Kuingia nyanjani kunahitaji uteuzi na ufunzaji wa watafiti pamoja na upangaji na uongozi wao.
Watafiti
Pale ambapo itawezekana, watafiti waliofanya mazoezi na walio na tajiriba pekee ndio wanaopaswa kutumiwa. Isitoshe, uelimishaji ni muhimu sana katika utafiti. Ikiwa watafiti wataalamu hawapo, basi shughuli za kuteua wahojiwa nyumbani zinafaa kukaguliwa kwa undani. Hojaji inapaswa kupitiwa kikamilifu, ikiwemo jinsi ya kusoma maswali hayo na kutilia mkazo maneno halisi. Umuhimu wa kuwapa wahojiwa heshima inayostahili na kutowakasirisha inapaswa kutiliwa mkazo. Watafiti pia wanafaa kuonywa dhidi ya kuwapa wahojiwa picha mbaya kupitia kwa mavazi yao, sura zao au miondoko ya miili yao.
Wanafunzi wa vyuo vikuu huajiriwa kama watafiti kwa sababu hawahitaji gharama kubwa. Hata hivyo, onyo dhidi ya uteuzi huu limewekwa. Wanafunzi wenye hamu ya utafiti wa mfumo wa kisiasa na jamii huwa na raghba haswa katika mambo ya kisiasa na wanaweza, mara kwa mara, kuwasilisha maoni yao kwa njia zisizofaa.
Kama tulivyotangulia kusema, inampasa mtu kuhakikisha kuwa watafiti na wahojiwa ni wa asili moja haswa ikiwa utafiti huu unahusu maswala yanayowiana. Kwa nyakati nyingine hata hivyo, utaratibu tofauti unahitajika kufuatwa.
Kazi za nyanjani
Kazi za nyanjani zinapaswa kuwa chini ya usimamizi mkali wa wasimamizi wa nyanjani. Kampuni zenye hadhi ya hali ya juu huendesha ‘nitarudi tena’ kwa asilimia 10 hadi asilimia15 ya nyumba zilizohojiwa, hutafuta aliyehojiwa ili kuhakikisha kuwa alihojiwa na pia hupitia maswali kuhakikisha kuwa majibu yaliyonakiliwa ni majibu halisi.
Pengine jambo lenye umuhimu hata zaidi ya kufanya hivi, ni kuwajulisha watafiti kuwa jambo hili litatendwa na malipo yao yatategemea matokeo yao yatakayotokana na ‘nitarudi tena’ hizi. Watafiti wa kazi za nyanjani hawana tofauti zozote na kundi wakilishi katika jamii. Kwa bahati mbaya, ripoti zimewasilishwa na watafiti kuhusu kuwapata wafanyakazi wa nyanjani wameketi chini ya mti na kujaza hojaji huku wakitumia majina bandia, anwani na majibu. ‘Nitarudi tena’ zinaweza kupitishwa kupitia kwa simu ikiwa huduma hii ni wazi kwa jumuiya nzima. Ikiwa ni nadra ‘nitarudi tena’ zinapaswa kufanywa kibinafsi na kabla ya timu ya watafiti kuondoka katika eneo teule.
Wasimamizi wa nyanjani wanapaswa kupitia hojaji zote kabla ya timu ya watafiti kuondoka katika eneo teule ili kuhakikisha kuwa kila kitu kimejazwa kwa ukamilifu na usahihi, na ikiwa si hivyo, basi wanapaswa kumtuma mtafiti arudi kwa mhojiwa ili kupata ujumbe unaotakikana.
Kupata data
Majibu halisi yatahitajika kutiwa katika muundo wa kusomeka katika tarakilishi. Kuna virobota vya programu ya tarakilishi vya takwimu kadhaa ambazo hutoa makala ya kuingiza data yanayoweza kufikiwa kwa urahisi na vinaweza pia kusoma na kumiliki data pale inapoingizwa katika tarakilishi. Statistical Package for the Social Sciences (SPSS) ni mojawapo ya programu zinazotumiwa pakubwa.
