Kuchagua na kuunda malengo ni mojawapo wa masula magumu kwa walimu hasa wanotengeneza mapendekezo ya miradi inayoshughulikia masuala ya kijamii. (tazama Upangaji wa Bejeti na Ufadhili wa Mpango wa Elimu kwa Wapigakura)
Kwa sababu hii, kuna dhana kuwa kuweka malengo ni ishara ya kiburi na ni vyema suala hili liachiwe wanafunzi wenyewe. Hata hivyo, wanafunzi ambao ni watu wazima wanaoshiriki mazungumzo na mwalimu wanahitaji kuelewa nia ya walimu na matarajio yao wenyewe. Malengo yaliyo wazi yatachangia jambo hili kuafikiwa.
[1]
Katika vikundi vidogo vya usemi kuna nafasi ya malengo kutungwa kwa pamoja. Nafasi hii haipo katika miradi ya kitaifa kwa hivyo lazima walimu watunge malengo kutegemea uelewa wao wa matakwa ya kielimu ya walengwa.
Uundaji wa Malengo
Wandisi wa malengo wanapaswa kukumbuka njia ambazo ni muhimu katika uendaaji na mazoezi ya kielimu. Kuna vifupisho kadhaa vinavyotumika katika mchakato huu. Marie – Louise Stron wa IDASA Afrika Kusini amebuni vifupisho vilivyo muhimu. Malengo ya WARM au YYYY kama tutakavyoyaita hapa ni yale ambayo yanayofaa (Worthwhile), yanayolenga matendo (Action – oriented), Yenye uhalisi (Realistic), na yanayopimika (Measurable). Malengo haya pia yanachangamsha, au kupendeza, kwa kuwa elimu ya watu wazima inapaswa kukumbushwa kuhusu jukumu lake la kukuza na kuwezesha.
Malengo Yafaayo
Malengo yawe yenye umuhimu kwa mwanafunzi , yangemezwe na kufungamishwa na matakwa ya kielimu na nafasi muhimu maishani za wanafunzi. Malengo yaegemezwe kwenye kile mwanafunzi anakichukulia kuwa muhimu wala si kile walimu anakiona kuwa muhimu. Mazungumzo yafanywe kubaini kilicho muhimu (tazama Ujenzi wa Ujumbe)
Wahusika wote watambue ufaafa huu tangu mwanzoni.
Malengo yanayoegemezwa kwenye vitendo
Malengo yatuungwe katika misingi ya mabadiliko katika tabia, maarifa na misimamo. Hata malengo kuhusu ufahamu yaeleze kitakachofanywa baada ya mafunzo na wala is mchakato wa shughuli. Lengo la Shabaha ni kueleza matokeo yanayotabirika kutokana na mchakato wa utechelezaji wa mradi.
Uhalisia wa Malengo
Malengo yakidhia upungufu wa muda, mbinu na rasilmali zilizopo vialiavyolikumba wanafunzi. Utungaji wa malengo yenye uhalisia unahitaji kuwepo kwa ufutanoa wa mambo / shughuli. Walimu hutunga malengo yafaaya na yanayoegemezwa kwenye vitendo ingawa hawayaafikii katika muda uliotengwa au mikakati inayotumiwa haiwawezeshi kuafikia malengo haya.
Uhalisia huwafanya walimu kuwa wakweli. Haifai kutunga malengo na kuanza kulalama kuwa yangefikiwa kama kungekuwa na muda wa kutosha, au kama walimu nyanjani wangekuwa na ujuzi wa hali ya juu, au kama wanafunzi wangekuwa wasikivu au wepesi kuongozwa.
Malengo kadirifu
Kuafikia malengo lazima yawe yanaweza kukadiriwa. Ukadiriaji wa matokeo unahitaji kuchunguza vielelezo vilivyobuniwa wakati wa kutunga malengo. Si rahisi kuthamia wanafunzi na mchango wa mradi ikiwa malengo si kadirifu.
Wandalizi wa miradi hujihusisha zaidi na utathmini wa kijumla wa mchago wa mafundisho, wanafunzi pia wapimwe uwezo wao ingawa zoezi hilo lisipewe utukufu mwingi. Mwangependa kujua ikiwa wanaweza kuamini waliojifunza na kuyatumia katika maisha yao ya kila siku au waendelee n masomo zaidi.
Utungaji wa malengo kubainisha miradi wa kielimu ni muhimu sana. Sehemu hii katika mchakato wa maandalizi huhitaji uangalifu mkubwa na ikiwa inashughulikiwa na kikundi, inaweza kuwa batilifu zaidi. Usahihi wa sehemu hii huufanya mradi mzima kuwa bora. Ukosefu wa usahibi katika sehemu hii ni baraste ya kujikanganya na kupoteza muda.
Maelezo:
[1] Kutokana na haja ya kuelezea mgawanyo wa malengo, moja likifuatwa na jingine, na uhitaji wa kutoa fasili zaidi. Walimu na waandalizi wamebuni katika nyakati tofauti na mahali tofauti njia zao wenyewe za kupanga maneno mbalimbali yapatikanayo katika lugha ya Kiingereza. Kuna uiano wa mikabala ingawa kuangali na tofauti na ni muhimu kuwa wanoshughulika na mandalizi wametambua kuwa wanabuni mipangilio hii kwa manufaa yao yenyewe. Katika nchi ambapo Kiingereza si lugha ya kwanza, mafundishi ya wahamasishaji hukumbwa na ukanganyifu na mafarakano ya tangu mwango kuhusu ikiwa kinachozungumziwa ni kusudi, nia, shabaha, matokeo au madhumuni. Neno lenye maana pana na maana mahususi hutokana na mazoea, uchaguzi na makubaliano ya kimaeneo.