Huku wanaofunza wakijiandaa na kulenga vikundi na tafiti, wengine huamua kwenda nyanjani kuzungumza na watu ambao wanafanya kazi na hadhira lengwa au eneo la uwakilishi bunge. Hii huwa yenye manufaa ya kutohitaji muda mwingi, iwapo itafanywa kwa makini kuhusiana na ubainishaji wa wanaoshiriki katika mjadala ili wafahamishwe. Pia husaidia wanaotoa elimu hii kufahamu tofauti ndogo na kutoelewana ambapo ingekuwa tofauti kupata iwapo njia ile nyingine ingetumiwa. Umuhimu mwigine ni kuwa watu kama hawa hutoa elimu ya kawaida kuhusu mazingira ya kielimu, mazingira ya kisiasa, na kutambua mahitaji mengine ya kielimu.
Huku kuuliza au kujadiliana huendeshwa katika kiwango cha weledi, waelimishaji kwa waelimishaji, au katika kiwango cha muelimishaji na kiongozi wa jamii. Kwa hivyo kuhakikisha kwamba umilikaji wa vipindi hujengwa kuanzia mwanzo. Kuna pia changamoto kwa njia hii, hasa wakati ambapo itategemea uondoaji wa data iliyokusanywa na kuongezwa. Lakini kwa manufaa ya kielimu ambapo elimu ya kawaida na umilikaji wa kawaida ni muhimu ni yenye nguvu na si ghali kuanzisha shughuli hii.
Inaweza kuongezewa ubora wake kwa gharama yake kwa kuiongezea mbinu mbili zinazohusiana. Ya kwanza ni makongamano ya kushauriana ambapo watu huja pamoja na kujadiliana mahitaji ya kielimu, na mazingira ya kielimu katika mtindo uliobainishwa. Mtindo uliobainishwa unaweza kuwa rasmi kiasili, na wazungumzaji tofauti wakizungumzia mada tofauti au iegemee sana kwa dayolojia isiyo rasmi, na utangulizi mfupi utakaofuatwa na majadiliano. Ulengaji wa uteuzi wa makundi ya wanachama hutegemea uelewaji wa mweledi na uelewa wa kawaida.
Aina Mbili Tofauti ya Watu
Kwenda nyanjani na kuwahoji watu kwa bahati nasibu hakutoshi. Umakinifu wa uteuzi wa wahojiwa unastahii kuzingatiwa. Kuelewa maneno mawili “washiriki wa mijadala” na “waamuzi” humwongoza mtu katika uchaguzi unaostahili kufanywa. Maneno haya pia huashiria baadhi ya matatizo na upungufu ambao huenda ukakumbana nayo na kudokeza umakini unaostahili kuwa nao. Washiriki wa mijadala huzungumza kwa nafasi ya uwakilishi bunge lengwa au kwa niaba yao. Waamuzi huwa kati ya waelimishaji na hadhira na hufanya kazi ya kuwaunganisha.
Waelimishaji wataunda orodha ya watu ambao watazungumza nao kwa kutegemea utathmini wa elimu ya jamii na mashirika ya kijamii yanayoshughulikia uwanja sawa wa utafiti. Uwanja wa utafiti huenda ukawa wa kitaifa, kimaeneo, au wa kwaida. Pia, watatambua viongozi wa kijamii kwa kutegemea uhalali wao katika jamii fulani.
Mwishowe, wanaweza kuanza mazungumzo mema na watu wanaowaunganisha na jamii ya waelimishaji, kama vile wanafunzi, wasomi na wanachama bodi ya kidiplomasia. Hawa huenda wakawa wa muhimu ambapo kuna pengo kubwa kati ya kundi la waelimishaji na jamii; kwa mfano, iwapo kunao mpango wa kimataifa unaopangwa au wakati kikundi cha waelimishaji kinazuru maeneo ambayo hawajawahi kuzuru. Ni vyema kuwashirikisha watu hawa pamoja na waelimishaji katika mipango ya ziada ikiwezekana, hata kama watafsiri au madereva iwapo sio kama waelimishaji wenyewe.
