Kuna utamaduni mkubwa wa elimu kwa wazee kote ulimwenguni. Historia ya elimu hii ni tofauti kutoka eneo moja hadi jingine lakini huangazia nyuzi mbaimbali.
utaalamu au umeneja, kina cha ongezeko na ubunifu wa kibinafsi, hamasisho la jamii, uwezo wa kusoma na kuandika na nambari na ustawisho wa taaluma mbalimbali. Kutoka kwa urithi huu tunapata mitazamo mbalimbali:
- Tabia za wazee
- Wapi na lini elimu ya wazee hufanyika
- Nani ana uwezekano wa kuhusika
- Jinsi wazee wanavyosoma
- Njia bora zaidi za kuwafunza au, kulingana na wengine, kusaidiwa kusoma
Hata pale ambapo kuna mapendekezo mengine kwamba mitazamo hii hutumika kwa ujumla kwa jinsi watu wanavyosoma, utawala wa shule kama eneo la kimsingi na njia za mafunzo ya kielimu kwa watoto umewacha wazee wenye elimu ya shahada na isiyo rasmi kama maeneo ya utafiti.
Sifa za wazee
Wazee wana sifa ambazo zimejulikana ulimwenguni. Sifa hizi hueleza jinsi mtu anavyokuwa mzee ila si umri wao. Umri uliokubaliwa wa kuwa mzee unaweza kubadilika kutoka jamii moja hadi nyingine- na kuna jamii nyingine ambazo zimerefusha wakati wa kuwa watoto na vijana- na kwa njia hii zimetenganisha sekta kubwa za waliohitimu na elimu kishahada na utafiti wa elimu kwa wazee.
Wazee huchukuliwa kuwa na ujuzi wa mahitaji yao ya kielimu, kuwa wamekua kwa kiasi cha kuchagua iwapo na njia gani ya kupata elimu, kuwa na tajriba ya maisha na kazi hata kuwa na uwezo wa kufikiria na kutumia masomo halisi katika kiwango hiki cha tajriba, kuwa na uwezo wa kuchagua wapi na lini kusoma na kuwa tayari kukidhi gharama ya usomi huo (ikiwa gharama hii ni kwa njia ya wakati, pesa au fursa zilizopotea). Wazee huchukuliwa kuwa na wakati finyu na kuwa na haja ya kusawazisha mahitaji ya familia, kazi na eimu. Pia wanaweza kuchukuliwa kuwa tayari wamepata ujuzi wa wao wenyewe na wa dunia, ambao utatosha kustahimili kila siku ikiwa si kuongoza mazingira kwa matakwa yao wenyewe. Hii ni kusema, wazee hawako katika hali ya akili isiyokomaa au sleti tupu, kwa watu wengine waziandike.
Mafunzo kwa wazee hufanyika wapi?
Wazee huchagua mahali wakotaka kufanyia shughuli zao za kielimu. Wao hupendelea mahali ambapo panawiana na mahitaji yao na kiwango kikubwa cha mafunzo kwa wazee hufanyika katika mahali pao pa kazi au nyumbani au maeneo ambayo wazee wana uhusiano mzuri. Haya huhusisha taasisi za kupata shahada.
Hata pale ambapo maeneo mengine yanaweza kuwa tayari kwa mafunzo spesheli, wazee kwa mara nyingi hutumia maeneo ambayo hutumika kwa sababu nyingine. Elimu kwa wazee hufanyika katika makundi madogo, ingawa kuna ongezeko katika mikusanyiko mikubwa, katika maeneo ya umma na nafasi za elimu za kidini. Pale ambapo miungano ya jamii hijuhusisha na shughuli za elimu,wanaweza kufanya hivi katika makundi makubwa.
Lini Wazee hujihusisha na shughuli za elimu?
