Kwenda nyumba hadi nyumba
Baada ya kupata sampuli ya jumla inayohitajika kwa mfano; idadi kamili ya sampuli, na idadi ya mahojiano yatakayofanywa katika kila kisafu yamechaguliwa, hatua itakayofuata ni kuweka sampuli itakikanayo katika mahojiano halisi.
Aghalabu kuna njia mbili tofauti za kuzingatia kwa wakati huu. Jambo muhimu kubainisha ni kufanya uchaguzi kati ya sampuli ya bahati nasibu au sampuli kiasi.
Sampuli ya bahati nasibu
Hapa kila mtu katika jumuiya ana nafasi sawa ya kuchaguliwa katika sampuli ya mwisho. Hii inakisia kuwa idadi ya jumuiya nzima hujulikana. Ikiwa idadi hiyo ni “n” hivyo bahati ya mtu kuchaguliwa =1/n.
Ikiwa kunayo orodha ya watu wote wanaoishi katika jumuiya fulani, sampuli ya bahati nasibu halisi humaanisha kuchagua kwa bahati nasibu majina kutoka kwa orodha hiyo ya jumla hadi kufikia idadi inayotakikana. Au, kama sampuli imepangwa katika vijisafu(kwa mfano; watu waishio mashambani na mijini), idadi ya majina ya wanaoishi mijini ikiwa kama X, na Y kama idadi ya majina ya wanaoishi mashambani kutoka katika orodha, huchaguliwa. Watu hawa watatembelewa, watapigiwa simu au kutumiwa hojaji kwa njia ya posta wakati sampuli imechaguliwa.
Mahojiano ya kibinafsi kwa kutumia sampuli ya bahati nasibu huwa ghali hata pale ambapo kuna orodha kamili yakila mtu katika jumuiya. Kuwatuma watafiti waliochaguliwa kwa bahati nasibu katika sehemu zilizochaguliwa kwa bahati nasibu bila kujali umbali ulioko kati ya sehemu zilizojitenga na sehemu zingine za utafiti ni ghali. Hivyo, nyingi za mbinu za mahojiano ya kibinafsi hutumia makundi ya sampuli nasibu. Gharama ya usafiri hupunguzwa kwa kutuma kikundi cha watafiti kwenye sehemu zilizochaguliwa kwa bahati nasibu kisha kufanya mahojiano kadhaa katika eneo hilo.
Sampuli ya makundi hutumika sana kwa sababu hupunguza gharama na pia kwa sababu orodha ya majina mara nyingi huwa haipatikani. Nchi nyingi, mikoa au manispaa huwa hazina orodha hizi, na iwapo zinazo, hazitampa mtafiti.
Hata hivyo, ingawa idadi ya jumuiya nzima na idadi ya watu wanaoishi katika sehemu mbalimbali au katika makundi mbalimbali huenda ikajulikana, kuna uwezekano wa kutokuwa na orodha ya majina kamili ya watu. Sampuli ya vijikundi katika maeneo ya sapuli husaidia watafti kwenda kwenye nyumba za watu binafsi ili kudumisha bahati nasibu na usawa wa bahati ya kuchaguliwa.
Kwa wakati mwingine, huenda ikahitajika kuwa na sampuli safu nasibu isiyolingana. Hii hutokea wakati kundi linalohitajika huhusisha sehemu ndogo sana ya jumuiya inayohitajika. Kwa mfano, sampuli inayolingana kule Afrika Kusini huhusisha asilimia 9 pekee ya wahojiwa wenye rangi tofauti na kama asilimia 2 ya wenye asili ya Kihindi. Lakini ikiwa, sampuli ya kitaifa ni watu 2,000, kwa sababu ya gharama, hii itatoa matokeo ya chini ya wahojiwa halisi wa rangi tofauti 200 na kama wahojiwa 40 wenye asili ya Kihindi.
Hata hivyo huenda isiwezekane kutegemea takwimu ya makadirio ya kundi la sampuli la watu 40. Hata ikiwa ni watu 200, kosa la takwimu huenda likawa kubwa kiasi cha kutokuwa na usaidizi wowote wa malengo ya kuongoza utaratibu wa wapiga kura wa rangi tofauti katika jamii lengwa. Hii huenda ikawa ya umuhimu mkubwa iwapo mtu angependa kutathmini tofauti zilizopo kati ya wanaume na wanawake, au waishio mijini na wanaoishi mashambani, au wanaounga mkono chama katika makundi ya sampuli ya watu wa rangi tofauti na yaliyo na watu wenye asili ya Kihindi. Idadi ya wahojiwa katika haya makundi yataanza kuwa na usaidizi finyu usioweza kusaidia.