Kutambua Watu
Wakati orodha ya majaribio imekusanywa, inaweza kutathminiwa na watu ambao wametambuliwa tayari. Kwa maneno mengine kukusanya orodha ya majina ya watu ni shughuli ya kurudiarudia. Waelimishaji hutambua watu kwa mara ya kwanza, pengime kwa kutegemea kwa habari waliyoipata kutoka kwa shirika la kijamii la kutegemewa, au hata maelekezo kutoka kwa tume ya uchaguzi. Kisha watu hawa hupendekeza wengine ambao waelimishaji wanastahili kuwazungumzia.
Orodha ya pili itaoana na kuhusishwa watu wasioteuliwa lila wakati. Majadiliano ya pili yatafanywa wakati orodha imekuwa kubwa. Kwa wakati fulani, katika zoezi hili, orodha itakuwa ya mzunguko. Yaani waelimishaji watakuwa wanatumwa kwa watu ambao tayari wamejadiliana nao.
Waelimishaji hutaka kuwa makini ili kudumisha rekodi nzuri ya majadiliano waliiyokuwa nayo na habari kuhusu wale waliofanyiwa mahojiano.
Usiri
Kwa wakati ambao majadiliano haya yamefanyika katika miktadha ya kivita, na mahali waliohusika wanajadili kuhusu matakwa ya wanachama wa uwakiishi bunge wao, patakuwepo na haja, habari itakayokusanywa itachukuliwa kwa siri, hasa wakati majadiliano yanafanywa kati ya weledi, patakuwepo na hoja nzito na zinazoashiria makundi yanayoendesha shughuli zao katika jamii na katika uakilishi bunge husika. Mijadala hii huchukuliwa kuwa mipango inafanywa kusaidia hadhira inayolengwa. Matumizi mengine ya habari yoyote yanaweza kuwa na athari kuhusu uhusiano uliopo kati ya wale wanaohojiwa na jamii wanamofanyia shughuli yao.
Changamoto
Mbinu zinazopendekezwa hapa zinategemea utaratibu uliotumika katika tafiti tathmini na zinazojulikana kama pembe tatu. Neno hili hutumika kubainisha nafasi ya eneo au mtu kwenye ramani. Yaani, habari inapatikana inayobainisha mwelekeo fulani. Kwa kujua mahali ambapo mwelekeo umechukua huwezesha mtu kuchora laini kwenye ramani. Kisha mwelekeo kama huo utachukuliwa kutoka mahali pengine. Kama haya yamefanywa safari tatu kutoka sehemu tofauti tofauti, pembe tatu ndogo itajitokeza kwenye ramani. Hapa ndipo mtu au eneo litapatikana.
Katika mijadala na mahojiano, ambayo hufanywa na washiriki wa mijadala na waamuzi kadhaa kuhusu jamii sawa, waelimishaji watakuwa wakinakili hoja kuhusu habari inayopeanwa na chanzo cha habari hiyo. Yaani, wataamua kuhusu habari na mahitaji pamoja na msimamo wa yule anayetoa ile habari.
Kama haya yamefanywa kwa uangalifu, na mijadala kama hiyo imefanywa na watu kadhaa, data kuhusu jamii itaendelea kuwa ya kutegemewa. Itakuwa rahisi kuiweka jamii katika ramani ya data ambayo nyingine itadhibitisha na kupanuka na nyingine itabainisha shauku na mitazamo hasi.
Ilivyotajwa, panaweza kuwa na matatizo. Haya huweza kuthibitiwa iwapo mbinu hii inahusishwa na kukusanya habari kutoka kwa mbinu zingine kama vile utafiti, data iliyopo na makundi lengwa. Inawezekana kutathmini data iliyokusanywa na makundi rejelewa.