Pale ambapo elimu imepangiwa, tofauti na ile isiyo rasmi, kuna uwezekano kuwa elimu hii inaweza kufanyika nje ya masaa ya kawaida ya kufanya kazi. Miradi mingi imewekwa jioni ama wakati wa wikendi. Wazee wanapaswa basi kufanya uamuzi kuhusu kuhudhuria wakati wa matukio kama haya na kubadilisha shughuli nyingine wakati wa wakati wao wa binafsi, ijapokuwa wana uwezo wa kupanga masomo wakati wa kufanya kazi.
Pale ambapo masaa ya kufanya kazi yanatumika, wazee watahitajika kupuuza malipo yao ili wahudhurie. Au sivyo, watahitajika kufanya kazi kwa masaa ya ziada ili kufidia wakati waliokuwa wakisoma. Katika hali kama hii, kuna gharama muhimu hivyo basi wazee wanaohudhuria shughuli za elimu wana motisha nyingi na wana matarajio makubwa.
Miradi ya elimu inayo uwezo wa kurahisisha kuhudhuria, au kupunguza ugomvi wowote unaoweza kutokea na kuhudhuria huku, ina nafasi bora zaidi ya kuvutia kundi kubwa la watu.
Nani wanaohusika na shughuli za elimu ya wazee?
Kuna ushahidi ambao unaonyesha kuwa wazee hufanya programu za kielimu ambazo wamejichagulia katika nyakati teule katika maisha yao. Wale ambao wana tajiriba njema za elimu, haswa katika viwango vya msingi na upili, huenda wakachagua programu za kielimu ambazo ni rasmi.
Wale ambao wanapaswa kuchagua kazi au hata mambo ya kibinafsi, wale ambao wana wakati au wale wanaoelewa kuwa ndoto zao hazitatimizwa bila uwezo wa ziada watashiriki katika programu rasmi. Watu katika mashirika walio na programu za kielimu ambazo zinahusiana na kuendelea kikazi wanaweza kuongozwa kwa programu hizi, lakini si wazee wote wana nafasi hii.
Kwa sababu ya hamu zao za kibinafsi, wazee hawawezi kutarajiwa kuchagua programu za kielimu kwa sababu ziko tu. Wanafaa kuwa na manufaa, lakini manufaa haya si lazima yaambatane na elimu yao. Wale wanaoamini kuwa elimu italeta tofauti katika maisha yao au ya wale walio karibu nao, iwe kwa kutimiza mahitaji teule katika kutatua shida fulani, huenda wahudhurie kulingana na changamoto fulani, wanaweza kushiriki katika shughuli za kielimu ikiwa shughuli hizi hazihusishi kuhudhuria bali kusoma, kutazama na kusikiliza.
Wazee watachagua njia bora zaidi za kutumia nyenzo finyu walizonazo za wakati na pesa. Programu za kielimu zinazourudisha pamoja na kufunza, ambazo zinawafikia watu waliko badala ya wao kulazimika kuhudhuria, na zile ambazo zinahusiana na maisha yao ya kila siku, zinaweza kuwa na matokeo bora zaidi. Lakini waelimishaji hawafai kudharau wajibu ambao watu wengi wanao kwa jamii na kwa manufaa ya kibinafsi.
Wazee husomaje?
Watu hawahitajiki kuhudhuria programu za kielimu ili wasome. Wengi wao wataendelea kusoma kutoka kwa matukio-kwa kufanya vitu wenyewe, kwa kuwatazama wengine na kuiga au kuboresha wanachofanya, kwa kujaribu kitu na zingine zote zinapofeli, ‘kusoma mwongozo’ au kufuata seti za utaratibu zinazoletwa na wale ambao wamekuwa mbele yao.
Wale ambao wanasoma bora zaidi, tofauti na kujirudiarudia, ni wale wanaoakisi wanachofanya na jinsi wanavyofanya. Mitazamo ya akisi hizi hutegemea njia ambazo walivyo katika maisha ya usoni na hii huleta tajriba na mabadiliko.
Kwa wakati mwingi, wazee wamekuwa bora katika kila wanachofanya, ikiwa wana uwezo wa kuleta maana na kuakisi kwa uzoefu wao.