Hivyo, sampuli ya kupita kiasi ya makundi madogo kama haya huweza kutumika. wakati ambapo makundi madogo yanaweza kupitisha tu mahojiano arobaini kwa kuzingatia misingi ya uaswa, uamuzi waweza kutolewa kufanyisha mahojiano mia moja ili kuwa na habari ya kutegemewa. Wakati data yote imechaguliwa, sampuli isiyokuwa na usawa hurekebishwa kwa kutathmini mahojiano mia moja kwa vipimo vinavyofaa ili viwakilishe sampuli yote kikamilifu.
Kutathmini pia husaidia katika hesabu ya watu ambapo habari hupatikana, na huenda isijulikane hadi wahojiwa watakapokubali. Kwa mfano, idadi ya wanaume kwa wanawake katika jumuiya inayotakikana na pia idadi ya watu katika safu kadhaa za kielimu huenda ikajulikana. Lakini huenda isijulikane iwapo tutapea kipaumele sampuli safu kwa sababu, mtafiti hatapata habari hadi pale atakapokaribishwa kwa nyumba au simu yake ijibiwe, iwapo mhojiwa ni mke au mume au kiwango cha elimu walicho nacho.
Iwapo sampuli imekamilika, inawenza kulinganishwa na jumuiya halisi kwa kuegemea hesabu za watu ambapo habari hupatikana. Watu katika sampuli wanaweza kutathminiwa kwa upande wowote unaotakikana. Hebu fikiria, kwa mfano, idadi ya wanawake maradufu katika sampuli inahojiwa kuliko wanaopatikana katika jumuiya nzima. Kwa kisa kama hiki, kila mwanamke katika sampuli atatathminiwa ili kuleta uwiano wa wanawake katika sampuli kuwa unaotakikana.
Uundaji wa sampuli ni msingi wa kujua gharama ya utafiti husika. Sampuli inayohitaji kiasi kikubwa cha wahojiwa kutoka sehemu za mashambani huenda ikawa ghali kwa kuwa watafiti watahitajika kwenda sehemu za ndani za mashambani.
Ili kuweza kutafiti sampuli wakilishi kwa msingi wa kitaifa, kwa kawaida huhitaji kiwango kizuri cha muundo msingi na wafanyikazi wenye ujuzi. Hivyo, mashirika ya kijamii hutoa kandarasi ya kuendesha mahojiano halisi kwa shirika la kitaaluma hata kama yana uwezo wa kuunda mradi na kuchanganua matokeo.
Hii huhusisha uchaguzi wa msururu uitwao vitengo msingi vya sampuli vitengo vya kimsingi vya ukaguzi (PSUs). PSUs ni vitengo vidogo zaidi ambavyo maeneo ya sampuli za mwisho yatachaguliwa kibahati nasibu. PSUs huhusisha maeneo madogo ya kijiografia ambako kuna data ya jumuiya inayotakikana (na kwa tafiti nyingi hii humaanisha jumuiya ya miaka 18 na zaidi). Katika majimbo mengine yaliyo na data nzuri ya sensa, hizi huweza kuitwa maeneo ya takwimu.
Maeneo ya sampuli za mwisho hayawezi kuchaguliwa kwa bahati nasibu kutoka katika PSUs kwa sababu PSUs yatakuwa karibu kila mara na kipimo cha jumuiya tofauti. Hata mahali palipo na takwimu zinazojulikana za Maeneo ya Sensa (EAs) inayohusisha nyumba kiasi fulani kila moja (kwa mfano, huko Zimbabwe EAs huwa na nyumba kila moja), idadi ya watu katika kila nyumba hutofautana. Hivyo kila PSU ya kutegemewa lazima itathminiwe kwa idadi halisi ya watu wanaoishi katika nyumba husika. Kutokana na haya, nafasi ya kuchagua eneo la sampuli ya mwisho kutoka kwa PSU lazima iwiane na idadi halisi ya jumuiya ya PSU.