Kampuni za utendaji kazi nyanjani zitaingiza data hii na kutoa ripoti stadi. Shirika linalolipia utafiti linafaa kuwa na data yake lenyewe katika kisanturi cha tarakilishi, haswa kinachowiana na muundo wa SPSS. Shirika hili huenda pia linataka kufanya uchambuzi wake mwenyewe, au kama halina tajriba katika uwanja wa takwimu, hutegemea yeyote yule mwenye tajriba kufanya vile. Shirika hili linapaswa kuwa na uhuru wa kuendesha na kutathmini kilichotolewa. Kuna uwezekano pia wa kuwa na seti nyingine kubwa za umiliki wa data, mpangilio au uhusiano, ambazo zinaweza kuendeshwa, lakini kampuni ya utafiti haitawasilisha hizi katika ripoti yake stadi.
Wakati
Ili kufanya kazi nzuri, kipindi cha muda kutoka ukusanyaji hadi uchambuzi na kutoa ripoti ya data husika kinaweza kuwa kirefu kupindukia. Hata pale ambapo kuna umuhimu mkubwa wa kwenda nyanjani kwa haraka ili kunasa hisia za umma kuhusu tukio la dharura, ni vigumu kutafakari kuhusu kufanya kazi nzuri kwa muda wa chini ya wiki sita.
Gharama
Gharama ya miradi itahusisha gharama za uendeshaji, uingizaji wa data, na gharama za jumla. Sehemu kubwa ya gharama hizi ni ya utendaji kazi uwanjani na unahusisha gharama ya usafiri,upangaji na kazi halisi ya watafiti na wasimamizi wa nyanjani. Watafiti hutegemea idadi ya mahojiano yanayohitajika kufanywa, idadi ya simu zitakazopigwa au idadi ya nyumba zitakazotembelewa ili kutathmini idadi ya mahojiano kamili, idadi ya maeneo ambayo hayawezi kufikiwa kwa urahisi na muda wa kila mahojiano. Hivyo basi, idadi ya sampuli, kusafu, ukusanyaji wa mahojiano na ikiwa uwezekano au sampuli ya kiasi imetumika ni muhimu kiutaratibu na kigharama.
Kwa vile kuendesha shughuli za utafiti huru huhusishwa na gharama, inawezekana kupata nafasi ya swali moja au mawili ya tafiti zinazoendelea au hata kumi na mawili. Mashirika ya utafiti hupendelea kufanya utafiti mara kwa mara,na kwa sababu idadi kubwa ya wateja wao wanaweza wakaongezea maswali. Gharama za utafiti hugawanywa. Gharama hizi huenda zikahesabiwa kulingana na kila swali pamoja na malipo ya awali. Mashirika mengi huamua kutegemea maswali yao kutoka kwa tafiti zinaoendelea. Hii huwa njia mwafaka wakati mtu hutaka kuongezea maswali machache kwa sampuli wakilishi. Kwa mfano, kuchunguza mielekeo iliyopo kuhusiana na uchaguzi unaokaribia au viwango vya usajili vinavyofanywa. Vilevile, urudiaji wa tafiti kama hizo humwezesha mtu kuchunguza hali kila wakati na kuelewa mielekeo kwa wakati mrefu.
Maswali kama “Kwa nini watu wana haja sana?” au “Kwa nini watu hawajajisajili?” hutuongoza kwa maswali mengi ya kujiuliza. Maswali yakiwa mengi, gharama huelekea juu. Kwa kuongezea kwa haya, inaweza kuwa muhimu kupata wahojiwa walio katika hali ya kupiga kura ya uchaguzi na demokrasia ili kupata majibu mwafaka. Ukiwa na tafiti zilizofanywa, huenda pasiwe na mamlaka juu ya iwapo wahojiwa wanajibu swali kuhusu mashindano ya uchaguzi mara moja au waulizwe kuhusu vile wanavyotumia mafuta ya petroli kwa kila mwezi. Mwishowe, kwa sababu ya gharama inayohusika na mahitaji ya wateja, tafiti zinazoendelea huenda zisifanywe katika maeneo ya mashambani au yaliyo na wakazi maskini.