Makundi ya Kurejelewa
Waelimishaji wanaweza kubainisha kundi ndogo la Makala kutoka katika mashirika yanayoaminiwa na watu ambao wanaweza kupata habari kutoka kwao ambayo wanaipata nyanjani. Makundi kama haya hukutana kila mara lakini hayana mvuto wa moja kwa moja katika mwelekeo uliopendekezwa wa mpango au matokeo yake yanayotarajiwa.
Njama na kutotegemewa
Kunao wakati ambapo baadhi ya watu na mashirika huwa na mvuto kwamba waelimishaji wana mtazamo fulani wa jamii. Panaweza kuwa na mtazamo kuwa kundi la waelimishaji limepata pesa ambazo zitatumiwa katika jamii. Au kundi la waelimishaji linastahili kuunda mipango kwa njia fulani maalum ambayo hunufaisha jamii au hata chama fulani cha kisiasa. Iwapo kundi la waelimishaji linahusisha watu kutoka nje, huenda hata wasijue kuwa wale wanaowahoji wanakutana na kujadiliana mitazamo ya miradi wenyewe kwa wenyewe.
Njama kama hizi hazistahili kuchukuliwa ili kudunisha ukubalifu wa habari inayotolewa. Watu wanavutiwa kwa kuwa waamuzi au kudumisha hali zao katika jamii. Huenda wasiwe na haja ya kukubali maeneo ya kutojua kwao na wanaweza kuchangia zaidi kwa viwango vyao vya athari ili kuvutia kundi la waelimishaji.
Fikira za kikundi
Kuna uwezekano wa kuwa na maoni kati ya walioteuliwa kuhusu maswala ya jamii ambayo hayawiani na ukweli uliopo. Wakati wa mpito na maafa, kuna madarasa yenye umuhimu kiasi katika mapatano ya ukweli, na mashirika hayawezi kuendelea sawa na madarasa haya.
Pia, kunaweza kuwa na mashirika ya kisiasa yaliyonawiri na maoni ambayo yanachukuliwa kimzaha. Haya yanaweza kuwa ya kweli. Kundi moja huenda likaungwa mkono na wanajumuiya wote. Lakini katika nyadhifa hizi za ustawi, si rahisi kukosa kutokubaliana na kutoweka. Kwa kawaida hali hii huzua kauli ya kutamausha, kwamba wanachama wa miungano yenye tegemeo finyu wanaweza pia kuweka madai kutathminiwa.
Ulindaji lango
Kuna wale ambao ni walinda lango badala ya kuwa viongozi. Wao huongoza fursa ya kufikia ujumbe wa jumuiya lengwa. Wengine wameteuliwa katika jumuiya, ilhali wengine hawajateuliwa. Sababu za huu ulinda lango zinaweza kuwa za kiitikadi, kisiasa au kibinafsi. Timu za kuelimisha zitazua tofauti za ndani kwa ndani ili kuhakikisha kuwa hawawachwi nyuma kwa sababu wote ni waume, au wote ni wa nchi moja fulani au wa utamaduni fulani au asilia moja.
Hii haitazuia ulindaji lango. Lakini maendeleo ya mitazamo kariri yanaweza kutatua hii. Katika jamii za kitamaduni, waelimishaji huenda wakakosa utulivu ikiwa wanataka kupita katika lango kuu. Kuna safu ainati za kutatua hili lakini pengine safu yenye uzito ni uundaji wa uhusiano wenye ukweli pamoja na msuluhishaji ambaye atamwasilisha muelimishaji kwa uongozi wa kitamaduni.
Kutathmini ujumbe
Waelimishaji watatoka kwa hali moja hadi nyingine pale ambapo watashuku ya kuwa ujumbe unaweza kuwa umebadilishwa na wale watakaokuwa wakitafuta watu ambao wana radhi ya kuwa wenye haki kwa maoni yote ya kisiasa na wanaoweza kuonyesha utegemezi wa maoni yao kwa kutoa ushahidi wa ukweli. Au wanawezachagua kuendesha mahojiano ambayo yanahusisha wanachama lengwa kwa asili ya sampuli ndogo, kwa madhumuni ya kuhakikisha badala ya kuendesha utafiti mzima.