Wakati kila PSU imetathminiwa kulingana na idadi ya jumuiya, maeneo ya sampuli ya mwisho yanaweza kuchaguliwa kwa bahati nasibu kutoka kwa orodha ya PSUs. Idadi halisi ya maeneo ya sampuli ya mwisho hutegemea idadi ya mahojiano yatakayofanywa katika kila eneo na idadi kamili ya sampuli. Tafiti nyingi huendesha kati ya mahojiano tano na saba katika kila eneo. Hivyo, iwapo mahojiano matano yatafanywa katika kila eneo, na jumla ya idadi ya sampuli ni 2500, orodha ya maeneo ya sampuli ya mwisho 500 lazima ichaguliwe kibahati nasibu.
Sasa tunafahamu tunakoelekea. Kwa mfano, orodha iliyoundwa inaeleza kuwa kuna vitongoji 350, vile vinavyojulikana sana vinaweza kuchaguliwa zaidi ya mara moja, na wilaya za uhakimu za sehemu za mashambani 150. Watafiti watatafuta ramani za kila mojawapo wa sehemu hizi, na kuchagua sehemu maalum katika kitongoji kibahati nasibu. Hii huenda ikachanganuliwa sana kwani watafiti wengine watapanga maeneo yaliyoorodheshwa kibahati nasibu kwa uwazi kisha wachague nambari kwa bahati nasibu, na waangalie inapatikana wapi kwenye ramani. Hapa ndipo mwishowe watatuma watafiti.
Katika maeneo mengi ramani nzuri haziwezi kupatikana. Au, ramani za maeneo ya mashambani huenda zikawa kubwa sana kiasi cha kuonyesha tu sehemu zilizo na miji mikuu, lakini bila kuonyesha barabara katika miji. Katika kisa kama hiki, mtu atafanya uamuzi wa kuanzia mahali pa kawaida kama vile kanisa, shule, jingo la munispaa au mfereji wa maji.
Wakati watafiti washajua wanakotakikana kwenda, wanastahili kuzingatia sheria fulani zinazowawezesha kuchagua nyumba, lakini kwa bahati nasibu. Kwa mfano, wanaweza kwenda eneo lililokubaliwa, waangalie mashariki au magharibi kisha waelekee kwa nyumba kumi, na wafanye mahojiano katika kila nyumba ya tano. Sheria zinastahili kuwa nasibu, lakini mahojiano yote yanastahili kuzingatia sheria sawa. Wazo hapa ni kwamba mtafiti hastahili kuwa na uhuru wa kuchagua nyumba.
Hatua ya mwisho huhusisha uchaguzi wa mhojiwa halisi. Pia, ili kutoa nafasi sawa kwa kila mtu ya kuchaguliwa, si vyema kwa mtafiti kuongea tu na wale wanaowakaribisha kwa nyumba au wale wanaoshika simu. Kama watafiti wanaongozwa na sampuli iliyochaguliwa kutoka katika rejista ya jumla ya jumuiya, hivyo, wanahitajika kuwahoji tu wale ambao majina yao yanapatikana katika orodha.
Iwapo orodha kama hii haipo, wakati watafiti wako kwa nyumba au wanazungumza kwa simu, wanastahili kuweka takwimu ya nyumba, au waorodheshe watu wanaoishi katika nyumba ( na kwa kawaida wawe wazaliwa wa nchi wenye umri wa miaka 18 au zaidi). Kisha, wanastahili kuchagua jina moja kwa bahati nasibu na wamhoji tu huyo mtu. Njia ya kawaida ya kumchagua mtu kama huyu kwa bahati nasibu ni kwa kuuliza yule aliyesherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi majuzi. Katika sehemu za mashambani watu huenda wakatamaukiwa kwa kukosa kupewa nafasi ya kuchaguliwa kwa bahati nasibu. Njia nzuri hapa ni kupeana kadi za rangi kwa kila yule awezaye kuhojiwa, na kuzitwaa kisha kuuliza kila mmoja wao kuchagua kadi kutoka zilipowekwa, yule atakayechukua kadi inayotakikana ndiye atakayehojiwa.
Hata hivyo, si kila mlango tunaobisha au kila simu tunayopiga italeta utafiti kamili. Watu wengi hawatakuwa nyumbani, wengi watakuwa nyumbani lakini hawataweza kupatikana kwa sababu mbalimbali na wengi watakataa kuzungumza na watafiti. Kama tulivyosema hapo awali, ni muhimu watafiti kutokubali watu kujitenga katika sampuli. Hii ni kwa sababu, wale ambao hawako nyumbani au hawana hamu ya kushiriki wana uwezekano wa kuwa tofauti na sampuli nzima katika mambo muhimu.Wale ambao wana uwezekano wa kupatikana nyumbani, haswa mahojiano yanapofanywa katikati ya wiki, wanaweza kuwa vijana wadogo, wasiokuwa na ajira, wake nyumbani na wazee. Wale ambao hawatahiari kuzungumza na watafiti huonekana kujitenga na watu wengine. Watu wa aina hiyo huhitajika kuwakilishwa katika sampuli yoyote. Jambo hili huwa wazi, hasa wakati ambapo kujitenga huku kunahusishwa na mada inayohusika kama vile kupiga kura.
