Maeneo ya kupigia kura yanatoa nafasi ya dakika za mwisho ya kupata habari kwa wale ambao hawakuipata katika njia zingine. Wakati ambapo habari zinazoweza kutolewa zinaweza kuwa finyu, uzingativu unafaa kuwepo ili kutumia nafasi hii ya kupunguza gharama.
Wapigakura wanaweza kuwa wamekumbana na Mpango wa utoaji elimu wakati kabla ya uchaguzi. Kutoka kwa Mpango huu, wanaweza kuwa wamepata tu ujumbe kuwa wanafaa kujisajili kama Wapigakura na kuwa waende katika eneo la kupigia kura siku ya uchaguzi. Uamuzi utafaa kufanywa kuhusu ikiwa eneo la kupigia kura lenyewe, aidha kabla au baada ya uchaguzi, litatoa habari za dakika ya mwisho kwa Wapigakura. Kwa kuwa elimu hii huenda ikatolewa, ikiwa tu kupitia kwa wafanyikazi wanaosimamia foleni na kuhakikisha kuwa watu wana nyaraka au hati zifaazo tayari, ni muhimu kufikiria kuhusu njia ambazo haya yanaweza kufanyika kwa ufanisi.
Habari zifuatazo hutolewa kwa Wapigakura wanaowasili katika kituo cha kupigia kura:
Habari za Kimsingi
- mahali palipo na mlango wa kuingilia katika eneo la kupigia kura
- mahali palipo na orodha ya Wapigakura ambayo imebandikwa kwa umma ili kuwasaidia Wapigakura kujua ni eneo lipi la kupigia kura ambalo wametengewa (hasa pale ambapo pana maeneo kadha ya kupigia kura katika mahali pamoja)
- mahali pa kupiga foleni
- iwapo kuna mahitaji yoyote ya kiusalama ambayo watahitajiwa kuyazingatia
- mahali pa kupata viburudisho (vyakula na vinywaji) na huduma za choo au msala ikiwa foleni ni ndefu
- muda ambao watahitajika kusubiri
- nyaraka ambazo watahitajika kuonyesha ili kuthibitisha kufuzu kwao kupiga kura
- huduma ambazo watatarajia kupata kutoka kwa wafanyikazi wa uchaguzi
- mahali pa kutokea kwa foleni
Pia itakuwa muhimu kutoa au kuweka alama au ishara zinazohusiana na uegeshaji kwenye kituo.
Habari za kimsingi zinaweza kujalizwa na habari zaidi kama vile:
Habari Zaidi
- mpangilio wa eneo la kupigia kura
- majina na majukumu ya tume ya uchaguzi katika eneo hilo
- orodha ya wengine wanaoruhusiwa katika eneo la kupigia kura kama vile wachunguzi wa uchaguzi, wawakilishi wa vyama au wagombezi, majarida, makamishna wa uchaguzi na walinzi/watoa usalama
- orodha ya vyama na/au wagombezi wanaoshindana katika uchaguzi
- muundo wa karatasi ya/za kupigia kura na maelekezo ya jinsi ya kutia alama ya kutambulisha chaguo la mtu kwa njia sahihi
- utaratibu wa kutumia kuomba usaidizi au kushughulikia karatasi la kupigia kura lililoharibika
Habari hizi zinaweza kujalizwa na habari za kijumla zaidi kuhusu ngazi za uongozi ambazo zinapigiwa kura, huduma zinazotolewa na ngazi hizo za serikali, jinsi matokeo ya uchaguzi yataathiri uundaji wa serikali. Mambo haya ya kijumla yanaweza kuleta tofauti kwa uwezo wa Wapigakura wa kutengeneza chaguo lenye maana na mantiki na kupunguza shuku na ukosefu wa usalama kuhusu uchaguzi huo.
Hali ya Uchaguzi
Namna ambavyo habari hizi zote zitatolewa inafaa kufikiriwa kwa makini ili kuhakikisha kuwa zinaweza kufikiwa, ni wazi, zenye maana na hazipendelei hata kidogo. Kubandika tu mabango kwenye ukuta kwa sababu kuna wingi wa mabango kama haya haitoshi na hakika itakuwa hasara.
