Waelimishaji watatumia njia mbalimbali kulingana na utathmini wao wa vile watakavyoafikia malengo yaliyowekwa kwa matokeo ya kuchanganua mahitaji ya kielimu. Hata hivyo, kuna njia tatu muhimu au utaratibu wa aina tatu: matangazo, habari ya umma na elimu, na kusoma kwa makundi.
Njia za muungano
Miradi pana ya kielimu huenda ikatumia utaratibu wote wa aina tatu. Hii husababisha mitindo ya kuvutia kwa vile kila wanaotumia moja wapo wa utaratibu huu hutoa lugha yao, uchukulio wa mpangilio na mielekeo ya kielimu katika jumba a mikutano na kwa mradi.
Elimu ya upigaji kura hutegemea kuwa biashara ya uchaguzi kwa sababu ya aina kubwa ya hadhira na matokeo na matokeo ya kusoma. Hii ni mada ya kiuchaguzi pia kwa sababu lazima ishughulikie nchi mbalimbali na miktadha ya kichaguzi. Kuna wale ambao huamini michakato hii kuwa ya kiushirikiano wa pande zote na wale wanaoona kuwa huleta matokeo fulani ambayo hayakutarajiwa na ambayo huenda yakawa pingamizi kwa maendeleo ya upigaji kura.
Hata hivyo, inaendelea kuwa vigumu kudumisha njia ya kiutamaduni kwa shughuli ya elimu ya watu wazima kama vile elimu ya upigaji kura. Katika elimu ya kisiasa, dhana ya kuwezekana imebakia kutamalaki. Kwa kuongeza kwa hii ya mpangilio, kikundi kinachosoma michakato inayoonekana kukubaliana na inayofaa ya kidemokrasia ya mazungumzo na mijadala-huacha mengi yasiyofurahiwa kwa upande wa viwango. Kutokana na haya huonekana kuegemea kuiondoa miradi ya kielimu hadi mpangilio rasmi ya kishule. Na haya yana changamoto zake. Kwa hivyo inaweza kuwa vyema kuegemea kwa michakato ya matangazo , elimu ya umma na kusoma kwa vikundi kama raslimali ambazo muelimishaji hutoa njia zinazohitajika na ujuzi kuafikia malengo yao kwa njia bora zaidi.
Matangazo
Matangazo huanzisha nembo ya kujitambulisha, kutofautisha bidhaa moja kutokana na nyingine sokoni, na kuwahamasisha wateja kuhusu kuwepo kwa bidhaa au huduma. Mbinu huweza kutumiwa kupitisha ujumbe vizuri. Mbinu moja inayotumiwa hasa katika jamii zinazoona umuhimu wa elimu au kujiendeleza ni kutumia mbinu ya darasa kusisitiza ujumbe. Kutokana na sababu hii, mchakato wa matangazo huteuliwa mara nyingi kwa habari ya upigaji kura na miradi ya kielimu.
Mashirika ya kutangaza yana umuhimu wa ziada katika kuelewa kwao kwa wateja na uwezo wao wa kupata ujumbe kwa wakati mfupi kwa viwango vinavyohitajika vya athari za kitaifa na kubainisha mtindo maalum kwa hadhira lengwa.
Misingi maalum ya mchakato huu ni kuwa huanza na ujumbe unaohitajika kusambazwa na ambao umeundwa kutokana na mradi. Wakati mwingine ujumbe huwa na mahusiano ya moja kwa moja na utafiti wa mahitaji ya kielimu ya hadhira lengwa. Mara nyingi huundwa kutegemea sehemu ya uelewa wa hadhira na sehemu ya malengo ya mradi. Uamuzi huu utaegemezwa kwa uchukulio fulani kuhusu kile ambacho watu wanahitaji ili kushiriki katika uchaguzi. Kwa habari zaidi, tazama Matangazo ya Biashara.
Habari na Elimu kwa Umma
Mchakato wa pili katika kampeni ya kitaifa ya vyombo vya habari hutegemea misingi ya habari ya umma. Hutegemea mbinu za kupitisha habari kwa wengi, ambapo nyingine hutoka katika matangazo ya athari ndogo lakini pia hupuuza mambo mengine kuhusu umuhimu wa taasisi wa mashirika katika maendeleo ya mitazamo na tabia za watu.
Huku kuzingatia kwa mtu katika kikundi kuliko mtu kujitegemea mwenyewe huashiria mambo ya kimsingi katika mradi wa elimu ya umma. Ni kutokana na huku hutegemea kwa kujitambulisha kwa shirika na umuhimu wa mambo ya kimazingira ambao hufanya michakato ya elimu ya umma kufana katika jamii zinazoendelea na katika jamii ambazo huzingatia umoja wa kijamii.
Kusoma kwa makundi
Mchakato huu wa tatu na ambao umetamalaki katika taasisi za elimu rasmi ni ule unaozingatia kusoma kwa makundi katika mradi. Hata ikiwa katika darasa rasmi ambapo kunufaika kibinafsi na usaidizi wa kikundi na utendakazi katika mtindo wa kuelewa kwa wingi au kusoma kwa makundi kwa kawaida katika jamii. Wale ambao huchagua mbinu ya kusoma kwa makundi huzingatia urahisi wake dhidi ya madhara mengine madogo madogo.
Huku mazoezi ya kielimu ya uso kwa uso (tazama Mawasiliano ya Ana kwa Ana) huchukua kutokana na tajriba ya watu wengi na kuna mbinu nyingi za kielimu ambazo zimebuniwa kwa makundi madogo kuwa athari kubwa ya kielimu huonekana kupatikana tu ambapo kuna mijadala ya kila mara kati ya mwelimishaji na kikundi. Na hii huibua mikutano ya kila wakati ya wanaosoma na waelimishaji kuwa ghali isipokuwa pale ambapo taasisi tayari zimejengwa na miradi ya elimu ya upigaji kura inaweza kuingizwa kwenye mipangilio ya taasisi rasmi.
Kwa hivyo wale ambao hufanya kazi ndani ya mchakato hii kila mara huanzisha tajriba ya kielimu ya hali ya juu ya makundi madogo ya wasomaji pamoja na mahitaji ya elimu ya jumla. Kutokana na haya, kusoma kwa makundi hutumika sana kwa makundi maalum na kwa maendeleo ya mbinu rasmi huku elimu ya umma ya kawaida za mbinu za matangazo hutumika kwa wengi.