Wanaojitenga kuhojiwa wanaweza kusababisha maafa katika uwakilishaji wa sampuli. Kule Marekani, viwango vya wanaojitenga kuhojiwa vimeongezeka maradufu kuanzia miaka ya 1950. kwa kati ya asilimia 12 hadi asilimia 22 kila mahali na asilimia 30 hadi 55 katika mahojiano ya kibinafsi, huku asilimia 25 hadi 35 katika sampuli ya simu. Katika Afrika Kusini, wanaojitenga kuhojiwa waliongezeka hadi asilimia 100 katika maeneo ya Wazungu wanaoshikilia tamaduni zao, kulingana na utafiti uliofanywa kati ya 1993 na 1994.
Njia moja itumikayo sana kurekebisha hali hii ya kujitenga kuhojiwa ni kwa kutathmini mahojiano yaliyopatikana dhidi ya takwimu za sensa zinazojulikana. Kwa hivyo, kama haitaridhisha vijana wa umri wa kati wa kiume walihojiwa. Mahojiano yao hutathminiwa kwa vijisehemu. Kwa mfano, iwapo kuna nusu pekee ya kikundi hiki kuliko tulichohitaji katika sampuli iliyotakikana, tunapiga hesabu ya kila mojawapo mara 1.5.
Jambo hili huzua tatizo kwa sababu huchukulia kwamba wale ambao hawakuhusishwa katika sampuli au waliokataa kuhojiwa, kuwa wako sawa na wale waliohojiwa katika mitazamo yote kama ilivyofanywa katika utafiti. Hata hivyo, kuwa mtu hakuwa nyumbani (pengine kazini au dukani) au kuwa walikataa kuzungumza na watafiti hufanya wawe tofauti na wale waliokuwa nyumbani au wale waloikubali kuzungumza na watafiti.
Kuna baadhi ya mambo yanayoweza kufanywa ili kupunguza visa vya watu kukataa kuzungumza.Watafiti wanastahili kupewa mafunzo ya kina ili wawe wapole iwezekanavyo. Hojaji inastahili pia kuhusisha utangulizi unaofanya utafiti kuwa wa kuvutia kwa wanaotarajiwa kuwa wahojiwa na pia kuonyesha wazi umuhimu wa maoni yao. Mwisho, watafiti wanastahili kuuliza iwapo wamefika kwa wakati mwafaka la sivyo wawe tayari kuomba nafasi ya kukutana wakati mwingine ambapo mhojiwa hatakuwa na shughuli nyingi na anaweza kutenga wakati kwa mahojiano. Yaani wawe na miadi mwafaka na wahojiwa ili waweze kupata habari kutoka kwao.
Watafiti wanaweza kujaribu kupunguza visa vya watu kukosa kuwa nyumbani kwa njia kadhaa. Kwanza, wanastahili kujaribu kufanya mahojiano nyakati za jioni na wikendi. Katikati ya wiki huwa vigumu kwa sababu wanaofanya kazi huwa hawapatikani nyumbani, lakini wake nyumbani wanaweza kuwa na wakati mwingi wa kuongea. Wakati mbaya zaidi ni ule watu wanapojiandaa kupata chajio, wakati wanaandaa chakula au wanakula, hapa huwa wanagadhabishwa kwa kusumbuliwa.
Pili, watafiti wanastahili kuwa waangalifu sana kwa kile kiitwacho ‘nitarudi tena’ call-backs. Kama mtu aliye kwenye orodha au aliyechaguliwa kwa bahati nasibu kwa mfano kwa kutumia mbinu ya siku ya kuzaliwa hayuko, watafiti wanastahili kuuliza wakati mtu huyu anatarajiwa kuwa nyumbani ili warudi tena kwa wakati huo waweze kuendelea na mahojiano. Mashirika mengi ya utafiti huhitaji watafiti kutua sehemu mara mbili au tatu ili kumpata mtu halisi aliyechaguliwa. Tafiti kubwa zingine hutoa habari kupitia kwa vyombo vya habari.