Baada ya eneo la kupigia kura kuandaliwa katika hali ifaayo, wafanyikazi wa uchaguzi watataka kutoa mahitaji ya kimsingi au muhimu ya habari kwa Wapigakura.
Upangaji
Wakati ambapo wafanyikazi wote wa uchaguzi wanafaa kuendesha shughuli zao katika eneo la kupigia kura katika hali ambayo inaeleweka kwa umma, kunaweza kuwa na wale ambao wana jukumu maalum katika kutoa habari, aidha kwa Wapigakura wote au kwa wale ambao wataomba usaidizi.
- Jukumu la wafanyikazi wa uchaguzi
Miongoni mwa majukumu yanayotarajiwa ya wale ambao wanatoa habari kwa Wapigakura ni wakaribishaji na waangalizi wa foleni. Watu wa aina hiyo watasaidia katika kuelekeza Wapigakura kwenye foleni na kutoka kwenye foleni hadi kwenye milango ya eneo la kupigia kura. Pale ambapo foleni ni ndefu, wanafanya mipango ya kuwashughulika Wapigakura wakongwe auwalemavu. Pia wanaweza kusaidia kuandaa watu kupiga kura kwa kuangalia kuwa wana nyaraka sahihi, kwa kujibu maswali kuhusu mchakato wa kupiga kura, na kuwahimiza Wapigakura ambao wanaonekena kutojiamini.
Wafanyikazi kama hao wanafaa kupewa mafunzo zaidi kuhusu elimu kwa Wapigakura zaidi ya ile ambayo hutolewa kwa wafanyikazi wengine wa tume ya uchaguzi katika maeneo ya kupigia kura. Mafunzo haya yanafaa kujumuisha uzingatiaji kwa undani masuala ya kisiri, usiri wa kura, na suala la kutopendelea / kutoegemea. Haya yote yanafaa kuzingatiwa kwa makini sana hasa katika maeneo ya kupigia kura sio tu kwa madhumuni ya kuhakikisha shughuli nzuri ya upigaji kura kwa mtu binafsi bali pia kuweka tume ya uchaguzi ya eneo na mchakato wa upigaji kura katika hali ya kutokuwa na shuku.
Ndani mwa eneo la kupigia kura, wale ambao wanaomba usaidizi katika upigaji kura au walio na maswali kuhusu hali moja au zaidi ya utaratibu wa upigaji kura wanaweza kusaidia tu ikiwa mipango ya awali imeandaliwa kuhusu usaidizi kama huo katika sharia na kanuni za uchaguzi. Hapo uamuzi utafanywa kuhusu ni nani atakayetoa usaidizi kama huo na njia zipi zitatumiwa kufuatilia usaidizi wao ili kuhakikisha kuwa unaweza kueleweka kwa uwazi kama msaada na habari zinazohusu taratibu na wala sio kutaka kujua ni nani ambaye mtu huyo anaweza kupigia kura au kuwashawishi kupiga kura kwa njia fulani.
Mipango ya elimu kwa Wapigakura itafanya kazi na afisi au idara zinazowajibikia maandalizi ya eneo la kupigia kura ili kuhakikisha kuwa alama zilizo katika eneo la kupigia kura zinatoa habari zilizoelezwa na kanuni. Kwa sababu ya haya, mijadala inafaa kuanza kwa mapema zaidi iwezekanavyo katika shughuli za uandalizi wa uchaguzi. Baada tu makubaliano yameafikiwa kuhusu ni nini kilicho bora zaidi na ni nini kinachokubalika, wale wanaopanga muundo na mpangilio wa maeneo ya kupigia kura na kutoa habari kwa maafisa wanaosimamia uchaguzi kuhusu namna ya kuandaa maeneo ya kupigia kura wanafaa pia kuzingatia haja ya habari na uwezekano wa eneo wa kutoa tajriba ya kielimu.
