Baada ya mpango kubuniwa, uzingatiwe ikiwa watu wanauamini. Walimu wasichukulie jambo hili kuwa msaha hasa katika hali ambapo wanashinikizwa na uchaguzi. Lazima wahakikishe ujitoleaji kwa kutunza kitabu cha ratiba, kufanya mikutano na kuwasiliamu na kila mtu ambaye amehusika.
Ikiwa mpango huo umebuniwa kwa mchakato wa mashauriano unaojumuisha washika dau mbalimbali bado kutakuwa na wengione ambao hawakuhisishwa katika maandalizi yake. Inawezekana hata wale ambao walihusishwa katika ukusanyaji wa data mwanzoni au utungaji wa malengo kutohusishwa katika sehemu inayohitaji ufundi / ustadi wa kazi.
Ni muhimu kwa watakao dhamini na kutekeleza mradi kujitolea kwa mradi huo na sehemu zake mbalimbali. Kujitolea si jambo la mzaha. Watu wengine huenda wakaondoka, ni vyema kuwa na mikakati ya kujumuisha na kuhamasisha wageni punde tu wanapojiunga na mradi.
Kushikilia Mpangilio kwa Kulegeza katika Utekelezaji
Basi, kwa kuwa mpango kama huo umetengenezwa kwa gharama fulani, na kwa kuwa kuna uwezekano wa kuwa na tatizo la kutojiamini wakati fulani katika utekelezaji wake, patakuwa pia na haja ya kushughulikia kujitolea ili kufanikisha mpango huo. Hili la mwisho ni la kisanaa hivyo basi linahilitaji ustadi wa koanisha uaminifu katika mpangilio asilia dhidi ya uwezekano wa mabadiliko kutokana na makosa katika mradi au mabadiliko katika mchakato wa jinsi mpango huo unavyotekelezwa.
Kuweka Kitabu cha Utekelezaji wa Mradi
Shughuli ya kwanza ni kuanzisha hiki kitabu, kinaweza kupeanwa kwa washikadau na kutumiwa na wafanyakazi kujitambulisha na kuelezea mradi wao kwa washirika na wenza
Kitabu cha aina si la kionyeshe mandalizi ya mradi mzima, lakini maandalizi hayo yanaweza kuonyeshwa kama nyongeza kwa wanaohitaji. Iwe na mpangilio mzuri wa muktadha malengo, mkakati, maelezo machache wanaotekeleza na mashirika. Nyongeza hii inaweza kuwa katika umbo la mabango, chati za kupinduliwa au kutumika katika chombo cha kurushia picha.
Kuaandaa Mikutano Kuhusu Mradi
Kuna aina mbalimbali za mikutano kuhusu mradi inayohitajika.
Shughuli za mwanzo za washika dau ni kuarifu yeyote anayetaka kupata habari mradi huo. Mikutano ya wafanyakazi itawahamsisha wafanyakazi wageni puunde tu wanapojiunga na mradi huo.
Katika sura ya utekelezaji, mikutano itafanyika kutathmini maendeleo ya mradi, kutambulisha vifaaa vipya au kutangaza wafanyakazi wapya na sehemu mbalimbali za firadi.
Mikutano kama hiyo ihusishe mseto wa mawasiliano bora na mashauriano mwafaka. Mikutano ya wafanyakazi ishirikishe mafundisho, maendeleo ya wafanyakazi, na tathmini za kibinafsi; mikutano ya wadau iwe vipengele vya kutoa ripori na kuthibitisha uwajibikaji.
Usambazaji Habari
Katika mradi mkubwa, mikutano haiwezi kuarifu kila mtu mara kwa mara kinachoendelea hasa ikiwa wametawanyika kote nchi. Kuongezea kwa habari zinazotolewa na vyombo vya habari vya kitaifa na kijamii, na ufungamanisho wa mashirika yanayotekeleza mradi, mradi wenyewe unahimizwa kuwa na njia zake za kusambaza habari.
Gharama ya utayarishaji wa makala ya habari itakuwa kubwa ikiwa makala hayo yatakuwa ya hali ya juu na ikiwa ya sambazwa katika eneo kubwa. Hili lizingatiwe ikiwa mradi una nia ya kujitangaza katika eneo kubwa. Hata hivyo ni muhimu kuchapisha makala ya mara kwa mara yanayotota habari kamilifu za mradi.
Teknolojia mpya inarahisisha kuchapishwa kwa makala ya rangi yaliyopangwa na kuharibiwa vyema. Mbinu ya usambazaji ifikiriwe kabla ya uchapishaji. Ni vyema kuandaa makala yanayoweza kutumwa kwa faksi au barua pepe.
Makala kama hayo yanaweza kusambazwa kwa gharama ya chini. Ikiwa walengwa wengine hawana simu, faksi au tarakilishi, nakala moja inaweza kutolewa na kunathilishwa ili kupata nakala za kutosha kusambazwa kwa mashirika au watu binafsi walio na ushiriki katika mradi husika.
Kuanzisha Tovuti
Mtandao hutekeleza majukumu mawili, kupasha umma habari na walimu na wenza wanoshiriki katika utekelezaji wa mradi kupata habari za kiufundi wanazohitaji.
Mtandao unahakikisha habari zinazobadilika mara kwa mara na hati kubwa ( sheria za uchaguzi) ziwapatikana zinapohitajika na si lazima zilifhadhiwe au kutafutwa afisini nchini kote.
Kutambua thamani ya Umma
Kudumisha ujitoleaji kwa mradi kuna maana ya kujenga imani K+K umma and kuidumisha. Kuafikia hili lazima watu waone kuwa kuna shughuli zinazoendelea hata kama mradi liauwafikii. Vyombo vya habari kupeperusha habari zao kunazidisah ummarufu wao.
Baada ya kutambua thamani ya umma ni vyema kuikuza kupitia kwa vyombo vya habari, sherehe, mikutano mikubwa ya umma na kuzitangaza.
Hata hivyo mradi hauwezi kutegemea thamani ya umma ikiwa mradi lazima ufikie watu mahali walipo. Shughuli zinazohusisha umma zinaweza kuleta madhara ikiwa hazikupangwa vyema. Mikusanyiko iwepo kutokana na shughuli za mradi na wala si kabla au badala ya mradi.