibu yanayofanana kutoka kwenye kundi moja hadi jingine, wakati wowote ule. Aina mbalimbali za majaribio ya kitakwimu zipo ili kusaidia kupma viwango vya ufaafu jengwa na utegemewa.
“Uendeshaji” ndio hasa unaogharimu muda mwingi katika mchakato mzima wa uchunguzi. Kulibadilisha wazo ili liwe maswali faafu na ya kutegemewa ambayo yanapima hasa kile yanachopaswa kupima huhitaji mawazo ya kindani na ususi wa makini.