Mabango au mabandiko yanayoonyesha taratibu za upigaji kura yanaweza kuandaliwa na kuonyeshwa nje ya eneo la kupigia kura, au hata yanaweza kubandikwa kwenye vibanda vya kupigia kura. Alama kwenye madawati zinaweza kutaja si jina pekee la dawati hilo (kwa mfano, Orodha ya Wapigakura) lakini pia inaweza kuonyesha au kueleza kwa uwazi ni nini ambacho mpiga kura anahitajika kufanya kwenye dawati hiyo.
Kwa mara nyingine, alama / ishara zinafaa kuwa na athari ya kijumla, na uzingatifu unafaa kufanywa ili kuzibandika katika maeneo yafaayo na kuyatengeneza katika viwango vifaavyo (Tazama Mabandiko na Mabango). Habari nyingi zaidi inaweza kukanganya, hasa iwapo itatazamwa na watu wengi zaidi wenye viwango tofauti vya elimu.
Katika hali ambapo haiwezekani kutuma habari kupitia kwa barua pepe hadi kwa Wapigakura ambayo inawasaidia kujiandaa kupiga kura, au pale ambapo habari zaidi zinahitajika katika dakika ya mwisho, inawezekana kuandaa na kusambaza vijitabu kwa watu wakati wanaingia kwenye foleni ili kupiga kura. Habari kama hizo zinaweza kurudia zile ambazo zimebandikwa, zinazotoa habari za kimsingi kuhusu taratibu za kupiga kura na kuhusu mpangilio wa eneo la kupigia kura. Zinaweza kuorodhesha haki za Wapigakura, zinaweza, au kijitabu kama sawa na hicho kutolewa baada ya kupiga kura, ili kuwashukuru watu kwa kujitokeza kupiga kura.
- Vifaa (vya kimaandishi) vinavyotolewa kabla na baada ya kupiga kura
Wakati mpiga kura anapoondoka, vifaa vinavyotoa habari zaidi kama vile wakati ambapo matokeo yatatangazwa, jinsi ambavyo kura zinabadilishwa na kuwa viti (nyadhifa) au habari kuhusu serikali vinaweza kutolewa. Hizi ni baadhi ya nafasi chache kwa serikali au mamlaka ya kusimamia uchaguzi kuhakikisha mawasiliano na Wapigakura wengi zaidi, kama sio wote, hasa katika nchi zinazoendelea.
Mawasiliano na Wapigakura kwa kawaida yanaweza kuwa finyu bila kujali undani wa Mpango wa elimu. Kutokana na haya, inaweza kuwa watu wanakuja katika maeneo ya kupigia kura wakiwa na maswali ambayo hayajajibiwa. Ni jambo linalowezekana kutumia wakati ambapo watu wanakuwa katika foleni ili kukamilisha habari kwa Wapigakura na kutoa huduma kama vile ukaguzi wa orodha ya Wapigakura.
Huduma kama hizo zinaweza kutolewa kwenye madawati ya habari nje ya maeneo ya kupigia kura. Madawati haya yanaweza kuwekwa kwenye kingo/pembe za maeneo au yanaweza kukubaliwa katika mahali jumla pa uchaguzi. Huenda yakahusisha nakala za orodha za Wapigakura na orodha za maeneo jirani ili watu walio mahali pasipofaa wanaweza kuelekezwa upwa. Madawati hayo pia yanaweza kuwa na wafanyikazi ambao wanaweza kuendesha warsha na maonyesho ya hapo kwa hapo kwa watu binafsi na makundi ya watu.
Kama mipango inayohusu taratibu na kushiriki kwa mashirika ya kupigania haki za kijamii ya kujitolea yatakubali huduma kama hizo, ujumbe kuhusu elimu kwa Wapigakura ya dakika za mwisho unaweza kuwahimiza watu kufika katika maeneo ya kupigia kura ambapo watapata usaidizi. Katika hali hii, wakati mwingi na nguzu nyingi kwa upande wa Wapigakura na waelimishaji utaokolewa. Hapa ni mahali ambapo Wapigakura watafurahia kuwa, pale ambapo watapewa motisha ya kujifunza, na pale ambapo ni nini ambacho wanataka kujifunza. Jitihada chache zaidi zinaweza kujitokeza kuwa za kufaa zaidi, na kuwaelekeza watu kwenye habari zaidi.