Ni wakati tu mtafiti ametua safari zinazohitajika bila kufaulu ndipo atakaporuhusiwa kumhoji mtu badalia kwa nafasi ya mhojiwa halisi. Pia hawastahili kumpata mhojiwa badalia kutoka kwa nyumba hiyo bali wanastahili kufuata sheria kama vile kuendea nyumba zingine mbili au tatu, kulia au kushoto au kupiga simu kwa namba mbili mpya kwenye orodha chini au juu ya namba asilia na kuumaliza mchakato ule ule tena.
Jitihada hizi zote hufanywa ili kuhakikisha kuwa wale ambao huenda wasipatikane nyumbani hawaondolewi kwenye sampuli na kuwa hawapati wahojiwa badalia ambao hawapatikani nyumbani kwa urahisi.
Manufaa ya sampuli nasibu ni kuwa huruhusu watafiti kunufaika na sheria za kihisabati za sampuli kwa manufaa ya kujumlisha matokeo ya sampuli kwa jumuiya kubwa. Sheria hizi hutueleza kuwa avereji au mini ya sampuli yoyote iliyochaguliwa kwa bahati nasibu itakuwa sawa na mini ya jumuiya nzima ambamo ilichaguliwa. Kwa kila idadi ya sampuli iliyopeanwa, sheria hizi hutoa fomula ya kufanya hesabu ya kosa lenyewe katika sampuli yoyote. Hivyo katika idadi ya sampuli iliyotolewa, makisio ya sampuli yatakuwa kuongezea au kuondoa mini halisi ya jumuiya nzima kwa asilimia 95 ya wakati. Hii ni kwa sababu ya wingi wa idadi ya sampuli zinazochaguliwa. Sheria za uwiano huashiria kuwa kama asilimia tano itakuwa nje ya kawaida ya ukubalifu wa kosa . Hata hivyo, asilimia 95 ya sampuli itakuwa katika kiwango cha ukubalifu katika mini ya jumuiya ya ukweli. Idadi ya sampuli ikiwa kubwa, kiwango cha ukubalifu huwa ndogo.
Sehemu Rasmi za Kiasi Zinazotarajiwa
Njia mbadala ni ya sampuli rasmi za kiasi. Hapa sampuli nzima huchaguliwa kuwakilisha jumuiya nzima kwa kutegemea vipengele vyote vinavyoitofautisha kwa mfano, uamuzi hufanywa kuwa sampuli inastahili kuwa na asilimia fulani kutoka katika kila mkoa na kila mji, asilimia fulani ya wanaume na wanawake, asilimia fulani ya kila jamii-lugha na ya kila tofauti ya rangi. Hata hivyo, uteuzi wa mhojiwa wa mwisho huachiwa mtafiti. Kila mtafiti hupewa sehemu rasmi ya kiasi anayotarajiwa kujaza katika eneo lake: hapa orodha ya majina ya watu ambao lazima wawapate na wawafanyie mahojiano wanaotosheleza kategoria zote za watu. Kwa hivyo, mtafiti anaweza kuambiwa kutafuta wanaume watano na wanawake watano wa Kiafrika wanaoishi mjini na wanawake wanane na wanaume saba wanaoishi katika sehemu za mashambani. Hata hivyo, hawaambiwi nyumba wanamopatikana watu hawa au barabara au njia yoyote ya kinasibu ya kufuata. Ni lazima tu wawapate watu hawa kutoka kwa kategoria zinazohitajika. Kwa sababu watafiti hupumzishwa shughuli ya kupitia kwa hatua zote za kinasibu tulizofafanua pale juu, wana uwezo wa kupata wahojiwa kwa haraka na kwa gharama ya usafiri ya chini. Jambo hili hufanya sehemu za kiasi kuwa si ghali kuliko sampuli nasibu.
Hata hivyo, changamoto kubwa ni bahati nasibu za kuhusishwa zinazojulikana na zilizo sawa zenye sifa za sampuli ya bahati nasibu zimepeanwa, nadharia za kihisabati za bahati nasibu haziwezi kutumika hapa kutoa matokeo ya kuwakilisha jumuiya nzima. Marudio ya majibu kutoka kwa sampuli ya sehemu kiasi yanaweza kufanywa. Hata hivyo, kiwango cha uwakilishaji wa idadi halisi katika jumuiya nzima hakiwezi kupatikana.