Tafiti huwa muhimu wakati wa kufahamu jumuiya kubwa ya watu. Lengo ni kuhoji kundi ndogo la jumuiya ambalo huwakilisha jumuiya nzima. Sampuli huwa changamano na huhitaji takwimu nyingi na hesabu. Hata hivyo, ni vyema kuelewa kwanza msingi wa mantiki ndipo uweze kuwasiliana na kampuni za utafiti wa nyanjani yale ambayo ni muhimu na kuelewa wafanyayo kwa utoshelevu.
Ni kwa jumuiya ipi habari inatafutwa na kujumuishwa? Je, ni wapiga kura wote? Ni wale wanaoelekea wapiga kura pekee? Wanaume pekee au wanawake pekee? Ni wenye umri mdogo tu au wazee? Ni wapigakura waafrika au wazungu?
Ukichukua sampuli ya jumuiya kubwa inaweza kulinganishwa na kuandaa mchuzi. Wakati wa kuchanganya mchuzi kwa bakuli kubwa, mpishi hodari atakueleza kuwa unahitaji kuonja tu vijiko viwili au vitatu ili kuelezea utamu wa bakuli nzima ya mchuzi huo. Wazo hili huchukulia kuwa mchuzi umechanganywa vyema kwenye bakuli na kuwa chumvi haipatikani tu katika sehemu moja ya bakuli au vyazi havijatulia chini ya bakuli na vitunguu saumu kuwa sehemu moja ya bakuli. Iwapo mojawapo wa haya matokeo yatapatikana itachukuliwa kuwa kijiko cha supu ile hakitawakilisha bakuli nzima. Vilevile ikichukuliwa kuwa supu imechanganywa vizuri kwenye bakuli, kwa kubahatisha kuchovya vijiko hutoa wazo nzuri la utamu wake na haijalishi iwapo mchuzi ule ulitolewa katika chungu cha kawaida kwa jiko la nyumbani au kutoka kwenye vyungu vitumikavyo mikahawani vilivyotengenezewa viwandani. Idadi sawa ya vijiko hutoa matokeo sawa iwapo mchanganyiko ulifanywa vizuri kwenye bakuli. Idadi ya mchovyo wa vijiko inaweza kuongezwa kwa viwango toshelevu lakini sio kama vile kuongeza viwango vya bakuli.
Katika jumuiya ndogo iliyochanganywa vyema kuna makundi (au safu ya watu) ambao mielekeo yao hutofautiana kabisa na ya watu wengine (kama vile kuna tofauti za mwonjo wa aina za mboga na za viungo vyenye ladha) ambao wamechaguliwa kwa kubahatisha. Hata hivyo watu hawa huwekwa kwenye kundi moja katika maeneo fulani, miji ama ujirani.
Uwezekano wa sampuli kukosa au kutowakilisha makundi au safu zilizochakuliwa kwa bahati nasibu hupungua kwa kiwango kikubwa. Katika matokeo, wakati wa kuchagua sampuli inayowakilisha jumuiya(bakuli ya mchuzi) itahitaji kupanga safu ili kupata makundi madogo yaliyo tofauti na kuchagua sampuli ndogo ya jumuiya hii dogo (ili kupata sampuli ya kutosha ya viazi, mchele na nyanya).
Hii inamaanisha kuwa unazingatia kuwakilisha watu wa rangi zote, jamiilugha zote, sehemu zote, tajiri na masikini, au waishio mijini na mashambani. Kwa kawaida uundaji wa safu hizi hutegemea kiwango cha safu ya jumuiya halisi. Hivyo, kama komponenti/kiungo cha mashambani ya jumuiya kinayohitajika ni asilimia 52, sampuli ya komponenti ya mashambani inatakiwa kuwa sawa nayo.
Hata hivyo, wakati uamuzi wa kupanga safu kwa mwelekeo wa zaidi ya vipimo viwili, maamuzi kulingana na mchanganyiko wa sampuli, huenda yakawa tata. Kwa mfano, sampuli ya kitaifa nchini Afrika Kusini huenda ikaamuru katika idadi fulani ya watu wenye mchanyiko wa rangi, watu wa mashambani kutoka magharibi mwa Cape huhitajika pamoja na idadi ya Waafrika na wazungu wa mashambani kutoka katika huo mkoa. Hii humaanisha pia kuchukua idadi ya watu kwenye miji mikuu kutoka kwa makundi yote kwenye mkoa huo. Mwanataaluma wa takwimu za kijamii au mwanahisabati anaweza kusaidia katika kuchanganua hali hii kwani huenda ikawa ngumu kwa mtu wa kawaida.