Kuakisi huku wa kinidhamu si rahisi kila wakati, haswa ikiwa uzoefu wao ni wa kiwango cha juu au umejawa na hisia ambazo hukinga yanayotendeka. Pia huenda ikawa hali ambayo watu hawana ujuzi wote uliopo ili kuleta maana ya yanayofanyika. Kwa hakika vizazi ambavyo vinaangaliwa na vinaendeshwa na nyota bila kubadilisha mitazamo yao kuwa ulimwengu ulikuwa katikati ya sayari.
Kwa hivyo, waelimishaji wanasaidia katika kuwapa wazee ujuzi huu utakaowasaidia katika uakisi na kujenga uzoefu wao kwa kusikiza kwa makini na kutoa mitazamo yaliyojengwa na elimu, katika tajriba yao na kwa kuunda nafasi kwa wazee kutofautisha uzoefu wao kupitia kwa mazoezi na uteuzi zenye upungufu, usalama na zilizobanwa, na kupitia kwa masomo yaliyoongozwa na utafiti.
Mhadhara
Ikiwa kusoma kwa wazee kunahusisha kuakisi wa kinidhamu, na ikiwa waelimishaji wana hamu ya kuwasaidia wazee kusoma bali si kufunza tu, mbona basi idadi kubwa ya shughuli za kielimu zinafanana? Nyingi zao huhusisha mihadhara au uwasilishaji kutoka kwa mtu anayekisiwa kuw ana tajriba au ujuzi unaotamaniwa na wale wanaosikiliza.
Mihadhara si lazima ziwe njia mwafaka za kupitisha ujuzi, wala si njia mwafaka ya kuwasaidia watu kupata elimu. Lakini bado mihadhara hii inaendelea kuongoza programu za kielimu. Wazee wote si lazima wategemee wengine ili waweze kupata elimu. Hata pale ambapo wamechagua kuhudhuria mhadhara, kuna uwezo wa kuenda pale na viwango mbalimbali vya ujuzi, elimu, maoni na uwezo ambao wanatumia kutathmini ujumbe wanaopewa. Pale ambapo wanataka ujuzi na ujumbe, mhadhara mzuri unaweza kuwapa hizi kwa njia zinazomwezesha mtu mzima kufanya uamuzi kuhusu uaminifu wa ujumbe – kwa kutathmini majibu ya wengine, kwa kuuliza maswali na hata kutathmini mwenendo wa mhadhiri. Ishara hizi huufanya mhadhara au mazungumzo tofauti na kutazama filamu ya mhadhara huo kibinafsi.
Pale ambapo mtu mzima amepewa upenyo kwa nyenzo na wakati wa majaribu, anaweza kufanya uamuzi na huenda pia wakatambua kuwa mhadhara huleta matokeo ya ujuzi wa kitabia. Lakini waelimishaji hawatataka kutegemea miundo isiyoaminika ya kupitisha ujumbe ikiwa wana uwezo wa kuendeleza tajriba yao ya masomo ili ihusishe mazoezi ya uakisi.
Njia za kusoma
Wazee wana njia tofutti za kusoma. Wengine huona rahisi kusoma kwa kijamii au vikundi vidogovidogo, wengine katika shughuli za kusoma zisizojulikana, wengine kwa kufanya vitu na kujaribu na wengine kuhitaji mafunzo na nyongeza ndogo.
Huku tukizingatia kuwa elimu kwa wazee ni ya hiari na ina wingi wa vipengele, haswa elimu ya mpiga kura na ya kisheria, wale wanaoona mtazamo huu ukiwa wenye kufanana, huenda wakachagua programu inayofaa. Pale ambapo hii haitendeki, wazee huenda wakachagua kutoka kwa programu hii. Programu ambazo zina viungo muhimu kuzihusu zitahitajika kuwiana na njia za wale wanaoshiriki.
Katika kujaribu kufikia idadi kubwa ya wazee katika programu hii, mengi yatahitajika kushirikishwa ili kuruhusu watu kuchagua vipengele vitakavyowawezesha kusoma kwa njia rahisi sana.